Zimeokolewa kiasi gani? Tunao watumishi wangapi? Itapanda maradufu ni uwongo mkubwa! Hivi unaelewa tukisema mishahara imepanda mara mbili, mara 3 au mara 4? Hiyo maradufu maana yake nini? Unamaanisha zaidi ya mara 10 au 50? Hata kama mishahara itapanda naamini itakuwa ni kwa ongezeko la asilimia fulani tu, haiwezi kupanda hata mara mbili ya walichokuwa wakipata, achilia mbali hiyo maradafu iliyotajwa na mshereheshaji.
Bahati mbaya ya Watanzania walio wengi, kiingereza hatujui, hata lugha yetu ya Kiswahili nayo hatuijui, ni nini tunachojua?