Mipira ya mbali

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Posts
5,329
Reaction score
5,024
Wasalaam,

Ukifanya kauchunguzi kadogo kwa familia nyingi zenye uchumi imara (achana na accidental millionaires), utagundua kuwa ni mipira ya mbali iliyopigwa au kuchezwa na watangulizi wa familia hizo. Mipira ya mbali huchezwa na wajasiriamali wachache sana hapa duniani.

Kwetu hapa ni wachache mno wanaocheza mipira ya mbali, ndo maana utasikia mzee aliondoka na mali zake.

Ugumu wa mipira ya mbali uko hapa, sio rahisi kwa kapuku kuwekeza ili aje apate mavuno makubwa baada ya miaka kumi na kuendelea, kwanza anafikiria ataishije mpaka kufikia hiyo siku.

Pili, yasiyo julikana hapa kati kati ni mengi mno. Kwa hiyo lazima mmoja ktk familia ageuke daraja ili wengine wavuke, je unaweza kuwa daraja la wenzako ili wajukuu watoboe?? Kama huwezi basi cheza mipira ya pasi fupi fupi tu.

Kama unafikiria kucheza mipira ya mirefu au mbali lazima ujipange vizuri kichwani zaidi ili usije ukahamishwa kwenye reli, ufanye utafiti wa kutosha juu ya investment yako katika kona zote usije angukia pua baada ya mabadiliko ya tabia nchi, au sera au technology kukupitia.
 
Ni kweli kabisa, ila ukiwa financially educated ni rahisi sana katika karne hii kuzalisha utajiri wa vizazi na vizazi ndani ya 10-15 years.

Kwa mfano kujenga mradi wa real estate kuzalisha positive cash flow ili deni lilipwe ndani ya miaka 15-30 inamaanisha vizazi vyako vitakuja kumiliki hiyo property ikiwa haina debt-free na bado ikiwa na positive cash flow.

Sasa unakuta mtu kakopa pesa anaeda. Kujenga nyumba ya kuishi nje ya mji akifa watoto wanauza nyumba kutokana na migogoro na matatizo ya kifedha.
 
Generational wealth ni ngumu sana katika nchi zetu za Africa
 
Shida pia hatuwaandai watoto na wajukuu zetu ipasavyo kuja kutuliza hiyo mipira ya mbali na kuendelea na mchezo kuelekea mbele.

Ukichunguza vizuri kwa waliofanikiwa katika gemu hili wapokeaji wa hiyo mipira huanza kuandaliwa mapema sana. Sisi hilo ni nadra kutokea ndiyo maana mwenye mashuti yake akiondoka na mpira unaishia hapo hapo maana hakuna anayejua mbinu za upigaji wa mashuti yale kiundani.

Inabidi tuige kwa Wahindi...
 
Generational wealth ni ngumu sana katika nchi zetu za Africa
generational wealth ndo itakayotuokoa kama jamii, inawezekana, shida hatujaamua. Familia hata hazijui kama kuna haja ya generational wealth.
 
Maadamu wewe , na mimi na mwingine tunajua cha kufanya basi tuwaambie marafiki zetu, katika kumi tutakaowaambia pengine mmoja ataelewa somo na atafanya. Huyu atakuwa roll model kwa wengine na hivyo tutakuwa tumepiga hatua kubwa.
 
Una hoja nzuri ambayo ingekuwa na wachangiaji wengi sana.Changamoto ni lugha uliyoitumia.Mara mipira.Mara pasi.Andika lugha nyoofu.
 
generational wealth ndo itakayotuokoa kama jamii, inawezekana, shida hatujaamua. Familia hata hazijui kama kuna haja ya generational wealth.
Familia nyingi,mtu akiwa mtumishi anawaza tu kukopa na kujenga nyumba na akijitahid kanunua gari..hapo anajiona kamaliza.

Anashindwa kuwaandalia mazingira watoto wake hapo baadae...anajiwazia yeye..watoto wanasomeshwa tu halafu na wao wanakuja kuhangaika kutafuta kazi.. cycle inaendelea hvyo.

Sijui wazazi ni wabinafsi ama ni kukosa elimu??
 
Kuna kitu nilijifunza sehemu fulani, ni tatizo kwa wengi. Kitu hicho ni hiki hapa; "kitu gani mtoto anasikia pale nyumbani au anaona nini pale nyumbani kwa wazazi au ndugu wa karibu"
Kama mtoto anasikia baba na mama wanazungumzia kununua kiwanja Kariakoo leo hii, huyu mtoto anajengewa uwezo wa kufikiri mambo makubwa maana mtoto mwingine anaambiwa K/koo hakuna viwanja aende Chanika. Mtoto aliyevalishwa power bank, ujue ndo yatakuwa maisha yake, yaani bila power bank hakiendi kitu. Nikija kwenye hoja yako, hawa waajiriwa wengi wametokea kwenye familia hizi hizi za kuridhika na ajira na wengi tupo hapo. Watoto tunawaambia, ukifeli utaenda kulima, kwa hiyo mtoto anajua kulima ni adhabu ya walioshindwa shule. Je kulima ni adhabu? Ukifeli nakurudisha kijijini, je kijijini wanaishi walioshindwa shule??
 
Kuna haja ya kuwaandaa watoto mapema aisee.
Mtoto wa leo lazima ajue anakokwenda mapema kabisa, siyo kamaliza chuo ndo ajue pa kwenda ujue tayari hilo ni tatizo. Akikosa ajira rasmi, na mtaji huna unaanza kumlaumu Samia.
 
Mtoto wa leo lazima ajue anakokwenda mapema kabisa, siyo kamaliza chuo ndo ajue pa kwenda ujue tayari hilo ni tatizo. Akikosa ajira rasmi, na mtaji huna unaanza kumlaumu Samia.
Absolutely true.
 
Umasikini bado ni tatizo kwenye familia zetu. Hao tunao walaumu unakuta yeye tu kwenye ukoo mzima ndio angalau ana unafuu wa maisha.

Hivyo anapoanzisha familia yake bado majukumu ya ndugu wengine kwenye ukoo yanamtoa kwenye reli ya kutengeneza maisha bora kwa familia yake mwenyewe.

Wazungu wa amerika magharibi, west na central Europe wameweza kufanikiwa kwa sababu hawana attachment na extended family.Kwao wanajali familia zao tu. Baba, mama watoto basi. Wajomba na mashangazi ni mazungumzo tu tena kwa nadra, hawana mambo ya mizinga na michango ya harusi.
 
Sijui wazazi ni wabinafsi ama ni kukosa elimu??
Wazazi sio wabinafsi na sidhani kama elimu ni tatizo hapa. Mfumo unataka hivyo, wote hamuwezi kuwa bilionea.
Anashindwa kuwaandalia mazingira watoto wake hapo baadae...anajiwazia yeye..watoto wanasomeshwa tu halafu na wao wanakuja kuhangaika kutafuta kazi.. cycle inaendelea hvyo.
Kwa huku Africa, hususani TZ, unaweza kutaja familia moja au mbili zenye utajiri endelevu kwa vizazi ambao haukuhusika na namna yoyote ile ya dhulma au shirki?

Kwamba hakuna unufaikaji wa kinafasi serikalini au namna yoyote isiyo halali?

Na ili utajiri huo udumu kwa vizazi, ni lazima wizi, dhulma, shirki n.k vipasishwe kwa wanaorithi mali hizo sio?

Hii ni kama uongozi tu, wengi wanakuwa karibu na waridi, kunukia inakuwa ni kawaida.....Magu alifikaje juu pale, ni jambo la kujifunza!
 
Ndio kama NHC NSSF na Wananchi HOUSING ni mashirika ya serikali wakamwaga fedha DSM halafu kuja JPM anasema nahamisha mji.
Ni muhimu kutathmin but ukiamua amua tu.
 

Maisha sasa yamebadilika sana. Huwa nawaza kama sasahivi 80% ya graduates wanaomaliza wanakosa ajira, je miaka 20 ijayo hali itakuwaje? Yaani kama una mtoto mdogo sasahivi na unawaza aje kuajiriwa miaka 15 - 20 ijayo aisee hali itakuwa mbaya
 
Maisha sasa yamebadilika sana. Huwa nawaza kama sasahivi 80% ya graduates wanaomaliza wanakosa ajira, je miaka 20 ijayo hali itakuwaje? Yaani kama una mtoto mdogo sasahivi na unawaza aje kuajiriwa miaka 15 - 20 ijayo aisee hali itakuwa mbaya
Kabisa mkuu,bahati mbaya Maisha yamebadilika ila sisi binadamu hatutaki kubadilika..tumekariri tu kusomesha watoto ili waajiriwe baadae.
 
Una hoja nzuri ambayo ingekuwa na wachangiaji wengi sana.Changamoto ni lugha uliyoitumia.Mara mipira.Mara pasi.Andika lugha nyoofu.
Mbona ameeleweka vizuri tu,kama Mimi nimemuelewa mno,na mfano aliotumia ni sahihi kabisa,mipira ya mbali ni wachache ambao wanaweza kuipiga ,kwanza inahitaji mtu mwenye roho ngumu, asiwe muoga,awe na maono,awe mthubutu, awe jasiri, asiyekubali kushindwa, maana yake ni mtu kubuni au kufikiri kuanzisha kitegauchumi kikubwa ambacho kitakuja kunufaishsa vizazi vijavyo,haijalishi yeye atakuwa yupo au hayupo,na wanaocheza pasi fupi fupi Hawa ni wale wanaofanya uwekezaji WA muda mfupi hataki kusubiri ,faida yake anataka aione Leo au kesho na si vinginevyo,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…