View attachment 3696706
Katika vilima virefu na vya kijani vya Kaunti ya Kisii magharibi mwa Kenya, barabara mpya zinabadilisha maisha na kuchochea biashara ya eneo hilo.
Malori yaliyojaa ndizi, maparachichi, miwa, na mawe ya kuchongwa sasa huondoka alfajiri, na kuwaingizia mapato ya haraka kulima wa eneo hilo.
Kabla ya kampuni za China kuboresha mtandao huo, miundombinu duni ilichangia viwango vya juu vya umaskini.
Leo hii, wafanyabiashara kama Jane Gesare, mwenye umri wa miaka 43, ambaye kwa muongo mmoja amekuwa akinunua na kuuza mazao mapya magharibi mwa Kenya, wanaweza kusafirisha bidhaa kwa haraka na uhakika.
Mama huyo mwenye watoto wanne husafiri katika vilima vya Kisii kununua ndizi moja kwa moja kutoka kwa wakulima kabla ya kuzisafirisha na kuzipeleka miji ya Kisumu na Nairobi.
Awali, kupita katika barabara hiyo ya kilomita 80 iliyojaa matope na mashimo ilichukua muda wa saa sita uliojaa machungu.
Lakini sasa, baada ya barabara hiyo kuwekwa lami na kampuni ya ujenzi ya China, safari hiyo hiyo inachukua dakika 80 pekee.
"Kabla barabara hii haijawekwa lami na Wachina, nusu ya ndizi zangu ziliiva na kuoza njiani. Lori lilikuwa likikwama. Hali hiyo haipo tena sasa," Gesare aliiambia Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.
Awali suala la kuchelewa kwa usafiri lilipelekea kukataliwa mara kwa mara kwa mavuno ya chai ya Samson Onserio.
Shirika la Maendeleo ya Chai nchini Kenya (KTDA) linahitaji majani mabichi ya chai yawasilishwe ndani ya saa sita baada ya kuchumwa, muda ambao ulikuwa mgumu kufikiwa kwenye barabara zisizo na lami.
"Malori yalikuwa yakichelewa kila mara, na tulipoteza bonasi zetu," alisema Onserio.
Lakini kutokana na barabara mpya ya lami, mavuno yake sasa yanafika kiwandani ndani ya muda usiozidi saa moja, jambo linaloongeza kipato chake cha kila mwaka.
Katika kaunti zenye watu wengi za Kisii na Nyamira magharibi mwa Kenya, mamia ya kilomita za barabara za lami sasa zinapita katikati ya mashamba ya migomba, migodi ya mawe ya kuchongwa, na mashamba ya chai, zikifungua fursa mpya za kiuchumi kwa jamii za eneo hilo.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Mamlaka ya Barabara Kuu ya Taifa ya Kenya (KeNHA) na Mamlaka ya Barabara za Vijijini ya Kenya (KeRRA), kampuni za China zimejenga au kuboresha zaidi ya kilomita 250 za barabara katika kaunti hizo mbili katika kipindi cha miaka sita iliyopita.
Muhimu zaidi kati ya hizi ni barabara kuu ya Isebania-Kisii-Ahero yenye urefu wa kilomita 206 na barabara zinazoiunganisha, ambayo imekuwa uti wa mgongo wa uchumi wa eneo la Nyanza Kusini. Njia hii, inayoanzia Isebania kwenye mpaka wa Tanzania na kupita Migori, Homa Bay, na Kisii kabla ya kuishia Ahero katika Kaunti ya Kisumu, ni kiungo muhimu cha kimataifa kinachounganisha Tanzania na Sudan Kusini kupitia Kenya.
Barabara hii ilikarabatiwa kwa ufadhili wa pamoja kutoka serikali ya Kenya na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Kasi ya utekelezaji iliongezeka mwaka 2024 wakati Kenya ilipopata ufadhili kutoka China ili kufufua miradi 15 ya barabara iliyokuwa imekwama.
Matokeo yake tayari yanaonekana wazi: mkulima wa maparachichi wa eneo hilo, John Manyura, alibainisha kuwa barabara mpya ya Nyabigena-Nyakorere-Gesonso inawawezesha wanunuzi kufika mashambani moja kwa moja.
Huko Tabaka, eneo maarufu kwa shughuli za uchongaji wa mawe laini (soapstone), mafundi wanasifu barabara ya Nyachenge-Tabaka-Ogembo, iliyojengwa na kampuni ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Henan, China (CHICO) kwa kubadilisha jinsi wanavyosafirisha na kuuza bidhaa zao zilizochongwa.
"Zamani, wanunuzi kutoka Nairobi hawakuweza kufika kwa sababu barabara ilikuwa mbaya sana. Sasa watalii na wasafirishaji bidhaa nje ya nchi wanakuja na magari yao moja kwa moja hadi eneo la machimbo," alisema Eric Nyabuto, mwenye umri wa miaka 55, ambaye ni mchongaji.
Barabara mpya zilizowekwa lami zimetoa msukumo mkubwa kwa waendeshaji wa usafiri wa umma na bodaboda, huku zikichangia kuongeza wanafunzi kujiunga na shule za eneo hilo kwa asilimia 30.
Mbali na usafiri, miundombinu hiyo imechochea upanuzi wa biashara ya majengo ya kibiashara, na kupelekea kuongezeka kwa maduka, nyumba za kupanga, na makusanyo makubwa ya ushuru wa manispaa.
Katika kaunti za Kisii na Nyamira, wakazi wanasifu mara kwa mara barabara hizo zilizojengwa na Wachina kwa ubora wake wa juu.
"Kampuni za China zilikuja hapa na mashine nzito ambazo hatukuwahi kuziona. Ziliweka mifumo mizuri ya mifereji ya maji, njia za ziada kwa ajili ya magari kupanda milima, na madaraja ya watembea kwa miguu. Hata wakati wa mvua kubwa, barabara haisombwi na maji kama zile za zamani," alisema Joseph Miruka, kiongozi wa jamii.
Kaunti za Kisii na Nyamira ni muhimu kwa uzalishaji wa ndizi na chai nchini Kenya, na zinawakilisha eneo linalokua kwa kasi zaidi nchini katika uzalishaji wa maparachichi.
Kwa mujibu wa maafisa waandamizi wa kilimo wa Kaunti ya Kisii, kuweka lami kwenye barabara muhimu zinazounganisha maeneo hayo kumeleta mafanikio makubwa, huku hasara ya ndizi baada ya mavuno ikipungua kutoka asilimia 40 mwaka 2018 hadi asilimia 12 mwaka 2025.