Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Mirathi ya Kobe Bryant yazua gumzo USA, utajiri wote wagawanywa kwa mke na watoto huku wazazi wakiishi kimaskini

Katika uislamu kuwatunza wazazi ni lazima na sio ombi kutokufanya hivyo ni dhambi kubwa itakayokufanya uingie jahanam.......

Mwenyezi haikubali ibada ya mtu asiyewatendea wema wazazi wake............
kwani hapa habari inahusu kuwatunza wazazi au kukosa fungu la mirathi
mjitahidi kujikita kwenye mada
 
Kuna wazazi hawafai uwape hata 10 jueni tu hivyo
 
Sasa unalaumu nn hapo?
Wazazi walikuwa na maisha yao wakamzaa kobe.
Kobe akawa na maisha yake akatengeneza familia yake, maana yake kobe akawa kizazi kingine mbele.
Sasa mzazi anahusikaje hapo zaidi ya hisani tu?
Yaani nisiipende familia yangu kwa sababu ya mzazi wangu?
Mzazi anatakiwa kuwa mpenzi mtazamaji..
Anajukumu la kupenda mkwe wake na wajukuu pia, akitimiza hilo atapendwa na familia yote na hizo offer atapata tu, kama si kwangu basi kwa mke wangu au wajukuu zake.
You nailed it. Kama wazazi waliishi vyema na mkwe wao hawawezi kosa dola, yaani hata wajukuu wasikuangalie, basi kuna mahali unakosea
 
Sio principle, ni wajibu wa watoto kuwatunza Wazazi wao. Hivi mkuu, Mzee wako akiumwa, wewe hutamuuguza!?
Wajibu kwa sheria gani? Kwa kanuni gani?

Hapa tunaongelea kumtunza mtu kwa pesa, urithi, si mtu kuumwa.

Na hata kuumwa kuna professionals wamesomea hiyo kazi ya kutunza wagonjwa, mimi sina utaalamu huo, naweza kujiweka kimbelembele kumtunza mtu anayeumwa, nikamuwahisha kufariki.

Mimi kazi yangu itakuwa kumtembelea na kusimamia mambo ya msingi tu.

Acheni ujima.

There is such a thing as division of labor, do you know that?
 
Family is Family. Na wazazi ndio mwanzo wa cheni ya familia. Yaani watoto wanauana kwa ajili ya Mali za wazazi wao, lakini wazazi waishi au wafe homeless au bila huduma muhimu za maisha wakati watoto wao wana mabilioni! Sioni logic hata kidogo.

Mwenyezimungu kakujaalia mapesa, unaanzisha NGo na unachangia mapesa kibao kuwasaidia watu baki wenye mahitaji mbalimbali, ilhali wazazi wako wanaishi maisha ya kifukara, hii ni ajabu sana.

Bora mtu ufe fukara.
 
Back
Top Bottom