Mipango miji na usafiri Dodoma

Mipango miji na usafiri Dodoma

Kwa akili hizi za mpanuko wa miji ndio hutuletea shida. Huwezi kutumia masaa 4 kutoka Dar mpaka Dodoma na unataka kuunganisha Babati, Iringa Singida etc Uje uzuiwe masaa mawili kwenye kuunganishwa.

Miji yote mikubwa iliyopangiliwa inaangalia hili. Tutalitambua hili tumeshachelewa tuishie kubomoa majengo na kuharibu miundo mbinu. Ikiwezekana iwekwe provision ya city railways kuunganisha Uwanja wa ndege, Uwanja wa mpira, Stend za mabasi, mji wa serikali ili tuwe na mji wa mfano uliopangika na wenye usafiri wa uhakika.
Mimi nadhani wenye ma bus ndio wanatakiwa kujiongeza sio kila kitu mpaka wafikiwe, wanatakiwa kuna na mawakala wao pale kuwahudumia abiria ambao wanataka kusafiri na ma bus yao kuunganisha safari wewa Dar na Dom hili litasaidia na wao kupanga ratiba zao kuendana na Train. Lakini kama suala la umbali tu wa SGR na Bus Stand mimi nadhani hili halina solution sababu ukipelekwa wewe stand au wachache mpelekwe kuna abiria wengi wanashuka Dom wataingia usumbufu kama huo kulipa nauli kwenda makwao, kama mbali kwako basi ni mbali kwa wengine pia.

Stand Ya Magufuli Dar ni karibu kwa watu wa Kimara, Mbezi mpaka ubungo na sehemu zingine lakini ni mbali sana kutoka Mbagala, Kigamboni..... Na pia inachangamsha uchumi watu wanapata kazi.
 
Mji hauwezi kupanuka kama mtakusanya vitu vyote sehemu moja. Sasa toka SGR lazma kuwe na tax, boda au bajaji ili uende sehemu nyingine.

Hata stendi ya Morogoro iko mbali na ya SGR
Hapo niliichona ni kukosekana kwa usafiri wa daladala kati ya stesheni na stend.
 
Sio lazima view karibu,ila kuwe na mawasiliano ya kueleweka! Unaifahamu Dodoma?mleta hoja yuko sahihi!Dodoma kulikuwana na CDA ila hawakuwana akili Kabisa....Kwa mamuzi ya Jiwe kwenda Dodoma....kama mji ungekuwa umepangwa kwa akili ...
DODOMA Ingekuwa bonge la Jiji!
Kilichokosekana ni RELIABLE PUBLIC TRANSPORT ndani ya mji. Sio suala la hizo stations kuwa karibu, haziwezi kukaa karibu popote pale.
 
Jana nilisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Singida. Nikaona nitumie usafiri wa Treni mpaka Dodoma asubuhi kisha niunganishe bus kutoka Dodoma kuelekea Singida.

Nilifanikiwa kufika mapema Dodoma kwa treni. Dhahama ikaanzia nilipofika kituoni kutafuta usafiri wa kwenda kituo cha mabasi cha nanenane ambacho kipo umbali wa km 8 kutoka kituo cha treni maarufu sgr.

Swali lilipita kichwani lilikua hivi kuna mawasiliano ya mipango miji wakati wa ujenzi wa vituo hivi. Kwanini havikuwekwa karibu na kama si pamoja. Muda, usumbufu na fedha inayotumika kwa msafiri ingefanya mambo mengine ya msingi.

Je kuna wakati watakuja wataalam waseme walikosea kisha waweke city train ili kuunganisha stendi ya bus na sgr? Wabomolee watu na kulipa fidia.?

Ni vyema tujitafakari kama nchi na utaalam wa wanaofanya kazi za usanifu miji, mipango miji na watoa maamuzi ili tusije kutukanwa na vizazi vijavyo.

Ili la umbali wa kituo cha sgr Dodoma na nanenane stand liangaliwe na kufanyiwa kazi.
Wanaoelekea Singida na Tabora unaende kupandia stend bubu Kizota
 
Inawezekana kwa mawazo yako unaona wamekosea ila wao ktk jicho la kiuchumi wamewaza mbali izo km 8 kuna watu wa bodaboda, bajaji, taxi na hata daladala watafanya biashara na itachangia kukuza uchumi, shida yetu tunapenda unafuu nafuu ktk kila kitu bila kuangalia suala la uchumi wasafirishaji watafaidika vp

Treni yenyewe umepanda kwa bei ya chini nusu ya bei ya bus kulipa elf5-10,000 kupanda tax au bajaj nako inakua shida
Njia rahis panda basi uende moja kwa moja adi unakoenda
Swala ni muda. Na urahisi. Kama ni swala la uchumi marching guys wangeruhusiwa wauze karanga uwanja wa ndege. Waunganishe miundo mbinu. Italeta maana kupunguza muda wa safari.
 
Kilichokosekana ni RELIABLE PUBLIC TRANSPORT ndani ya mji. Sio suala la hizo stations kuwa karibu, haziwezi kukaa karibu popote pale.
Kwa sababu ya shughuli na misafara ya viongozi ni kawaida kusimamishwa muda mrefu ikisubiriwa ipite
 
Back
Top Bottom