Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Kulikuwa na shida gani wazazi kuonesha picha kwa waandishi? Au zilionesha "uhalisia" wa familia enzi hizo? Ha ha ha! Ila kama ndio ukweli why akasirike?
Una mentality ya kikoloni na usipotazama wanao watakutenga kwa dhana yako hii ya mtoto hakui. Mtu mzima yeyote anatakiwa ahojiwe kuhusu personal life mwenyewe, sio mzazi wake. Kama ni mzazi basi huyo mtu awe amefariki au akiwa hai atoe ruhusa. Sio kisa mzazi wake ndio ulipwe hela na media za udaku uanze kusema mwanangu alibakwa akiwa mtoto.

Chid Benz alilalamika watangazaji wa Clouds Media walipomlipa na kumhoji mama yake na akasema mambo bila kuchuja. Wao wenyewe watangazaji huwezi waambiwa wazazi wao wahojiwe na watangazaji wengine wakakubali.
 
Marehemu babu yangu alikua hivi pia, yeye kusomesha wajukuu ilikua sio big deal kwake, wewe ukifanikiwa ni maisha yako na wanao, hutokaa usikie analalama ati humpi pesa, humkumbuki etc.

Yeye alikua na bustani zake, mifugo na mashamba yaliyomkeep busy uzeeni mwake.
Nadhani wazee wengi kutaka kuletewa kila kitu na watoto ndo hujenga hiyo dhana ya sijui laana na hizo blah blah za kutaka huduma kwa lazima ilhali na mtoto ana majukumu yake mengine.
 
Nimejaribu kufuatilia inaonyesha wazazi wa Kobe ndiyo tatizo.

1. Kukataa kijana wao amwoe Vanessa. Sababu ikiwa ni umri mdogo Kobe wakati anataka kumwoa Vanessa. Kobe alikuwa 21 na Vanessa 17 wakati wanavalishana pete ya uchumba. Pia sababu nyingine Vanessa si African American. Wazazi walipendelea aoe African American.

2. Si wazazi tu hata dada wa Kobe walikuwa hawampendi Vanessa. Kumbuka Kobe alikuwa anawahudumia kwa kila kitu dada zake.

3. Kwenye interview Kobe aliwahi kusema aliwahi kutaka kuwanunulia nyumba nzuri wazazi wake lakini wakasema not enough.

4. Wazazi wa Kobe walishawahi kuuza baadhi ya medali muhimu za Kobe bila ridhaa ya Kobe. Hii si sawa.

5. Wazazi na dada wa Kobe hawakuhudhuria harusi ya Kobe.

Ukifuatilia kwa ukaribu wazazi au familia ya Kobe ilikuwa inamsumbua na kutompa uhuru wake kufanya maamuzi kama anavyotaka. Hii si sawa.

Pia nimeona hata mama wa Vanessa ni shida sana.

Amefungua shauri la madai akitaka alipwe $96 kwa kila saa masaa 12 kwa siku kwa miaka 18 akidai alikuwa anawasaidia Kobe na Vanessa kulea watoto wao. Yani bibi anataka alipwe kuwaangalia watoto hapa na pale kwasababu Vanessa amesema si kweli mama yake alikuwa anawasaidia kulea watoto kama kazi bali ni yeye ni bibi na alikuwa anaangalia watoto kama wanavyofanya wakina bibi wengine tu.

Pia kumbuka huyu mama wa Venessa alikuwa anapatika kila kitu na nyumba/apartment ya bure analipiwa.

Hapo unaweza ona Kobe alikuwa mtu poa na si kweli alikuwa hawajali wazazi.
 
Hii ni tabia ya kitajiri sana. Na mara nyingi watu wenye tabia hii huwa wanajipanga kusimama wenyewe na kuridhika na maisha yao hata kama si ya kifahari.

Halafu hao mara nyingi huwa na utajiri wa watu. Yani mshua anaweza kuwa hana hela ila ile network yake ya watu inavyoweza kufanya mambo tu ni zaidi ya hela.
 

Umeweka vizuri historia kwa facts.

Tatizo watu wengi wanataka kumhukumu Kobe kwamba alikuwa na roho mbaya bila hata kujua facts za historia yake kwanza.
 
Kabisa mkuu, msiba wake tulisherekea maana watu walikua wengi mno, ile connection aliyokua nayo hakuna mwanafamilia alieirithi kwakweli.
Na kweli hakua tajiri kiivyo ila ile kutolia shida kulimjengea heshima mtaani aonekane tajiri sana.
 
Mkuu usichanganye mambo.
Kuheshimu mzazi na kumrithisha mzazi ni vitu viwili tofauti.
Tunapaswa kuheshimu wazazi ila sio kurithisha wazazi.
Tunarithisha watoto, wazazi tunawapa only upendo
Sijazungumzia kumrithisha mzazi mali. Ila kama ana uhitaji, na mali moto anazo nyingi kwa nini ushindwe kumpa sehemu yake?

Kama mzazi angeamua kubania mali zake akaacha kumpatia mtoto malezi na elimu bora hizo mali angezipata vipi?!
 
Ni sahihi kwa namna moja ama nyingine, lakini mkuu kiranga hawa macelebrity mimi sitaki kusikia excuse zao wamemake hela nyingi kuwatunza wazee wao sio issue ni hawataki kwa sababu zao tu, lapili hawa wamerekani ndo watu wakusekwa wazee wao kwenye retirement homes, socially kuna vitu vingi sana wanapuyanga
 
Sehemu nyingi duniani zina sheria za ‘child support’.

Kuna sehemu yoyote duniani yenye sheria za ‘parental support’?

Kama hakuna, ni kwa nini?
 
Hapa inategemeana uwezo wa Baba wakati huo dhidi ya kipato cha Mtoto huyo.
Africa uchumi wake umepita au inapitia siasa nyingi ambazo hazi akisi ukweli hivyo inaweza kuwaachia wazazi wetu katika Hali Mbaya au kumbana Mtoto kuchomoza.
Mfano wazee wetu enzi hizo kazi zilikuwa zinapatikana, hivyo Imani Mtoto atakuwa Naye atapata kazi, Naye atafanya yake, THB ipo atajipanga atajenga, kabla ya ku staafu, Kiwanja anaomba atapata, matibabu bure au kama ni NHIf ipo for life, lakini unaonaje sasa hivi Hali sio Hali., hivyo hatuwezi kusema hapa Mzazi alishindwa, kujiwekea akiba ya uzeeni .
 
Kitu cha muhimu kabisa ni kwamba mzazi ana wajibu wa kumlea mtoto mpaka afikishe umri fulani. Zaidi ya hapo ni option kuendelea kum support.

Na mtoto akifikisha umri fulani, anaanza kujipanga kuwa na watoto wake na kuwalea.

Mtoto akianza kazi tu, anatakiwa kuanza ku focus ku save kwa ajili ya nyumba yake, kwa ajiki ya mafao yake ya uzeeni, kwa ajili ya kusomesha watoto wake, hapo uje umuongezee na kuhudumia wazazi wake tena? Kwani wazazi hawakujipanga siku zote hizo?

Labda mimi niko biased kwa sababu wazazi wangu hawahitaji msaada.

Lakini naona, jii mipango ya mtoto kutegemewa kumhudumia mzazi kwa kiasi kikubwa ni mzazi kukosa kujipanga, na kwa kiasi k8ngine kikubwa ni matatizo ya uchumi wetu kiujumla kamanulivyosema sitaki kuwa mtu nisiyetambua hilo, ila kama tuna matatizo ya uchumi, tuyatatue, tukiwawekea mzigo huo watoto, italeta mzigo mkubwa sana kwa mtoto kuhudumia watoto wake na wazazi.

Imagine baba umeshindwa kujiwekea akiba ya uzeeni mpaka unamtegemea mtoto, haponunatengeneza vicious cycle of poverty, huyo mtoto wako ukiwa unamtegemea yeye, na watoto wake wanamtegemea yeye, inakuwa kama jeshi moja linalopigana vita ya pande mbiki, atachoka mapema sana na atashindwa kufanya mambo yake mengi ya maendeleo. Kizazi hata kizazi tutabaki kwenye umasikini tu.
Tutakuwa tunafanya kazi kuhudumia watoto na wazazi tu, hakuna uwekezaji wala maendeleo.

Kama tulikuwa na mipango hiyo huko nyuma, tujipange tuondoke huko.

Halafu, tu normalize watoto kufocus kutunza watoto wao, sio wazazi. Tuondokane na mfumo wa kijima wa kufanya watoto kuwa ndiyo akiba ya uzeeni, hao watoto wakifa kabla ya wazazi, wazazi watafanya nini? Watoto wasipojali wazazi, wazazi watafanya nini?

Kama kuna umuhimu wa kutunza na kurithi, basi iwe mzazi ndiye anamtunza na kumrithisha mtoto, si mtoto kumtunza na kumrithisha mzazi.

Kama tuna matatizo ya kiuchumi, tuyatatue hayo matatizo ya kiuchumi, tusiwabebeshe watoto kazi za kutunza wazee kwa sababu tumeshindwa kutatua matatizo yetu ya uchumi na tunawafanya hao watoto kuwa ndiyo mafao yetu ya uzeeni.

Wao nao wanatakiwa kutunza watoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…