Mishahara Midogo Serikalini: Serikali iingie makubaliano na taasisi za fedha watumishi wakope kupitia posho na pia sheria ya moja ya tatu itazamwe upy

Mishahara Midogo Serikalini: Serikali iingie makubaliano na taasisi za fedha watumishi wakope kupitia posho na pia sheria ya moja ya tatu itazamwe upy

Ukweli ni kwamba, kwa miaka mingi mishahara serikalini imekuwa duni na bahati mbaya zaidi, uwezo wa serikali kuongeza mishahara sasa unaonekana kushuka na bila shaka sababu kubwa ni serikali kuwa na miradi mikubwa na ya gharama pasipo kuwa na vyanzo vya uhakika (hawakujipanga).

Hivyo, kutokana pia na ukweli kuwa sababu mojawapo kubwa ya watumishi kutaka nyongeza ya mishahara ni ili wakopesheke katika taasisi za fedha hasa mabenki ili waweze kuendesha maisha yao ikwamo kupata mitaji, kujenga, n.k.

Hata hivyo, watumshii wengi kwa sasa hawakopesheki kutokana na kubanwa na sheria inayotaka mtumishi kubaki na walau na moja ya tatu ya mshahara wake baada ya makato yote yakiwemo makato ya alzima kisheria ( PAYE, BIMA YA AFYA, n.k).

Hivyo, ili kuwasaidia watumishi ambao kwa sasa ni kama wako katika mkwamo baada ya kupata nyongeza isiyotosheleza mahitaji wala kuwawezesha kukopa, nashauri serikali ifanya mambo yafuatayo:-

1. Watumishi sssa waruhusiwe kukopa kupitia posho wanazopata kila mwezi.

Serikali, kwa kushirikiana na taasisi za kifedha kama mabenki, waingie makubaliano kuruhusu posho zinazolipwa kila mwezi zitumike kuombea mikopo walau ya muda mfupi ( mwaka mmoja mpaka miaka miwili ikiwezekana).

Posho serikalini ziko za aina nyingi na ziko ambazo hulipwa karibu kila mwezi na hizi ndio hasa zinaweza kutumika katika mpango huu wa kuwasaidia watumishi waweze kukopesheka.

2. Serikali itazame upya sheria inayoka mtumishi abaki na walau moja ya tatu ya mshahara ghafi wake (basi salary).

Kutokana na tofauti kubwa ya mishahara serikalini, si sahihi kuwataka watumishi wote kubaki na walau moja ya tatu ya basic salary zao wakati wana viwango tofauti vya mishahara.

Kwa mfano, mtumishi mwenye mshahara wa milioni moja na nusu au zaidi, kwaninii asipewe wigo mkubwa zaidi wa kukopa kulingana na mshahara wake?

Nafikiri wakati umefikia sheria hii itazamwe upya kuruhusu watumishi wenye mishahara mikubwa wakope zaidi kwani bado wanaweza kubaki na take home ya kutosha kuendesha maisha yao japo siku zote mshahara huwa hautoshi.

Kama ambavyo sheria au taratibu hubadilishwa kulingana na mahitaji ya wakati, basi ni wakati sahihi kwa serikali kubadili hii sheria/kanuni kuwwzesha watumishi kukopa na kuendesha maisha yao.

Kama serikali haitaki kubadili hii sheria na kuruhusu baadhi ya posho kutumika kuchukulia mikopo, basi iwe tayari kuboresha masilahi ya watumishi ikiwemo kuongeza mishahara ya wafanyakazi kwa kiwango cha kuridhisha.
Anayeona mshahara mdogo aache kazi
 
Back
Top Bottom