Miradi ya uwekezaji nchini imeongezeka kwa 16.5 ndani ya Mwaka chini ya Uongozi wa Rais Samia

Miradi ya uwekezaji nchini imeongezeka kwa 16.5 ndani ya Mwaka chini ya Uongozi wa Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imeendelea na juhudi mbalimbali za kuhamasisha na kuvutia uwekezaji nchini.

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, bungeni hii leo Mei 04 2023 Waziri wa Wizara hiyo, Dkt Ashatu Kijaji ameeleza kuwa katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 Wizara imesajili jumla ya miradi mipya 240 (Wazawa - 89, Wageni - 94 na Ubia - 57) inayotarajiwa kuwekeza jumla ya dola za Marekani milioni 4,387.17 na kutengeneza ajira 39,245, sawa na ongezeko la miradi 34 (16.5%) ikilinganishwa na miradi 206 (Wazawa - 63, Wageni - 79 na Ubia - 64) iliyosajiliwa katika kipindi kama hicho kwa mwaka 2021/22.

Akitoa uchanganuzi wa miradi hiyo ameeleza kuwa kati ya miradi 240 iliyosajiliwa, katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023, miradi 187 sawa na asilimia 77.9 imeanza utekelezaji kwenye sekta za Kilimo (18), Majengo ya Biashara (10), Miundombinu (2), Rasilimali watu (5), Viwanda (101), Huduma (5), Mawasiliano (1), Utalii (9) na Usafirishaji (36).

Matokeo haya ni matunda ya juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu pamoja na kushiriki katika makongamano ndani na nje ya nchi na ziara zinazofanywa na Viongozi Wakuu nje ya nchi.

Unaweza kusoma bajeti nzima chini hapo
 

Attachments

Back
Top Bottom