Kuna baadhi ya misemo inapumbaza na kulemaza. Maneno yanaumba!
Mwanzo mgumu! Ukiendelea kuamini na kukiri mwanzo mgumu hakika magumu hayataisha kwako.
Ngombe wa masikini hazai, akizaa huzaa dume. Hapa masikini akiamini maana yake ngombe, mifugo au mali zake haziongezeki.
Mkono mtupu haulambwi. Msemo huu unachochea mazingira ya rushwa. Sehemu ya huduma ukisikia msemo huo lazima taa nyekundu iwake kichwani.
Penye udhia penyeza rupia! Rushwa inachochewa hapo.
Mungu wa Yakobo, Isaka na Israel atanipigania! Hapa kuna upotofu. Sema MUNGU wangu au Mungu aliye ndani yangu atanishindia.
Napambana na hali yangu! Aisee bado napambana! Utajikuta unaendelea kumbana maisha yako yote sababu ya kuamini na kutamka mapambano. Maisha sio vita! Badala yake tumia msemo Nasonga mbele! au ninaendelea kufanikiwa.
Bado najitafuta! Unayemtafuta ni wewe mwenyewe. Maana yake umepotea unaishi katika utengano au umejitenga wewe mwenyewe. Tumia maneno nimejipata, nimejitambua, nimejifahamu!
Kuna nyimbo kama; "wanaume tumeumbwa mateso kuhangaika". Kama unaweza kuepuka kuimba, kusikiliza au kucheza wimbo kama huo ina faida kubwa sana kuliko hasara!