Mishahara ilipwe kwa mkupuo wa miezi mitatu mitatu

Mishahara ilipwe kwa mkupuo wa miezi mitatu mitatu

Mtumishi gani anaweza kusubiri siku 90, Ndipo apokee mshahara wake ? Kama wapo ni wachache sana.akiupokea huo mshahara siku chache mbelenj hana ata mia maana madeni kibao mtaani.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Wapo wenye madeni na wasio na madeni, pia wenye madeni itawasaidia kukopesheka Tena pindi watapomaliza madeni yao kwa mkupuo, wasio na madeni wataendelea kuboresha vyanzo vya kuwaongezea kipato
 
ni ubunifu mzuri wenye lengo la kuwasaidia watumishi wenye kima cha chini, ambao ndio walio athiriwa zaidi na hali ngumu ya kimaisha.

Lkn pia waziri husika anaweza kuboresha njia bora zaidi ya kuwapunguzia makali ya maisha.
 
Mimi naona walipwe kwa wiki. Mfano mtu anayelipwa laki moja kwa sasa hivi mfumo wa wiki umruhusu kulipwa 25,000 kila wiki.
 
Nchi nyingi wanalipana kwa wiki. Pia hili linapunguza ukali wa maisha.
Sasa mkuu tumtazame anaelipwa kima cha chini cha mshahara, 250,000/=
Inamaana Kila wiki apokee 51,500/=?
Hapo atunze ili ifikie 400,000/= ya kumlipia Ada mwanae inabidi asubirie wiki ngapi?

Wakati huo angelipwa kwa mlimbikizo angepokea 750,000/=
Angetatua changamoto za ujumla
 
Sasa hao hata wakianza kazi na kipokea mishahara ni hivyo hivyo kwani mafisadi wanatoka wapi ndiyo hao hao wasio jua matumizi mazuri
Ndio kuna mwenzangu hapa ananambia yeye (akishapata kazi) chap anaomba mkopo wa mil 45 dah nikajisemea huyu si anataka kuwa mtumwa wa mkopo milele ila nilitaka kumuambia ila ni mbishi saaana nikamuacha.
 
Sasa mkuu tumtazame anaelipwa kima cha chini cha mshahara, 250,000/=
Inamaana Kila wiki apokee 51,500/=?
Hapo atunze ili ifikie 400,000/= ya kumlipia Ada mwanae inabidi asubirie wiki ngapi?

Wakati huo angelipwa kwa mlimbikizo angepokea 750,000/=
Angetatua changamoto za ujumla
Lakini hiyo miezi mitatu inayofuata ataishije, si mwisho wa siku atakuwa analala njaa na kula rushwa? Mshahara ni kukufanya uweze kuishi bila taabu huku ukifanya kazi zako vizuri. Tukienda kwenye extremeties. Maana yake kwa point yako mtu akilipwa kwa mwaka ni bora zaidi. Wakati kwa point yangu mtu akilipwa kwa siku ni bora zaidi. Unaona inafaa kulipwa kwa mwaka?
 
Ndio kuna mwenzangu hapa ananambia yeye (akishapata kazi) chap anaomba mkopo wa mil 45 dah nikajisemea huyu si anataka kuwa mtumwa wa mkopo milele ila nilitaka kumuambia ila ni mbishi saaana nikamuacha.
Anajua atakuwa analipwa mshahara kiasi gani!?
 
Lakini hiyo miezi mitatu inayofuata ataishije, si mwisho wa siku atakuwa analala njaa na kula rushwa? Mshahara ni kukufanya uweze kuishi bila taabu huku ukifanya kazi zako vizuri. Tukienda kwenye extremeties. Maana yake kwa point yako mtu akilipwa kwa mwaka ni bora zaidi. Wakati kwa point yangu mtu akilipwa kwa siku ni bora zaidi. Unaona inafaa kulipwa kwa mwaka?
Kwa miezi mitatu ni afueni.
 
Back
Top Bottom