Daladala zinaposimama kwenye foleni huwa zimeandikwa baadhi ya misemo kama hii :
1.Yatima hadeki.
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni.
4.Kobe hapimwi joto
5.Hâta Uwe na heshima vipi huwezi kumpokea Askari bunduki.
6.Pombe pombe tu kunywea bar mbwembwe
7.Kama mapenzi pesa kaolewe na banki.
8.njia ya chooni haioti nyasi.
9.Mavi hayana miba lakini ukikanyaga lazima uchechemee.
10.Silaha pesa bastola mzigo.
11.Hata bibi alikuwa binti.
12.Likizo ya maskini ugonjwa.
13.Mchana nzi usiku mbu.
14.Paka haishi kwa msela.
15.Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa.
16.Hata barabara ina matuta lakini huwezi panda viazi.
17.Usimshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake.
18.Supermarket hawauzi mkaa.
19.Mtimbwi hauna saitimira.
20.
21.
22.
23.
24.
25.
26.
Na misemo mingine mingi jaziliza....