Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Ukinuna uwe na sababu.
Mchana Inzi,Usiku Mbu
Usiyempenda kaja.
 
Kapigwa Chini...Kavimba Juu

attachment.php
 
jr.jpg


Nimekuwa napenda sana kusoma misemo mbali mbali katika magari hasa mabasi ya abiria na yale ya mizigo.
Ndipo nilipoamua kuwauliza madereva, nani anayetaka maneno hayo yaandikwe? Majibu yao ni kuwa, wapo matajiri wanataka semi hizo ziandikwe, wakati mwingine ni madereva wenyewe huwa ndiyo wanaandika. Ila semi wanazoandika madereva ni zile zinazokuwa katika bomba au ngao (nyuma chini).

- Semi hizi zinabea maana kubwa sana ikiwa ni zaidi ya kufurahisha kwa wakati wake. Mfano,
- Ukicheka na nyani utakula mabua.
- Hata ukioga, mjini huendi.
- Ulifikiri kumwambia baba yako HALLO kwenye simu ndiyo heshima?
- Akikua ataacha!
- Hata kwetu wapo.
- Wanga sasa basi, ukimwi unatosha.
- Mimba mnatoa, Ukimwi je ?
- Jino moja mswaki wa nini?
- Swali kabla hujaswaliwa.
- Dume kwenye mfuko wa nyuma?
- Usivue viatu kuna mbigiri.
- Changanya na zako!!!
- Unga robo, usicheze mbali.
- Butua uwakomboe wenzako.
- Si ulisema tamu, unalia nini?

Naomba utushirikishe semi ulizowahi au unazozisoma toka katika magari hayo.

1.Kunja miguu shuka fupi
2.Hata huku wapo
3.Na leo kaseme tena
4.Hakuna komandoo wa mapenzi
5.raha ya nyumba choo
6.mwanaume asifiwi sura
7.kila siku bora ya jana
8.utamu wa chips mimba
9.mkubwa pesa mvii rangi tu
10.Mchawi binadam paka anatumwa tu
 
1) Maisha kutafuta kaburi unataftiwa.
2) ukitaka nji wasikufate achakula vilivyo oza.
3)baba kwenye mapenzi unazima taa huduma kwa mtoto hadi serekali za mtaa
 
Back
Top Bottom