Wamarekani wanamlaumu Kobe Kobe ana makosa ya kutowapa wazazi wake maisha hakuandika wosia kabla hajafa hivyo ni kama alichagua kutojumuisha wazazi wake katika wosia wake hivyo mali zote zimeenda kwa mke wake.
Ukweli wamarekani wana utamaduni wa ajabu sana, how can a person be worth Trillions of Money and his parents are broke? This life is not fair.
Kobe Bryants parents are broke. His dad was forced to auction off the ring Kobe gave him in the year 2000 ili apate hela ya ku survive huku mkewe na Kobe kapewa mirathi ya dola milioni 600 ambazo kobe kaacha bank.
Nyie ndio hamuelewi maisha.
Mzazi ana wajibu wa kulea mtoto, mtoto hana wajibu wa kulea mzazi. Ikitokea mtoto kalea mzazi, vizuri. Ikitokea mtoto kajikita zaidi kulea watoto wake wazazi kawaacha, hiyo pia ni haki yake. Mzazi hatakiwi kumuacha mtoto, hususan akiwa mdogo, lakini mtoto ana uhuru wa kuwa karibu na mzazi au kujiengua aende na maisha yake.
Na urithi ni jambo la hiyari. Kobe Bryant angeweza kumpa mke wake pasu la mali na kugawa mali zake kwa watoto masikini.
Hakulazimika hata kuwaachia watoto wake urithi. Angeweza kusema nyie watoto siwaamini, nikiwapa mali mtazitapanya, nazigawa kwa watoto yatima ambao watazitumia vizuri, ni haki yake. Mali yake, yeye bdiye anaamua itumike vipi. Ukitaka kumpa baba yake Kobe mali, tafuta zako.
Licha ya hayo, urithi ni kwa watoto. Wazazi wanarithisha watoto.
Baba yake Kobe Bryant, Joseph Bryany, alikuwa mchezaji wa basketball wa NBA (Philadelphia, San Diego, Houston) na kimataifa. Yeye ndiye kamrithisha Kobe kucheza basketball. Baba Kobe kacheza mpaka Italy na France, Kobe kakulia Italy mpaka Kitaliano alikuwa anaongea. Sasa baba yake Kobe kashindwaje kujipanga miaka yote hiyo aliyocheza basketball NBA, Italy na France?
Mnajuaje uhusiano wa Kobe na baba yake ulikuwaje? Mnajuaje kama walikuwa na beef?
Kwa nini mnataka kuwafanya watoto kuwa ni mafao ya uzeeni?
Hizi tabia za watoto kutumiwa na wazazi kama mafao ya uzeeni ni ushamba, umasikini na ujinga. Tunaona watoto wengine wanakufa kabla ya wazazi wao, sasa ukitegemea mtoto atakufaa uzeeni, halafu akafariki kabla yako, hapo utafanyaje uzeeni?
Proved