Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Watumishi wa umma kaeni mkao wa kupokea mishahara minene. Kwa muda mrefu sasa tangu Dr Magufuri aanze kurekebisha mifumo ya utawala wa nchi, watumishi wa umma walionekana kama wametengwa sana hadi baadhi yao kupelekea kukata tamaa ya maisha. Sasa mkae mtulie…mambo yenu yameiva!
Kuna taarifa kwamba Serikali imepanga kuongeza mishahara ya umma maradufu ifikapo September baada ya kufanikiwa kuwaondoa watumishi na wanafunzi hewa na kupunguza mishahara ya baadhi ya watumishi waliokuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi huku wengine wakilipwa mishahara uchwara, hivyo fedha zote zilizookolewa zimeelekezwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamikia udogo wa mishahara kwa muda mrefu. Aidha, taarifa zinadai kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda vyeo/madaraja watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara mipya mara moja.
Ifahamike kwamba wakati Dr Magufuri anaomba ridhaa ya kuongoza nchi hii aliwaahidi maslahi bora watumishi wa umma, hivyo ahadi yake ndio inaanza kutekelezwa sasa. Kumbe lilikuwa ni suala la wakati tu. Sasa civil service imeanza kupata mwanga uliokuwa umekosekana kwa muda mrefu na kupelekea watumishi wa umma kuvunjika mioyo ya kuwatumikia wananchi. Hongerza sana Dr Magufuri kwa kuwajali watumishi wa umma.