Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

jr.jpg


Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

- Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
- Ukicheka na nyani utakula mabua.
- Hata ukioga, mjini huendi.
- Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
- Akikua ataacha!
- Hata kwetu wapo.
- Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
- Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
- Jino moja mswaki wa nini?
- Swali kabla hujaswaliwa.
- Dume kwenye mfuko wa nyuma?
- Usivue viatu kuna mbigiri.
- Changanya na zako!!!
- Unga robo, usicheze mbali.
- Butua uwakomboe wenzako.
- Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.
Siku hizi sio kweny kanga tu
 
Hizi maneno zingewekewa utaratibu wa kulipiwa kodi ya matamgazo tungepunguza utegemezi kwenye budget yetu.

"BABA YAKO ANALO" aliandika hayati Dr. Remmy ongalla kwenye mtukari wake.

Hongera kwa thread nzuri.
 
Back
Top Bottom