Miradi ya JKT na JWT/Shirika la mizinga, ni miradi ya kusikitisha sana, ni kipimo cha level ya uwezo wetu sisi Watanzania

Hayo unayoyataka yanahitaji fedha swali je serikali yako inaweka fedha usione China wanazalisha bidhaa unaenda nunua kariakoo nyuma yake kuna uwekezaji wa matrillion sio kazi ndogo hata kidogo kama unavyodhani
Kwa hiyo kinyume chake ndiyo kuwekeza kwnye Miradi ya Kuliabisha Jeshi na Taifa..??/ Kufungua mafremu ili kuliabisha Jeshi na Nchi...?
 
Ila kweli yani Jeshi eti wana project ya kufyatua Tofali.
Nadhani tatizo lipo kwenye vigezo vya kurecruit wanatumia vigezo vya miaka ya 1920 huko.
Saivi zama zimebadilika jeshini wanatakiwa watu vichwa kweli kweli.
Vichwa hawatakiwi sasa
 
Tatizo linaanzia Elimu
Nyerere hakuwekeza kwenye Elimu yeye aliwaona wazungu maadui, akaenda alivyotaka yeye bila kukosolewa.
 
Mleta mada uko sahihi. Hapa Dodoma kwa mfano, JWTZ wamechukua ajira za watu wengi sana na kuharibu mitaji yao.
*Viwanda vya kufyatua tofali.
* Fremu za hardware.
*Saloon za kiume.
*Kuuza kokoto na mchanga.
....na mambo mengine ya hovyo wanafanya wao.

Huko mambele gunduzi nyingi zinafanywa na majeshi lkn hawa wetu wako bize kuchuuza .
🤣
 
Tatizo linaanzia Elimu
Nyerere hakuwekeza kwenye Elimu yeye aliwaona wazungu maadui, akaenda alivyotaka yeye bila kukosolewa.
Jeshini wanaenda kupumzika ,miaka ya nyuma ilikuwa mtu akimaliza form six anakimbilia huko ,eti kuna maslahi.. Kiufupi jeshi wanaensa kukua na kuna vipaji vimelala ...Rafiki zangu wawili wamekimbilia huko baada ya form six tu.
 
Tafiti nyingi kwa nchi zilizoendelea huwa zinaanzia jeshini.sasa huku kwetu Tanzania mkuu wa majeshi mwenyewe sina uhakika kama ana hata diploma.
🤣😁😄😂😄🤣😁😄😄😂😁😁😁
 
Hivi wakati wa Magufuri hawakuwa na project yoyote?
JWTZ na ndugu yake JKT, waliapaswa kuwa ndio centre ya kuibua viwanda vya kizalendo Tanzania hii, Walipaswa kuwa ndio sehemu ya watu kwenda kujifunza uchumi wa kizalendo, Watu kwenda kujifunza kuto penda bidhaa za nje na wathamini bidhaa za ndani ya nchi kamam sehemu ya Uzalendo.

Centre ya uchumi wa kizalendo, made in Tanzania ilipaswa kuonekana pale.

Cha kusikitieha JKT unakuta wana miradi eti Gari lori za kusombea watu mchanga,

- Wana Maduka ya Hardware, wanafyatua tofali za kuuza, wana zoa taka mitaani, wana kampuni ya kufanya usafi mtaani, wana kampuni sijui za fumugations, wanakata bima za vyombyo vya moto.

To be honest hizi ni project za kureflect uwezo wetu kwenye kufikiria sio project za kizalendo hata kidogo haziwalishi uzalendo wa nchi hata kidogo.

JKT walipaswa kuwa na viwanda vyao vya kuunda zana rahisi hata za kilimo, Afya na kadhlika, walipaswa kuwa na maabara za kutafiti madawa hata ya miti shamba kama India na kuyazalisha na kuuza na hata ku export nje.

Sasa JKT kuwa na maduka ya Hardware ni mambo ya ajabu mno wanashindana na raia mtaani?

JWTZ Sasa
Hawa wana frame, wana kumbi za harusi, mara wana mradi wa kupasua kokoto, hizi ni project za aibu kufanywa na Jeshi la Ulinzi na usalama.

Sijui kama Duniani kuna nchi nyingine jeshi lake wana aina hizi za project, Frame ni vitu vya hovyo sana na vya kuonyesha kiwango chetu cha kuwaza kwamba tusivyo creativity tunao tegemea kuwa dampo..

JWTZ kwa uwezo wao walipaswa kuwa na kituo cha kutafiti na kuja na solution ya baadhi ya matatizo ya kijamii na kijeshi Kiwanda cha nyumbu kile kilipaswa kuwa kina export magari ya kijeshi na ya kiraia, kilipaswa ndicho kinazalisha mabus ya Magereza, Police, JKT na hata magari ya Serikali baadhi.

Ni aibu JWTZ na wao kushindana kuendesha Youtong wakati wana uwezo wa kuwekeza kwenye kiwanda cha nyumbu na wakazalisha mabasi yao mazuri kabisa.

Frame ni projects za aibu kwa JWT Na sijui kama kuna watu wa kuwashauri kuwaambia hizi ni project za aibu waachane nazo waachie watu wa kawaida mtaani.

Kuna siku watakuja na biashara za kukaanga Chipa hivi hivi tukiangalia.

JWTZ na JKT wanapaswa kuwa ndio kipimo cha projects za kizalendo Projects za made in Tanzania, projects za kuonyesha kwamba tunaweza.
Kwamba.. Soon wataanzisha vibanda vya chips..!!!?
 
Hayo unayoyataka yanahitaji fedha swali je serikali yako inaweka fedha usione China wanazalisha bidhaa unaenda nunua kariakoo nyuma yake kuna uwekezaji wa matrillion sio kazi ndogo hata kidogo kama unavyodhani
Sio kweli..... yani ata kuzalisha nguo zao wenyewe inahitaji matrillion ya pesa...!?
 
JWTZ na ndugu yake JKT, waliapaswa kuwa ndio centre ya kuibua viwanda vya kizalendo Tanzania hii, Walipaswa kuwa ndio sehemu ya watu kwenda kujifunza uchumi wa kizalendo, Watu kwenda kujifunza kuto penda bidhaa za nje na wathamini bidhaa za ndani ya nchi kamam sehemu ya Uzalendo.

Centre ya uchumi wa kizalendo, made in Tanzania ilipaswa kuonekana pale.

Cha kusikitieha JKT unakuta wana miradi eti Gari lori za kusombea watu mchanga,

- Wana Maduka ya Hardware, wanafyatua tofali za kuuza, wana zoa taka mitaani, wana kampuni ya kufanya usafi mtaani, wana kampuni sijui za fumugations, wanakata bima za vyombyo vya moto.

To be honest hizi ni project za kureflect uwezo wetu kwenye kufikiria sio project za kizalendo hata kidogo haziwalishi uzalendo wa nchi hata kidogo.

JKT walipaswa kuwa na viwanda vyao vya kuunda zana rahisi hata za kilimo, Afya na kadhlika, walipaswa kuwa na maabara za kutafiti madawa hata ya miti shamba kama India na kuyazalisha na kuuza na hata ku export nje.

Sasa JKT kuwa na maduka ya Hardware ni mambo ya ajabu mno wanashindana na raia mtaani?

JWTZ Sasa
Hawa wana frame, wana kumbi za harusi, mara wana mradi wa kupasua kokoto, hizi ni project za aibu kufanywa na Jeshi la Ulinzi na usalama.

Sijui kama Duniani kuna nchi nyingine jeshi lake wana aina hizi za project, Frame ni vitu vya hovyo sana na vya kuonyesha kiwango chetu cha kuwaza kwamba tusivyo creativity tunao tegemea kuwa dampo..

JWTZ kwa uwezo wao walipaswa kuwa na kituo cha kutafiti na kuja na solution ya baadhi ya matatizo ya kijamii na kijeshi Kiwanda cha nyumbu kile kilipaswa kuwa kina export magari ya kijeshi na ya kiraia, kilipaswa ndicho kinazalisha mabus ya Magereza, Police, JKT na hata magari ya Serikali baadhi.

Ni aibu JWTZ na wao kushindana kuendesha Youtong wakati wana uwezo wa kuwekeza kwenye kiwanda cha nyumbu na wakazalisha mabasi yao mazuri kabisa.

Frame ni projects za aibu kwa JWT Na sijui kama kuna watu wa kuwashauri kuwaambia hizi ni project za aibu waachane nazo waachie watu wa kawaida mtaani.

Kuna siku watakuja na biashara za kukaanga Chipa hivi hivi tukiangalia.

JWTZ na JKT wanapaswa kuwa ndio kipimo cha projects za kizalendo Projects za made in Tanzania, projects za kuonyesha kwamba tunaweza.
Uko sahihi. Angalau kipindi cha mwalimu Nyerere walikuwa wana miradi ya kisomi. Kulikuwa na kiwanda cha magari yakiitwa Nyumbu. Tungekuwa tuna akili sasa hivi ungekuta tunatengeneza magari yetu ya kijeshi wenyewe.
 
Jeshi linashindwa kuwa na miradi ya kimikakati kwa taifa!! Ni aibu sana tena sana JWTZ kufanya biashara za uchuuzi na kushindana na wajasiriamali wadogo.

Miradi ya kimkakati kama ya gesi asilia na nishati ni miradi ambayo ingepaswa kufanywa na kusimamiwa na jeshi na nchi ingepiga hatua kubwa.

Miradi kama utengenezaji wa madawa na vifaa tiba ni miradi ya kimkakati ambayo ingefanywa kwq weledi ingepunguza gharama za kuagiza dawa na vifaa tiba nje ya nchi.

Jeshi lingetumia wataalamu wake kufanya tafiti mbalimbali ambazo zingechochea na kuharakisha maendeleo kwa Kasi.

JWTZ inafanya kazi nzuri ya kulinda mipaka ya nchi ila lazima libadilike kuendana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
 
Back
Top Bottom