Mimi nadhani wenye ma bus ndio wanatakiwa kujiongeza sio kila kitu mpaka wafikiwe, wanatakiwa kuna na mawakala wao pale kuwahudumia abiria ambao wanataka kusafiri na ma bus yao kuunganisha safari wewa Dar na Dom hili litasaidia na wao kupanga ratiba zao kuendana na Train. Lakini kama suala la umbali tu wa SGR na Bus Stand mimi nadhani hili halina solution sababu ukipelekwa wewe stand au wachache mpelekwe kuna abiria wengi wanashuka Dom wataingia usumbufu kama huo kulipa nauli kwenda makwao, kama mbali kwako basi ni mbali kwa wengine pia.Kwa akili hizi za mpanuko wa miji ndio hutuletea shida. Huwezi kutumia masaa 4 kutoka Dar mpaka Dodoma na unataka kuunganisha Babati, Iringa Singida etc Uje uzuiwe masaa mawili kwenye kuunganishwa.
Miji yote mikubwa iliyopangiliwa inaangalia hili. Tutalitambua hili tumeshachelewa tuishie kubomoa majengo na kuharibu miundo mbinu. Ikiwezekana iwekwe provision ya city railways kuunganisha Uwanja wa ndege, Uwanja wa mpira, Stend za mabasi, mji wa serikali ili tuwe na mji wa mfano uliopangika na wenye usafiri wa uhakika.
Stand Ya Magufuli Dar ni karibu kwa watu wa Kimara, Mbezi mpaka ubungo na sehemu zingine lakini ni mbali sana kutoka Mbagala, Kigamboni..... Na pia inachangamsha uchumi watu wanapata kazi.