Mishahara mikubwa waliokuwa wanalipana Nyerere na viongozi wenzake kweli ilikuwa ni sahihi

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.

mwl-julius-k-nyerere.jpg

Rais wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere "MSHAHARA wangu ni Shilingi elfu tano kwa mwezi. Shilingi elfu tano katika nchi masikini. Masikini anayepata shilingi 200 kwa mwezi itamchukuwa miaka 25 kufikia kiwango cha mshahara wangu kwa mwezi. ndiyo nakubaliana na nyinyi kwamba tunalipana (Viongozi) mishahara mikubwa mno, na nitahakikisha mishahara hii tunayolipana inarekebishwa."

Maneno haya aliyatamka mwaka 1966. Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walioandamana hadi Ikulu kupinga kwenda JKT na pia kulalamikia mishahara minono ya viongozi wa serikali.

Cc; Jasusi, Nguruvi3, WildCard, Profesa, Mzee Mwanakijiji, adolay, Barubaru, ZeMarcopolo, JokaKuu, Sideeq, chama, FaizaFoxy, gombesugu, JMUshi, Zinedine, Mchambuzi, EMT, Pasco, JingalaFalsafa, Kimbunga,

Tabaka la watawala siku zote liko hivyo. Hata nchi za kikomunisti watawala waliwaambia wenzao wasimiliki mali kumbe wenyewe wamejihifadhia utajiri mkubwa nje ya nchi na nchini kwao.

Kila mtu inampasa kufanya kazi kwa bidii kupata kile anachokihitaji na kukitaka.
 
Ritz Sio sahihi na ndio maana alikuwa muwazi kupita kiasi na kusema kuwa watarekebisha maana ni mikubwa huku nchi ni maskini!

Huyu Babu yetu alikuwa muwazi na mwenye uzalendo uliotukuka tofauti na marais waliomfuata akiwemo Babaako nawewe ka-rais msaidizi na tajiri kuliko hata mzee Mengi!

Tunajua janja yako kwanini umeleta uzi huu; ni wazi unataka kuhalalisha mishahara mnazolipwa za kufuru kwamba hata enzi za Nyerere haya pia yalikua yanatendeka! Kwamba sio ajabu na ninyi mkifanya!

Inaonyesha dhahiri jinsi mlivyokosa vision lakini bado kitambo kidogo tu mtavuna mlichokipanda! Mtatuambia ni kwanini mmeifanya nchi yetu Mama-Tanzania shamba la Bibi yenu! Poor you..
 
Last edited by a moderator:
Sio sahihi na ndio maana alikuwa muwazi kupita kiasi na kusema kuwa watarekebisha maana ni mikubwa huku nchi ni maskini!

Huyu Babu yetu alikuwa muwazi na mwenye uzalendo uliotukuka tofauti na marais waliomfuata akiwemo Babaako nawewe ka-rais msaidizi na tajiri kuliko hata mzee Mengi!

Tunajua janja yako kwanini umeleta uzi huu; ni wazi unataka kuhalalisha mishahara mnazolipwa za kufuru kwamba hata enzi za Nyerere haya pia yalikua yanatendeka! Kwamba sio ajabu na ninyi mkifanya!

Inaonyesha dhahiri jinsi mlivyokosa vision lakini bado kitambo kidogo tu mtavuna mlichokipanda! Mtatuambia ni kwanini mmeifanya nchi yetu Mama-Tanzania shamba la Bibi yenu! Poor you..
Hizo ni fikra zako wapi nimekuambia kuwa natetea mishahara wanayolipana viongozi sasa hivi.

Mimi sina uhusiano wowote na Rais Kikwete, unachofanya ni makosa Name Calling.

Huu ni mjadala huru.
 
Hivi Jk analipwa ngapi?
Tukijua basi pia tutafahamu Maria nyerere anachukua kiasi gani kwa mwezi (80% mshahara wa rais) kutoka katika pesa za walipa kodi wasio weza kupata milo miwili tu kwa siku.
 
Ritz Tuwekee mshahara wa Kikwete ndo tuujadili, huo wa Nyerere hautusaidii kwa sasa.
 
Last edited by a moderator:
Ritz Tuwekee mshahara wa Kikwete ndo tuujadili, huo wa Nyerere hautusaidii kwa sasa...
 
Last edited by a moderator:
hoja ya mfu.. wewe badala ujadili kinana anavyomaliza tembo wetu, kikwete anavyizunguka duniani kama vasco da gama, asilimia 3 za madini tunazopata kutoka kwenye mrabaha. Unatuletea hoja za kpuuuuuzi
 
Nilijua utatia team una kiherehere dah ngoja ninyamaze nisije nikapigwa ban kwasababu ya huu utumbo ulioandika hapo juu
 
Mshahara wa shilingi 5 kwa mwaka kwa Rais si mkubwa kiasi hicho kama unavyotaka tuamini. Niliwahi kuhadithiwa na Mzee mmoja yeye wakati anaanza kazi miaka ya mwanzoni 70 alianza na kima cha chini cha shilingi 280 kwa mwezi. Wakati huko Dollar moja ya kimarekani ilikuwa ni sawa na shilingi tano za Tanzania na ndiyo likazaliwa jina la dala kwa shilingi tano na shilingi 20 yetu ilikuwa ni sawa na Pound moja ya kwa mama. Mzee huyo aliniambia kwamba pamoja na mshahara huo maisha yalikuwa ni rahisi mno watu kuweza kumudu gharama zao za maisha, kujirusha kila weekend na pia kuweza kuweka akiba katika bank accounts zao.

Kwa mshahara huo Mwalimu alipata haki yake halali hakufanya ufisadi wa aina yoyote ukilinganisha na waliokuja baada yake Mwinyi, Mkapa, Kikwete ambao wote ni mafisadi wa hali ya juu.
 
Hizo ni fikra zako wapi nimekuambia kuwa natetea mishahara wanayolipana viongozi sasa hivi.

Mimi sina uhusiano wowote na Rais Kikwete, unachofanya ni makosa Name Calling.

Huu ni mjadala huru.

Siku zote najua huna uhusiano na JK na nawaşhangaa sana wanaodhani wewe ni Ridhiwani.

Turudi kwenye mada. Kuna mtu yeyote mwenye uhakika kama kweli mishahara ilirekebishwa. Mshahara wake uliwa kiasl gani baada ya marekebisho? Na je kwa sasa Rair analipwa kiasi gani?
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Huyu tuliyenaye sina hakika kama anaweza kusema analipwa ngapi kwa mwezi na kamaanaweza kufikiria kupunguza kiwango (Kama ni kikubwa)
 
Mshahara wa shilingi 5 kwa mwaka kwa Rais si mkubwa kiasi hicho kama unavyotaka tuamini. Niliwahi kuhadithiwa na Mzee mmoja yeye wakati anaanza kazi miaka ya mwanzoni 70 alianza na kima cha chini cha shilingi 280 kwa mwezi. Wakati huko Dollar moja ya kimarekani ilikuwa ni sawa na shilingi tano za Tanzania na ndiyo likazaliwa jina la dala kwa shilingi tano na shilingi 20 yetu ilikuwa ni sawa na Pound moja ya kwa mama. Mzee huyo aliniambia kwamba pamoja na mshahara huo maisha yalikuwa ni rahisi mno watu kuweza kumudu gharama zao za maisha, kujirusha kila weekend na pia kuweza kuweka akiba katika bank accounts zao.

Kwa mshahara huo Mwalimu alipata haki yake halali hakufanya ufisadi wa aina yoyote ukilinganisha na waliokuja baada yake Mwinyi, Mkapa, Kikwete ambao wote ni mafisadi wa hali ya juu.
Hakuna sehemu yoyote niliyokutaka uamini. Nilichoweka ni maneno ya Nyerere mwenyewe.
 
Siku zote najua huna uhusiano na JK na nawahangaa sana wanaodhani wewe ni Ridhiwani.

Turudi kwenye mada. Kuna mtu yeyote mwenye uhakika kama kweli mishahara ilirekebishwa. Mshahara wake uliwa kiasl gani baada ya marekebisho? Na je kwa sasa Rair analipwa kiasi gani?
Sifahamu msahara wa rais. Kama kuna mtu anayefahamu atawekee.
 
Haya tuambie na kwa mshahara wa Mkapa je yule wa kima cha chini ingemchukua miaka mingapi kuufikia mshahara wa Mkapa kwa kima cha chini cha awamu yake, na kwa awamu ya Kikwete wa kima cha chini itamchukua miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete!?

Hakuna sehemu yoyote niliyokutaka uamini. Nilichoweka ni maneno ya Nyerere mwenyewe.
 
Hizo ni fikra zako wapi nimekuambia kuwa natetea mishahara wanayolipana viongozi sasa hivi.

Mimi sina uhusiano wowote na Rais Kikwete, unachofanya ni makosa Name Calling.

Huu ni mjadala huru.

OK, rais Kikwete yeye analipwa shilingi ngapi?
 
Nyerere alikuwa muwazi na kutangaza mshahara wake hadharani kwa wale walipa kodi waliokuwa ndio wanaomlipa mshahara wake. Unadhani kwanini Mwinyi, Mkapa na Kikwete waliamua kufanya mishahara yao siri ukilinganisha na Mwalimu ambaye aliutangaza mshahara wake hadharani!?

Back
Top Bottom