Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Meatu:Wakazi wa vijiji sita katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu wameanza kunufaika na huduma ya uhakika ya maji baada ya miradi ya maji iliyokuwa ikitumia nishati ya mafuta kubadilishwa na sasa kutumia nishati ya umeme.
Mabadiliko hayo yameelezwa leo Aprili 16,2025 na Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (Ruwasa) mkoa wa Simiyu, Mhandisi Emanuel Luswetura, aliyesema kuwa hatua hiyo imelenga kupunguza gharama kubwa zilizokuwa zinatokana na ununuzi wa mafuta pamoja na matengenezo ya mara kwa mara ya injini za dizeli.
"Miradi hii ilikuwa inatumia gharama kubwa kuendesha pampu kwa mafuta, lakini sasa kwa kutumia umeme na tumeunganisha ule umeme wa gridi ya taifa tumeweza kupunguza gharama za uendeshaji, ”amesema.
Amesema kuwa watahakikisha wanaendelea kusimamia ubora wa miradi ya maji ili kuzingatia thamani ya fedha ili wananchi wapate huduma kwa wakati.
Miradi ya maji ya vijiji vilivyonufaika na mabadiliko hayo ni pamoja na Sangaitinje,Nkoma, Sakasaka,Ng’hoboko, Mwamalole na Mwangudo
Yohana Jagadi mkazi wa kijiji cha Sangaitinje anasema kuwa kabla ya maboresho hayo, wananchi walikuwa wakilazimika kutembea zaidi ya kilomita tano kufuata maji, lakini sasa huduma inapatikana karibu na makazi yao.
"Ilifika mahali tulikuwa tunachangia mafuta ya pampu kama jamii ili tu tupate maji, lakini sasa hali imebadilika,tunaomba miradi mingine nayo ifikie hatua hii," amesema.
Paulina Ntobi, mkazi wa kijiji cha Sakasaka amesema kuwa huduma ya maji kwa sasa ni ya uhakika na imesaidia akina mama kuokoa muda ambao awali ulitumika kutafuta maji umbali mrefu.
“Kwa sasa sihitaji kuamka saa kumi alfajiri kwenda kisimani,maji yapo karibu na nyumbani na ni salama kwa matumizi,” amesema.
Ruwasa imeshirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kufikisha umeme kwenye vituo vya miradi hiyo na kuweka miundombinu ya kisasa ya kusukuma maji, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kuboresha huduma za maji vijijini kupitia matumizi ya teknolojia rafiki kwa mazingira.