Nchi maskini zitadumu kuwa maskini, sababu kuu ni mawazo ya kimasikini ya viongozi wake. Mawazo ya kimasikini yanaongozwa na kutaka kuabudiwa, kupewa sifa kupitiliza. Misafara ya viongozi wakuu wa Tanzania inakuwa na magari zaidi ya 30. Shughuli alipo kiongozi wa nchi eg rais, mkuu wa mkoa au wilaya viongozi wote wa kamati ya ulinzi na usalama huandamana nao. Wote wanahitaji posho toka kwa mlipa kodi maskini. Muda wa masaa zaidi ya 4 barabara hufungwa kupisha misafara ya wakubwa. Wanajua, na wanafurahia mateso kwa wananchi.