CMH
Member
- Jun 12, 2015
- 69
- 22
Alete waraka akamatwe?!Jamaa aliambiwa alete waraka but mpaka sasa hakuna taarifa zozote!!! Amekula chimbo!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Alete waraka akamatwe?!Jamaa aliambiwa alete waraka but mpaka sasa hakuna taarifa zozote!!! Amekula chimbo!!!
Wa TRA sio wafanyakazi wa serikali? Nafikiri wao ndio wanaoongoza kuliko hata madaktari, na bado wanashiriki kwenye ukwepaji kodi.SERIKALI imesema wafanyakazi wa sekta ya afya ndio wanaopokea viwango vikubwa vya mishahara wakifuatiwa na wale wa sekta ya elimu nchini.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora), Angela Kairuki, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalumu, Zubeda Sakuru (Chadema).
Katika swali lake, Sakuru alitaka kujua Serikali inakabiliana vipi na changamoto za masilahi kwa watumishi katika sekta ya afya.
Sakuru alisema kuna matukio ya vifo visivyo vya lazima vinavyotokana na ukosefu wa motisha kwa madaktari na wauguzi, ambao wanalipwa viwango vidogo vya mishahara na hawalipwi posho zao kwa wakati.
Akijibu swali hilo, Kairuki alisema Serikali imeendelea na jitihada za kuboresha mishahara ya watumishi wake, ikiwamo wataalamu wa sekta ya afya kwa kuzingatia uwezo wa kifedha.
Alisema kwamba mishahara huzingatia ngazi ya elimu, ambapo ngazi ya astashahada kwa upande wa Serikali Kuu ni Sh 390,000, kada ya walimu Sh 419,000, wauguzi Sh 432,000 na madaktari ni Sh 432,000.
Kwa upande wa stashahada, Serikali Kuu ni Sh 525,000, walimu 530,000 wauguzi 680,000 na madaktari ni Sh 680,000.
Kairuki alisema ngazi ya shahada kwa upande wa Serikali Kuu ni Sh 710,000, walimu 716,000, wauguzi 980,000 na madaktari ni Sh 1,480,000.
Pamoja na hayo, alisema Serikali inaendelea na utafiti wa tathmini ya kazi na itakapokamilika, itapanga upya mishahara na motisha kwa watumishi wote wa umma ikiwamo sekta hiyo.
“Kati ya mwaka 2010/11 hadi mwaka 2016/17,vianzia vya mishahara kwa kada za wauguzi vimeongezeka kutoka shilingi 614,000 hadi 980,000 kwa mwezi kwa wahitimu wa shahada.
“Vimeongezeka pia kutoka shilingi 425,000 hadi shilingi 680,000 kwa wahitimu wa stashahada na shilingi 260,000 hadi shilingi 432,000 kwa wahitimu wa astashahada.
“Kwa kada ya madaktari na maofisa tabibu katika kipindi hicho, vimeongezeka kutoka shilingi 886,800 hadi shilingi 1,480,000 kwa wahitimu wa shahada na shilingi 425,000 hadi shilingi 680,000 kwa wahitimu wa stashahada na shilingi 260,000 hadi shilingi 432,000 kwa wahitimu wa astashahada.
“Pamoja na hayo, Serikali itaendelea kuboresha masilahi ya waatumishi kadiri uwezo wake wa kulipa utakavyoimarika,” alisema Kairuki.
Chanzo: Mtanzania
Wa TRA sio wafanyakazi wa serikali? Nafikiri wao ndio wanaoongoza kuliko hata madaktari, na bado wanashiriki kwenye ukwepaji kodi.
ACHA AKILI TOPE HAKUNA KITU KAMA HICHO HII NCHI HAINA PESA NA MISHAHARA HIYO ITAONGEZWA KUPITIA BAJETI GANI,? CCM IMECHOKA HAKUNA JIPYA ZAIDI YA MATAMKOHABARI
SALARY KWA MWEZI September 2016
1.TGTS A1-546,000
2.TGTS B1-694, 000
3.TGTSC1-782,500
4.TGTS D1-939,000
5.TGTS E1-1,319,000
6.TGTS F1-1,653,000
7.TGTSG1-1,970,000
8.TGTSH1-2,584,000
9.TGTSI1-2,865,000
PROVED.......... HAPA KAZI TU
TGS A1~ 746,000
TGS B1 ~894.000
TGS C1 ~982,500
TGS D1~ 1,139,000
TGS E1~ 1,219,000
TGS F1 ~1,4053,000
TGS G1 ~1,670,000
TGS H1~ 1,884,001~ 2,665,000.
Hiyo ndiyo mishahara mipya ambayo waraka umetoka IJUMAA.
Inaanza kutumika September 2016.
NOTE:NI TETESI SIJADHIBITISHA
HABARI
SALARY KWA MWEZI September 2016
1.TGTS A1-546,000
2.TGTS B1-694, 000
3.TGTSC1-782,500
4.TGTS D1-939,000
5.TGTS E1-1,319,000
6.TGTS F1-1,653,000
7.TGTSG1-1,970,000
8.TGTSH1-2,584,000
9.TGTSI1-2,865,000
PROVED.......... HAPA KAZI TU
TGS A1~ 746,000
TGS B1 ~894.000
TGS C1 ~982,500
TGS D1~ 1,139,000
TGS E1~ 1,219,000
TGS F1 ~1,4053,000
TGS G1 ~1,670,000
TGS H1~ 1,884,001~ 2,665,000.
Hiyo ndiyo mishahara mipya ambayo waraka umetoka IJUMAA.
Inaanza kutumika September 2016.
NOTE:NI TETESI SIJADHIBITISHA
si kweli. hakuna waraka huoHiyo Kitu Ni Ya Kweli Kabisa Kuna Jamaa Yangu Anafanya Kazi Ktk Halmashauri Flani Upande Wa LAWSON huu waraka wanao tayari na kila halmashauri kwa uhakika zaidi tafuta mtu yoyote anayefanya kazi kitengo hicho ktk halmashauri yako