Mishahara ilipwe kwa mkupuo wa miezi mitatu mitatu

Mishahara ilipwe kwa mkupuo wa miezi mitatu mitatu

Mpandisha mishahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2014
Posts
1,742
Reaction score
1,558
Habari wanajamvi, binafsi niliwaza na kuwazua ni jinsi gani mishahara inaweza kuwa na uzito kwa mfanyakazi.

Majibu niliyopata ni kwamba ifike hatua serikali ipitishe sheria ya kulipa mishahara kwa awamu moja ndani ya miezi mitatu mitatu,
Kwa mfano unalipwa take home ya milioni 1.

January ml 1
February ml 1
March ml 1

Hivyo mshahara wa March unaingia full digits milioni 3.

Hii ni njia Bora ya kuwasaidia wenye kipato kidogo cha mishahara kuweza kufanya mambo ya akiba kwa wepesi.

Ahsanteni na karibuni katika mjadala.
 
Hela ni ileile mkuu ni noti zilezile. Issue ni kuwa hatuna money management. Wengi wanajisahau na hata malezi yetu hayakazii kuhusu nidhamu ya pesa toka udogoni matokeo ndio hayo.
Kama unaweza kufanya kazi katika makampuni kwa mkataba wa miezi sita na ukalipwa hela ya miezi sita na bado kazi ikafanyika Bila tatizo la money management, why serikalini ishindikane?
 
Utofauti wa Boom na mshahara ni mkubwa, boom waliona Kama ni pesa za bure bure, lakini mshahara unausotea mkuu
Waliona ni hela ya bure lkn madhara si wanayaona pale makato kufidia mikopo ya elimu yanapoathiri mishahara. Kwa mtu mwny nidhamu ya pesa kupewa hyo hela ya mkupuo kama unavoshauri n8 bingo sana kwani ataitumia vzr hata kuzalisha nyingne.

Ila nikiungana na mtoa mada mmoja aliyesema kama wa mwezi kama siku kadhaa tu kwisha je wa miezi mitatu? Kiufupi kwa Bongo sidhani.
 
Waliona ni hela ya bure lkn madhara si wanayaona pale makato kufidia mikopo ya elimu yanapoathiri mishahara. Kwa mtu mwny nidhamu ya pesa kupewa hyo hela ya mkupuo kama unavoshauri n8 bingo sana kwani ataitumia vzr hata kuzalisha nyingne. Ila nikiungana na mtoa mada mmoja aliyesema kama wa mwezi kama siku kadhaa tu kwisha je wa miezi mitatu.?kiufupi kwa Bongo sidhani.
Ukiwaweka watu kumi, uwape laki 8 Kila mwezi. Wapo ndani ya wiki wataokuwa wamemaliza, pia wapo ndani ya mwezi watakaokuwa hawajamaliza, Matumizi ya pesa ni akili yako tu.
 
Kama unaweza kufanya kazi katika makampuni kwa mkataba wa miezi sita na ukalipwa hela ya miezi sita na bado kazi ikafanyika Bila tatizo la money management, why serikalini ishindikane?
Nadhani time limit ndio hushtua watu ila ajira serikalini jusahaulisha watu kujiandaa. Kazi za miakataba wakati mwngne ni chachu ya maendeleo
 
Back
Top Bottom