Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

1.Yatima hadeki.

2.Utamu wa chips mimba

3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni.

4. Usiyempenda kaja.

5. Kobe hapimwi joto.

6. Acha kazi uone kazi kupata kazi.

7. Ukichezea koki utalowa.

8. Heshima pesa kipara kovu tu!

9. Mtumbwi hauna saitmira.

9. Silaha pesa bastola mzigo.

10. Hata uoge mjini huendi

11. Chezea mshahara usichezee kazi.

12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa.

13. Ikisimama Panda

14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe.

15. Njia ya chooni haioti nyasi

16. Likizo ya maskini ugonjwa

17. When i grow up i want to be a scania

18. Hata bibi alikuwa binti

19. Kisigino hakikai mbele

20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki.

21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi.

22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee.

23. Paka haishi kwa msela

24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa.

25. Tako nalo lina nywele lakin hazinyolewi.

26. Mchana nzi ucku mbu

27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake.

28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako

29. Supermarket hawauzi mkaa

30. We nisubiri mi nakungoja.

31. Wakijifanya Mapanya sisi Paka tupo.


Ongeza na yako!
 
Dah Ila Watanzania Noma Sasa Misemo Hii Inawekwa Kwenye Mikokoteni Ya Kuvuta Wanyama Au Mtu Anaandika Jina La Bass Au Kari Zuri _at mtu kaandika ferrari kwenye mkokoteni wa ng'ombe mbaya zaidi kavaa shati imeandikwa wasafi ukimcheki nguo zinachakalia mwilini bila ya kufuliwa
 
Pesa tunapata tatizo...........
 

Attachments

  • 1424586959479.jpg
    1424586959479.jpg
    27.9 KB · Views: 646
Back
Top Bottom