kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,875
Ikawa yule mtume na nabii mkuu alipoona umaarufu wake unashuka ,akawaita wasaidizi wake na kuwauliza watu wananizungumuziaje huku na huko. Nao wakamwambia kwasasa umaarufu wako kama unashuka kutokana na wao kukosa maziwa na asali uliyowaahidi toka mwanzo. Naye akiwa amejawa na gadhabu nyingi akauliza, je nifanyeje sasa ili nisikauke midomoni mwao na utukufu wangu udumu hadi itakapofika wakati uliokubalika?. Ndipo vijana wake aliowapenda upeo wakamwambia , ni wakati sasa wa kutengeneza miujiza ya ajabu katika nchi ambayo hakuna mtu awaye yote aliyewahi kuyafanya. Tazama kwa utukufu wako kila mkaazi juu ya nchi anaweza kupata Noah yake, tazama mvua ya vichwa vya treni vyaweza kushuka kama mana kutoka juu. Ndipo yule mwana mpendwa kuliko wote ambaye alimchagua kuongoza kile kitongoji maarufu akamwambia mtume na nabii mkuu, hakika bwana muda umefika na saa imetimia wa sisi wasaidizi wako kuwaweka ndani wale wooote wanaokupinga na kutupinga sisi watumishi wao. Nao wana wa nchi watakapouliza tutawaambia nabii ananyoosha nchi sawasawa na neno lake mwenyewe alilolinena, ( call me J 5:1_4)