Misemo kutokana na Vichwa vya Treni

Na baada ya kukaa siku tatu bila kiki mfalme akaghazabika sana akasimama akashika kidevu chake na kusema nileteeni wale wote wasiotoa kiki hapa
Nayo majeshi yake yakamtii yakaanza kamata kamata nchi yote ya ukawa ili litimie neno lililonenwa na nabii Lisu "sijawai ona mfalme ovyo kama huyu" waraka wa kiki 2: 37
 
Ndipo Ndungai akamtuma akamuulize kama ni yeye au tumsubirie mwingine. Sizonje akamwambia nenda ukamwambie Bashite kuwa Treni zinajileta, Rambirambi zinaliwa na wapinzani wanafungwa.... Amin Amin nakuambia Matetemeko yatatotekea lakini serikali haitahusika. Kwa maana makinikia aliyonipa baba sitapoteza hata moja.

Prof Osoro: 16:12-15
 
Basi mfalme alipoona wadanganyika wamefurahi na kupendezwa baada ya kumweka rumande Ruge na Seth, akamwendea mwenyekiti wa TifuaTifua na Katibu wake nao akawaweka ndani. Hata yule Kanjibhai naye hakuweza kupona mbele ya mkono wenye nguvu wa mfalme Sizonje.
I wish I could be IGP 34: 3-6
 
Ndipp mfalme akawauliza makuhani na watoza ushuru.."Ni nani kati yenu awezaye kutenda miujiza hii bila mimi kujua?
basi nao wakamjibi kwa woga
"hajawahi tokea mtu mwenye uwezo wa kuomba neema bila kupitia wewe akapata" huku mioyoni mwao wakinungunika
Basi mfalme akasema
"pumbavu zenu nyie mliokosa maarifa ondoeni Mara moja hivyo vichwa" Baada ya kusema hayo akaondoka huku akijipiga kifuani huku amezungukwa na walinzi lukuki...
Basi watu wa nchi ile waliposikia maneno Yale wakalalama wakisema
Ama kwa hakika mfalme huyu ametukuka na akatawale milele (utawala wa mabavu 1;5:2015_2020)
 
Makutano wote wakastaajabu makinikia 217 zitowe Noha milioni 45 wakasema hakika hili ni jambo geni machoni petu
Mfalme akafedheheka sana akararua joho lake alipoona wadanganyika wameshtuka
Bulyankulu 6:9
 
Ndipo makada wakajipiga vifua na kugalagala kwenye mavumbi kama chatu huku wakisema, "ewe Sizonje tuchukue utumwani milele"
Lumumba 4 : 5-13
Hahaaaaaa. Mtanifanya nionekane kichaa kwa kucheka pekee. Haya maajabu yapo Tanzania tu.
 
Hata makada wakamwendea na kusema, " mfalme tumemwona lipumba akipiga watu kwa jina lako nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu", lakini mfalme akawaambia, "msimkataze, kwani asiyepingana nanyi yuko upande wetu". Elimubure10.
:7-11.
 
Yule nabii asiyesikilizwa akapaza sauti hata pembe nne za utawala ule!"amini amini nawaambia mpaka kufika hesabu ya 2020 mutashuhudia machukizo mengi kutoka kwa kuhani mkuu!"
Ufunuo wa ukawa 08:15-20
 
Angalieni majina ya watoto wenu mara mashoto, mara kinoge,mara masumbuko, mara pombe halafu unakuta mtoto kalewa saa zote hata bila kunywa shauri yenu mimi napita tu.
 
22.Walipopata taarifa kutoka galilaya kuwa kuna vichwa bandarini, basi mfalme na jeshi lake wakapanda punda na farasi kuelekea Bandarini kuona neema za Mungu zilivyotamalaki juu ya uso wa Nchi ile.

23.Mfalme akafika na kushuka kutoka kwa mwanapunda akapaza sauti mbele ya lango la bandari akisema : Ni nani mwenye kupinga juhudi hizi ? Wote wakanyamaza kimya na kumsujudia mfalme.

24. Malaika toka mbinguni wakashusha ndege mpya sita kutoka Kampuni kubwa ya BOEING nao wananchi waliposikia habari zile waliwasha runinga kuamnisha masikio na macho yao.

Sipangiwi 4:22-24
 
Mi nadhani ndugu zangu ifikie hatua tukue kifikra. Tunapaswa tuendeshe mijadala yenye tija kuhusu vichwa vya treni itakayomsaidia Rais wetu JPM na sio mizaha na kejeli za kipuuzi.
Ewe Nyamtalakyono ni nani aliyekuroga hata unashindwa kujua kuwa Kuhani mkuu na wasidizi wake anatufanyia maskhara kutuambia kuwa muujiza wa vichwa vya treni hawautambui?
Je kuna mtenda moujiza mwingine katika milki hii zaidi ya kuhani huyu ?wale makuhani wenye mitazamo tofauti wamezuia kufanya miujiza mpaka hesabu ya 2020 itmie!na wengine wamefukuzwa na msaidizi wa kuhani kutoka hekaluni kwa mwaka mmoja huku kuhani mkuu akiwasubiri nje ya madhabahu wafanye maombi kinyume chake awasulubu!hujui hayo!
Kweli kizai hichi kinapotea kwa kukosa maarifa
Not to that extent 15:20
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…