Mishahara kada za Afya iongezwe, wanahatarisha sana maisha yao

Mtu kaona waongezewe , wewe unapinga ili Nini? Wamekuzuia wewe kudai nyongeza? Mchawi wa mtumishi sio serikali ni Hawa viherehere wanaojifanya watetezi wa serikali... Kumbe wivu umefurika mioyoni na nafsini mwao.!!
Wajinga ni wengi sana kiufupi kwenye serikali mishahara haikidhi viwango gepu kubwa sana kati ya wanasiasa na watendaji na ukicheki wanaowajibika na shuguli zote ni watendaji na sio wanasiasa.
 
Niambieni mshahara wa
Daktari Bingwa
Dactari GP
Afisa Tabibu
Tabibu msaidizi

Nurse Degree
Nurse diploma
Nurse certificate

Pharmacist
Pharm Tech
Pharm assistant

Halafu ndo nichangie hoja yangu
MD 1.4M+ akiwa na mkopo anaweza jikuta anaondoka 8-900k
Diploma zote mshahara take home 620k kwa ninavyojua source ni rafiki zangu
 
Mazingira ya hawa yanahitaji kuwa jasiri; kushuhudia watu wanakata moto si mchezo; au mgonjwa ametobolewa tumbo unatakiwa umtibu n.k
Mkuu Kuna watu wanafanya kazi katika mazingira magumu Mara 10 zaidi ya huyo anayeshuhudia mtu akikata moto mbele yake, ni basi tu sio wote Wamejaliwa kuongea.
 
Mkuu Kuna watu wanafanya kazi katika mazingira magumu Mara 10 zaidi ya huyo anayeshuhudia mtu akikata moto mbele yake, ni basi tu sio wote Wamejaliwa kuongea.
Niliwahi fanya kazi sehemu watu wa mochwari walikua wanalalamika sana maslahi nikaona aah si kweli wakagoma kwa muda wa wiki tu habari tuliipata.
 
Kama wanalipwa 2m. Mbona yeye kapendekeza angalau diploma alipwe 1.5m uyo wa 2m ni nurse wa nchi gani
 
Yani kada ya afya kuna wanaohatarisha pia maisha yetu tena wengi mno. Ety daktari badala akuchome sindano kidoleni anakupima mapigo ya moyo ya matrakroni.
 
kama ww unaondoka na 15M basi afisa wa TRA ataondoka na 100M
Inawezekana kabisa mkuu. Kuchoropoa tuu ma MDs wanakula vichwa vya kutosha kila siku. TRA sidhani , labda TPA customs na watu wa boarder
 
Na kada ya Udereva pia iongezwe wanahatarisha sana maisha yao.
 
Tukiacha kazi wewe ndio wa kwanza kufa kutokana na roho yako ilivo nzuri.
 
Na wewe nenda kawe mbunge
 
Inawezekana kabisa mkuu. Kuchoropoa tuu ma MDs wanakula vichwa vya kutosha kila siku. TRA sidhani , labda TPA customs na watu wa boarder
tra sehemu yenye mianya mingi ya rushwa kuliko kwenye afya
 

esi mwenye degree mshahara wake milioni haifiki sembuse diploma

Hata nesi mwenye degree mil 1 hafiki,acha ujuaji na stori za vijiweni walio kwenye field wanaelewa uhalisia mkuu
 
Niliwahi kuambiwa kuwa jamii ina chuki sana na watu wa afya.
Na hata maafisa wengi wasio idara hii wana chuki na kada hizi za afya.Wengi wanajua hii chuki,ndio maana hata mgonjwa akienda hospitali, hawaoni shida kuomba rushwa.

Chuki hizi zimeletwa na kuwepo idadi ndogo ya watumishi wa afya ambapo wanaohitaji huduma ni wengi.
Lakini pia kuwepo malipo ya huduma za afya kumefanya chuki izidi kuwa kubwa.
Sababu ugonjwa ni maumivu,kutoa pesa ni maumivu mengine,kukosa huduma kwa sababu umekosa pesa,ni maumivu mara mbili,na wanaoonekana ni hawa watumishi wa afya.
Kama serikali isipoajiri wengi,na kuweka bima ya afya kwa wote, hizi chuki hazitoisha
 
Kama unaona pesa ni ndogo acha kazi ,Kuna wimbi kubwa la watu wa afya wanabeba zege mitaani na wanahitaji hata laki na nusu kwa mwezi hawaipati.

Kwa hiyo ni maamuzi yako tu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…