Kumuachia haimaanishi uwe Mzembe , watu wasiosoma vizuri maandiko ndio wanatafsiri na kutumia vibaya huo msemo .Lakini hata mafundisho yameelekeza mtu apambane ili kufanikiwa .
Kumuachia Mungu katika utafutaji ni kunahusisha kufanya jitihada na nyenzo muhimu ili kupata kitu hiko na kutovuka mipaka mfano kutumia njia haramu kama uuaji ,dhuluma ,ufuska nk pamoja na kutokata tamaa na kuwa na dhana nzuri juu yako na Mwenyezi Mungu wakati wa shida au mambo yakienda tofauti na matarajio na kuendelea kupambana katika njia nzuri na Bora.