Uanzishwaji wa miradi mikubwa ya kijeshi mnayodhaniwa na ‘great thinkers’ utaendelea kubaki kuwa ndoto za alinacha. Ukiweka pembeni changamoto za kiuchumi kama ukosefu wa uwekezaji mkubwa unaohitajika kwa teknolojia za kisasa, bado tunakumbwa na matatizo ya kisera na kimfumo,kwa kuwa ni wazi kabisa kuwa kwa sasa Tanzania inaendelea kushuhudia mifumo iliyoshindwa (systematic failure). Zaidi ya hapo, hatuna rasilimali ya kitaaluma (intellectual resource) ya kuweza kuendeleza au kubuni teknolojia kubwa na ya kisasa ya kijeshi. Ingawa kuna uelewa wa jumla miongoni mwa watu kuhusu masuala ya kijeshi, uhalisia wa uhandisi, uundaji wa silaha, uendelezaji wake, na mifumo ya usafirishaji ni mchakato mgumu sana kuliko inavyofikiriwa. Inahitaji kiwango kikubwa cha maarifa ya juu ya kisayansi na maelfu ya wafanyakazi waliobobea kwa viwango vya juu katika maeneo mbalimbali ili kuweza kutengeneza na kusimamia mifumo ya kisasa ya kijeshi. Je, JWTZ ina hiyo skilled labour force ya kiwango hicho? Kwa sasa, hatuna mtaji wa mabilioni ya dola wala nguvu kazi ya kitaalamu ya kijeshi inayoweza kuendeleza teknolojia hizo za hali ya juu tunazozitamani. Hili si suala la ndoto bali ni changamoto ya kiuhalisia inayohitaji kutazamwa kwa jicho la kisera, kisayansi na kimkakati.