Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

Misemo inayoandikwa kwenye vyombo vya usafiri, we acha tu!

1. Mwisho wa ubaya aibu
2. Hata mbuyu ulianza kama uyoga
3. Nibora kuishi na nyoka pangoni kuliko kuishi na mwanamke mkorofi
4. Kuwa mkweli leo ili usiadhirike kesho
5. Iga ufe
6. Kunya kanya kuku bata akinya kaharisha
7. Kesi ya nyani kapelekewa ngedere
8. Mwanamke kiuno makalio hata kwa mchina yapo
9. Baba kanikataza
10. Mali ni mateso
mkuu hiyo niliyobold kuna mzee mmoja kijijini kwetu (anajiita Mangosii) alikuwa na mandolini lake ameandika hivo... lol
 
FUATA UPOTEE

hii gari sitoisahau ilikuwa ni hiace inapiga ruti za kibena hospital -mjimwema ilikuwa inakimbia mbaya kwenye ile miteremko ya police na inzunilo ilikuja ilipata ajari mbaya sana na kuua abiria karibia wote na dereva alikatika miguu yote
 
FUATA UPOTEE

hii gari sitoisahau ilikuwa ni hiace inapiga ruti za kibena hospital -mjimwema ilikuwa inakimbia mbaya kwenye ile miteremko ya police na inzunilo ilikuja ilipata ajari mbaya sana na kuua abiria karibia wote na dereva alikatika miguu yote.

Msemo wake huo ni kweli ulishawapoteza wengi ukifukuzana nae tu anakupoteza (anakusababishia ajari )
 
Ninafurahishwa na misemo inayaoandikwa katika magari hususani daladala.

1. Silaha pesa Bastola mzigo
2. Hata uoge mjini huendi
3. Chezea mshahara usichezee kazi
4. Hata manyunyu ni mvua

Endeleza hapo.
 
Ninafurahishwa na misemo inayaoandikwa katika magari hususani daladala.

1. Silaha pesa Bastola mzigo
2. Hata uoge mjini huendi
3. Chezea mshahara usichezee kazi
4. Hata manyunyu ni mvua

Endeleza hapo.

1. Ubishoo bila hela sawa na upara bila elimu.

2.Abiria usije na sheria zako ndani ya gari; za serikali zinatushinda kwa wingi!
 
Back
Top Bottom