Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Msamaha ni jambo jema sana kama binadamu na pia ni sehemu ya ibada. Kitabu kitakatifu cha biblia tunasoma maandiko yakisema samehe saba mara sabini ikiwa na maana kwamba msamaha hauna kikomo.
Vile vile kitabu hicho kinasema kwamba tuheshimu mamlaka iliyowekwa na Mungu na ya Kaisari tumpe kaisari na Mungu tumpe Mungu.
Awamu ya tano na sita tumeshuhudia misamaha ya kisiasa kwa baadhi ya watuhumiwa na hata wafungwa maarufu.
Nikianza na awamu ya tano tulishuhudia mfungwa maarufu Babu Seya na wanawe wakiachiwa huru.
Baada ya kuapishwa kuwa Rais, Samia alianza kwa kuwasamehe masheikh wa uamsho na kuwatoa mahabusu walikokuwako kwa kipindi kirefu, hiyo ilifuatiwa kwa kufutwa kesi nyingi sana zilizokuwa zikiendelea mahakamani, zikiwemo za Tundu Lissu Makamu Mwenyekiti wa Chadema.
Hivi majuzi baada ya kikao na viongozi wa Dini na maombi ya kumsamehe Mbowe, tuliona DPP akiingiza nia yake ya kutoendelea na kesi jambo lililomfanya mbowe kuwa huru.
Mambo yote hayo yaliyofanyika kama nilivyoainisha hapo awali katika bandiko langu hili utaona uhusiano wa moja kwa moja wa mamlaka ya Urais na vitendo hivyo.
Ikimaanisha kwamba maamuzi hayo yamekuwa influenced moja kwa moja na kiti.
Ili kesi iende mahakamani na mpaka maauzi ya mahakama yatolewe taasisi mbali mbali za nchi zinakuwa zimehusika, hapo tunakuwa na takukuru,polisi,idara ya usalama, DPP na mahakama.
Taasisi hizi kulingana na mfumo wa nchi yetu ni huru, zinapaswa kuwa huru katika kutekeleza majukumu yake ya kusimamia utiifu wa sheria kwa raia wote hapa nchini.
Michango ya wanasiasa katika taasisi hizo ni kama haipo kwani inapokuja swala la kusimamia sheria siasa inakua haina nafasi tena.
Kwa sasa tumekua tukishuhudia maombi na nguvu za kisiasa katika kumaliza maswala ya kisheria hiyo ni hatari kwani tunajenga Taifa la watu wanaotegemea huruma ya wanasiasa badala ya kufuata sheria.
Ukiachana na maamuzi ya kisiasa kuingilia mchakato wa kisheria jambo hili limeendelea hata kwenye taasisi za kiulinzi na usalama ambapo jana ulipita msamaha mwingine kwa JKT waliogoma na kufukuzwa.
Sasa utaona ni namna gani misamaha inazidi kujichimbia zaidi katika Taifa letu badala ya kufuata sheria na kuheshimu mamlaka.
Kwa kufanya hivi tunakua tunakatisha tamaa watendaji wa taasisi zinaohusika na kusimamia utii wa sheria na usimamizi wa haki na pia tuna salimisha uhuru wetu kwa wanasiasa kwamba katika nchi hii maamuzi yote yatafanywa na wanasiasa tu.
Ushauri wangu ni kuhakikisha tunazipa uhuru zaidi taasisi zetu kuliko kuwekeza na kuongeza nguvu kwa wanasiasa.
Naliona Taifa letu likiangukia katika vurugu kubwa ya kutokuheshimu mamlaka wala kutii sheria kwani mwisho wa siku mwanasiasa ataingilia na hatimaye mhusika kuwa huru kwa matendo yake ambayo alipaswa kuwajibika nayo kisiasa.