Niliwahi kuambiwa kuwa jamii ina chuki sana na watu wa afya.
Na hata maafisa wengi wasio idara hii wana chuki na kada hizi za afya.Wengi wanajua hii chuki,ndio maana hata mgonjwa akienda hospitali, hawaoni shida kuomba rushwa.
Chuki hizi zimeletwa na kuwepo idadi ndogo ya watumishi wa afya ambapo wanaohitaji huduma ni wengi.
Lakini pia kuwepo malipo ya huduma za afya kumefanya chuki izidi kuwa kubwa.
Sababu ugonjwa ni maumivu,kutoa pesa ni maumivu mengine,kukosa huduma kwa sababu umekosa pesa,ni maumivu mara mbili,na wanaoonekana ni hawa watumishi wa afya.
Kama serikali isipoajiri wengi,na kuweka bima ya afya kwa wote, hizi chuki hazitoisha