Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Tetesi: Mishahara kupanda maradufu!

Status
Not open for further replies.
Hayawi hayawi sasa yamekuwa! Watumishi wa umma kaeni mkao wa kupokea mishahara minene. Kwa muda mrefu sasa tangu Dr Magufuri aanze kurekebisha mifumo ya utawala wa nchi, watumishi wa umma walionekana kama wametengwa sana hadi baadhi yao kupelekea kukata tamaa ya maisha. Sasa mkae mtulie…mambo yenu yameiva!


Kuna taarifa kwamba Serikali imepanga kuongeza mishahara ya watumishi wa umma maradufu ifikapo September baada ya kufanikiwa kuwaondoa watumishi na wanafunzi hewa na kupunguza mishahara ya baadhi ya watumishi waliokuwa wakilipwa mamilioni ya shilingi huku wengine wakilipwa mishahara uchwara, hivyo fedha zote zilizookolewa zimeelekezwa kuongeza mishahara ya watumishi wa umma ambao wamekuwa wakilalamikia udogo wa mishahara kwa muda mrefu. Aidha, taarifa zinadai kuwa watumishi wote wanaostahili kupanda vyeo/madaraja watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara mipya mara moja.


Ifahamike kwamba wakati Dr Magufuri anaomba ridhaa ya kuongoza nchi hii aliwaahidi maslahi bora watumishi wa umma, hivyo ahadi yake ndio inaanza kutekelezwa sasa. Kumbe lilikuwa ni suala la wakati tu. Sasa civil service imeanza kupata mwanga uliokuwa umekosekana kwa muda mrefu na kupelekea watumishi wa umma kuvunjika mioyo ya kuwatumikia wananchi. Hongerza sana Dr Magufuri kwa kuwajali watumishi wa umma.
Unatoa pongezezi za ahadi!?!?
 
September 1:
Maandamano ya UKUTA nchi nzima.

September 1:
Siku ambayo jeshi la wananchi Tanzania litafanya usafi huko Arusha.

September 1:
Imetajwa kua siku ya kuongezwa mishahara kwa wafanyakazi wa uma, ikiwemo kupandishwa vyeo kwa wanao stahili.

September 1:
Dr Slaa ana timiza mwaka mmoja kuanzia pale 1 September 2015, alipo tangaza rasmi kujingatua Chadema na kujiondoa kwenye siasa.
Umesahau kupatwa kwa jua
 
Watumishi wa umma mtasubiri sana. Kumbuka hata uteuzi wa mawaziri tuliusubiri sana mwisho wa siku hakuna kipya
 
Namsikiliza Kairuki Tbc 1 mikataba wakiweka mshahara lazima ipandishwe mara dufu aiseh!!
 
mleta taarifa huyu ahaminiki , kwani ni mmoja wa wanajukwaa wanaopinga kwa kejeli juhudi za rais kuifanya Tanzania inayojitegemea kiuchumi na kijamii,.
 
U
September 1:
Maandamano ya UKUTA nchi nzima.

September 1:
Siku ambayo jeshi la wananchi Tanzania litafanya usafi huko Arusha.

September 1:
Imetajwa kua siku ya kuongezwa mishahara kwa wafanyakazi wa uma, ikiwemo kupandishwa vyeo kwa wanao stahili.

September 1:
Dr Slaa ana timiza mwaka mmoja kuanzia pale 1 September 2015, alipo tangaza rasmi kujingatua Chadema na kujiondoa kwenye siasa.
Usiache la kupatwa na jua mkuu!
 
Umesahau kupatwa kwa jua
Na hizi pia zina husika tarehe moja.
1472397675335.jpg
1472397727467.jpg

U

Usiache la kupatwa na jua mkuu!
 
Binafsi nimechoshwa na hizi stori za kupanda kwa mishahara zipo tokea July bt cjaona ukweli wwte kuhusu hili jambo so cjaona umuhimu zaidi ya kutujazia screen saver zetu hapa!
 
....
....aiseeh J4 watu wana Akili sanaaaaaaa duh....weita wape mbili mbili kila moja humu Jamvini
 
mkuu, kuanzia septemba mishahara itapanda na watumishi wanaostahili kupanda vyeo watapandishwa na kuanza kulipwa mishahara yao mara moja.

#tpaul...

Ujue una heshima yako na hekima zako hapa JF...

Una uhakika na hili..? Usije wapa watumishi wa umma moyo, alafu ukute hakuna kitu... watakufa watu..

So ebu leta details vizuri
 
Vipi kuhusu uhamisho wa watumishi
mkuu, serikali imeishapiga marufuku tabia ya kuwahamisha watumishi pasipo malipo...mtumishi ukihamishwa inapaswa ulipwe kwanza ndipo uhame.
 
Kwa hilo next week watu wanaanza kula mishahara mipya?
 
Duu kama kweli safi but mi mpaka nione huyu mshahara kwanza ndo niamini hyo kitu la sivy badoo sna tu
 
Mkuu tpaul hiyo hela yenyewe ya kuongeza mishahara mara mbili itatoka wapi? Ni jambo zuri kuongeza mishahara kwa wafanyakazi wa umma hata mara tatu, lakini Serikali hii haina pesa na mapato ya Serikali yanaanguka kwa kasi ya kutisha labda wakaombe mkopo mwingine wa trilioni kadhaa Exim Bank ya kule China ili waweze kufanya hivyo.
Madeni yenyewe yamewashinda kuwalipa watumishi ,miaka nenda rudi ni uhakiki na ahadi zizizo na ukomo;je Leo uwezo wa kuongeza mishahara watatoa wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom