Miradi mikubwa inayojengwa kasi imepungua sana, huko mbeleni tutaambiwa gharama zimeongezeka mara dufu

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mradi wa Mwalimu Nyerere wa umeme, Barabara za mwendokasi, Mradi wa umeme Rusumo na daraja la Busisi speed yake imepungua Sana. Lakini pia usimamizi wa Wizara na idara za serikali si wakuridhisha. Mradi unavyochukua muda mrefu ndivyo gharama uongezeka. Niwaombe JMT tukimbizane imalizike Kwa wakati .

Lakini pia nimpongeze Mhe. Rais Kwa kupata fedha za mwendokasi awamu ya sita. Natamani kuona barabara inayotoka mjini kwenda airpot to Chanika inapewa kipaombele Kwa Sasa Kwa Sasa itasaidia kisarawe kupanuka, itasaidia kufungua milango ya biashara ukanda huo na kukuza Pato la mwananchi na Taifa
 
Kila mradi wa serikali huwa inachelewa na gharama.lazima ziongezeke kwa sababu za riba..

Mitajie mradi ambao umechelewa vs schedule.Kwa mradi wa umeme Bunge lilishaambiwa umechelewa kwa zaidi ya siku 300 kulingana na ratiba,sababu zingine sio lazima zikawa za serikali bali covid na hali ya hewa.
 
Awamu ya 6 imekataa pesa na kodi za dhuluma.

tunajenga kwa pesa halali lbd ndio maana unaona speed imepunguwa

Dhuluma inamwisho mbaya
Pesa tunazo nyingi Sana shida yenu mnashindia pono badala ya kutafuta habari za uhakika.

Kwa taarifa yako,hadi mwezi January Wizara zinazotekeleza miradi mikubwa zimepokea wastani wa 50% ya bajeti zao,kinyume na miaka ya nyuma ambapo utekelezaji wa bajeti ulikuwa haufiki hata 75%.Mfano wizara ya ujenzi hadi sasa ina 55% .

Sekta ya ujenzi niliko mimi hadi sasa utekelezaji wa bajeti tuko 60%,haijawahi tokea,waulize wakandarasi watakupa majibu zaidi.
 
Yaani nakwambia awamu hii ni miujiza tu inatokea.
 
Pesa tunazo nyingi Sana shida yenu mnashindia pono badala ya kutafuta habari za uhakika.

Kwa taarifa yako,hadi mwezi January Wizara zinazotekeleza miradi mikubwa zimepokea wastani wa 50% ya bajeti zao,kinyume na miaka ya nyuma ambapo utekelezaji wa bajeti ulikuwa haufiki hata 75%.Mfano wizara ya ujenzi hadi sasa ina 55% .

Sekta ya ujenzi niliko mimi hadi sasa utekelezaji wa bajeti tuko 60%,haijawahi tokea,waulize wakandarasi watakupa majibu zaidi.
Nashukuru unatoka kwenye sekta husika, tusaidie mambo mawili kupanua uelewa
1. Fedha miradi zimetengwa kwenye budget na zimeshatolewa Kwa kiwango hicho? Maana awali fedha za miradi hii zilikuwa hazisomwi kwenye budget sijui Kwa Sasa kama utaratibu umebadilika

2. Ni kwanini speed imepungua wakati fedha zimeshatengwa kw kiwango hicho? Kwanini Mawaziri wasiwalazimishe wakandarasi kuongeza speed? Mfano nakuja Dsm mara Kwa mara sioni barabara ya kimara kibaha ikikamilika wala kuona wakandarasi wakiwa site Kwa wingi ule zaidi ya mwaka Sasa. Tatizo ni Nini?

Hatuwezi tukafanya Jambo gharama zisiongezeke kwa mradi kutekelezwa nje ya muda?

Kuhusu COVID, naombeni mtusaidie uhusiano wa COVID na miradi hii Kwa Leo tunavyozungumza maana Nchi haipo kwenye lockdown
 
Hii ni kwenye makaratasi? Maana huku field hakuna tunachokiona. Au zinaishia kwa wala urefu wa kamba??
 
1.Kwanza sina uhakika kama fedha zilikuwa hazitengwi kwenye bajeti,hili sijawahi liona vinginevyo kungekuwa hakuna haja ya ku table bajeti za Wizara na Serikali.

2.Hili la speed kupungua sijui unalipima vipi,walioko site wanasema ujenzi unaendana na work programe isipokuwa kwa mradi wa Bwawa la umeme ndio tuliambiwa ulichelewa kidogo kwa sababu za mvua,covid nk.

Ni vyema kusikiliza kipindi cha Ben Mwanantala huwa wanatoa progress Kila wiki. Nadhani kilichobadilika na mapicha picha na mapambio nothing else.

Kuhusu hiyo barabara ya Kibaha tuliambiwa utekelezaji umefikia 90% na Kuna variations zimejitokeza zinahitaji ongezeko la gharama na kwamba wanaendelea na tathmnini,pia kumbuka Waziri aliagiza mkandarasi afumue sehemu aanze upya kwenye hiyo hiyo barabara.Sina maelezo zaidi ya hayo kwa kuwa sio project Manager, maelezo yangu haya ni kwa mujibu wa serikali.

Ili gharama zisiongezeke ni lazima kuwe na flow nzuri ya pesa kutoka Serikalini,uhusiano wa covid na miradi ni kwamba unakuta kuna materials zinatakiwa kuagizwa nje ya nchi kama mitambo nk huchelewa kufika kwa wakati, sababu ni restrictions zilizokuwepo zilivuruga regular supply chain na production.
 
Hii ni kwenye makaratasi? Maana huku field hakuna tunachokiona. Au zinaishia kwa wala urefu wa kamba??
Labda wewe huna macho,ukiwa kipofu huwezi kuona..

Miradi mikubwa sio sawa na madarasa lazima quality control ifanyike inavyostahili.👇

Screenshot_20220211-211916.png

Screenshot_20220210-223456.png

Screenshot_20220208-125829.png

Screenshot_20220204-212430.png

Screenshot_20220203-154307.png

Screenshot_20220129-231048.png

Screenshot_20220128-082942.png

Screenshot_20220122-163321.png

Screenshot_20220118-132103.png
 
Pesa tunazo nyingi Sana shida yenu mnashindia pono badala ya kutafuta habari za uhakika.

Kwa taarifa yako,hadi mwezi January Wizara zinazotekeleza miradi mikubwa zimepokea wastani wa 50% ya bajeti zao,kinyume na miaka ya nyuma ambapo utekelezaji wa bajeti ulikuwa haufiki hata 75%.Mfano wizara ya ujenzi hadi sasa ina 55% .

Sekta ya ujenzi niliko mimi hadi sasa utekelezaji wa bajeti tuko 60%,haijawahi tokea,waulize wakandarasi watakupa majibu zaidi.
Dohhh unasema wanashindia pono Hahaha
Hebu watake radhi

Ova
 
Mradi wa Mwalimu Nyerere wa umeme, Barabara za mwendokasi, Mradi wa umeme Rusumo na daraja la Busisi speed yake imepungua Sana. Lakini pia usimamizi wa Wizara na idara za serikali si wakuridhisha. Mradi unavyochukua muda mrefu ndivyo gharama uongezeka. Niwaombe JMT tukimbizane imalizike Kwa wakati .

Lakini pia nimpongeze Mhe. Rais Kwa kupata fedha za mwendokasi awamu ya sita. Natamani kuona barabara inayotoka mjini kwenda airpot to Chanika inapewa kipaombele Kwa Sasa Kwa Sasa itasaidia kisarawe kupanuka, itasaidia kufungua milango ya biashara ukanda huo na kukuza Pato la mwananchi na Taifa
Hebu punguza kulalamika
Duh,we ni malalamiko jazz band

Ova
 
Mradi wa Mwalimu Nyerere wa umeme, Barabara za mwendokasi, Mradi wa umeme Rusumo na daraja la Busisi speed yake imepungua Sana.
Bila shaka serikali imeupokea ushauri wangu na kuufanyia kazi. Mm nilishauri kuwa hii miradi ni mingi Sana hatuwezi kwenda nayo yote. Minginegine iachwe

Awamu ya 6 imekataa pesa na kodi za dhuluma.

tunajenga kwa pesa halali lbd ndio maana unaona speed imepunguwa

Dhuluma inamwisho mbaya

Serikali haina uthibiti mzuri wa fedha kwani wizi kwenye hii miradi mikubwa umekithiri!! Rais Samia muda si mrefu utaanza Kulia Kwani watamletea invoice za malipo yenye gharama kubwa sana kwa sababu ya ongezeko ya gharama za hiyo miradi [Cost overruns]!! Itakuwa bahati sana kama serikali haitastakiwa na hawa wanaojenga hiyo miradi mikubwa hasa bwawa la Mwalimu Nyerere!!
 
Pesa tunazo nyingi Sana shida yenu mnashindia pono badala ya kutafuta habari za uhakika.

Kwa taarifa yako,hadi mwezi January Wizara zinazotekeleza miradi mikubwa zimepokea wastani wa 50% ya bajeti zao,kinyume na miaka ya nyuma ambapo utekelezaji wa bajeti ulikuwa haufiki hata 75%.Mfano wizara ya ujenzi hadi sasa ina 55% .

Sekta ya ujenzi niliko mimi hadi sasa utekelezaji wa bajeti tuko 60%,haijawahi tokea,waulize wakandarasi watakupa majibu zaidi.
Yaani Wizara yako ya UJENZI imepewa Budget ya 55% lkn unasema hadi sasa mmetekeleza 60%

Naanza kupata wasiwasi nawewe unahusika kwenye upigaji au unaimba story za Makaratasi.
 
Serikali haina uthibiti mzuri wa fedha kwani wizi kwenye hii miradi mikubwa umekithiri!! Rais Samia muda si mrefu utaanza Kulia Kwani watamletea invoice za malipo yenye gharama kubwa sana kwa sababu ya ongezeko ya gharama za hiyo miradi [Cost overruns]!! Itakuwa bahati sana kama serikali haitastakiwa na hawa wanaojenga hiyo miradi mikubwa hasa bwawa la Mwalimu Nyerere!!
Hata hizo flyover za Chang'ombe na uhasibu ikiwa ni pamoja na mwendo kasi Mbagala naona ni ujinga ujinga tu! Ngoja liende kila siku miforeni hapo hawamalizi hata upande mmoja wa flyover haujaisha siku zote hizo wakati JPM kwacha ujenzi umeshaanza!
 
Ilikuwa na teni pasenti ya mzee, na kundi lake la Kalemani, Sasa hamna namna watalipana
 
Back
Top Bottom