Misemo gani ya kijinga na kipumbavu watu hutumia kufarijiana?

Waliokudharau leo kesho watakuheshimu.
 
Ubaya wa misemo ya kiswahili inapingana yenyewe kwa yenyewe mfano
"Subira huvuta heri" inapingwa na
"Ngoja ngoja utakuta mwana si wako"

Hata huu wa Malipo ni hapahapa itakua tu na msemo mwingine wa kuupinga
Kuna swali la Kiswahili la kidato cha Nne,ambalo huuliza baadhi ya misemo,nahau na methali zimepitwa na wakati.Jadili
 
Hatuagizwi na Maboss sisi wenyewe Maboss.....Jichanganye kama hutalala Njaa
 
Kuna swali la Kiswahili la kidato cha Nne,ambalo huuliza baadhi ya misemo,nahau na methali zimepitwa na wakati.Jadili
Mfano wa misemo iliyopitwa na wakati ni
"Ukiona mwenzako ananyolewa zako zitie maji" huu msemo umepitwa na wakati watu wananyolewa na mashine nywele zinatakiwa ziwe kavu siyo lazima kuloanisha nywele.

Huo Msemo ufutwe hauleti maana kwa sasa
 
Sasa kama wewe ndio unapambana kwa juhudi zako binafsi, Huyo Mungu haitajiki na hana msaada wowote.

Ni kujifariji na kujipa matumaini uchwara kwamba kuna Mungu anayewezesha mipango yako ilhali ni wewe mwenyewe unapambana kwa juhudi zako binafsi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…