Mishahara mikubwa waliokuwa wanalipana Nyerere na viongozi wenzake kweli ilikuwa ni sahihi

Mishahara mikubwa waliokuwa wanalipana Nyerere na viongozi wenzake kweli ilikuwa ni sahihi

Kwani mapungufu ya Nyerere yanamfanya JK kuwa Kiongozi Imara
Mantiki ni hii"Hatushindanishi Ubovu" nyerere pamoja na mapungufu yake kama binadamu hakuna kiongozi wa Tanzania anayeweza kulinganishwa naye labda kwa Mbali Sokoine,ila siwezi kumuweka sababu akuwai kuwa Rais
 
Kuna nukuu nyingi za Nyerere kukemea na kuchukua hatua,sijaona nukuu za viongozi wenu waliotanguliza matumbo yao mbele,kila kiongozi akitaka kukemea uovu anamnukuu Nyerere,kwanini isiwe Kikwete,Mkapa,Mwinyi
"Vox popoli vox dei"
 
Kwani mapungufu ya Nyerere yanamfanya JK kuwa Kiongozi Imara
Mantiki ni hii"Hatushindanishi Ubovu" nyerere pamoja na mapungufu yake kama binadamu hakuna kiongozi wa Tanzania anayeweza kulinganishwa naye labda kwa Mbali Sokoine,ila siwezi kumuweka sababu akuwai kuwa Rais
Nani kakuambia tunashindanisha? Kila ufisadi na zama zake.
 
Rais wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere "MSHAHARA wangu ni Shilingi elfu tano kwa mwezi. Shilingi elfu tano katika nchi masikini. Masikini anayepata shilingi 200 kwa mwezi itamchukuwa miaka 25 kufikia kiwango cha mshahara wangu kwa mwezi. ndiyo nakubaliana na nyinyi kwamba tunalipana (Viongozi) mishahara mikubwa mno, na nitahakikisha mishahara hii tunayolipana inarekebishwa."

Maneno haya aliyatamka mwaka 1966. Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walioandamana hadi Ikulu kupinga kwenda JKT na pia kulalamikia mishahara minono ya viongozi wa serikali.

Nikisoma hiyo quotation, inaonekana Nyerere alikuwa anahoji watawala kulipwa mishahara mikubwa.

Hakuona kama ni sahihi yeye kulipwa Sh 5000 kwa mwezi katika nchi maskini kama Tanzania.

Hiyo ndiyo iliyomfanya akakubaliana na hao wanafunzi kuwa watawala walikuwa wanalipana mishahara mikubwa na kuhaidi kuwa atahakikisha mishahara hiyo waliyokuwa wanalipana inarekebishwa.

Suala kubwa hapo Ritz ni je, hiyo mishahara kweli ilirekebishwa wakati wa utawala wake au hata baada ya utawala wake?
 
Last edited by a moderator:
Kuna mtu yeyote mwenye uhakika kama kweli mishahara ilirekebishwa. Mshahara wake uliwa kiasl gani baada ya marekebisho? Na je kwa sasa Rais analipwa kiasi gani?

Inadawa kuwa

...Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' ...... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'

Japokuwa

Say what...? Hizo habari za mshahara wa rais nimekuwa nikizitafuta kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila mafanikio yoyote.

Wewe umejuaje mshahara wa raisi Mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 27,000? Enzi hizo mishahara ya viongozi ilikuwa ikiwekwa wazi ama?

Mkapa mshahara wake wakati akiwa rais unaujua? Kikwete je?

Majibu

Mwaka 1992 nilisoma kwenye gazeti la Mfanyakazi...kama unalikumbuka
na walisema 'mshahara wa Rais wakati huo ni 27,000/- na bado nakumbuka....hilo...mishahara ya Marais wengine sikupata data lakini unaweza fanya calculation kwa kuanzia kima cha chini by the time Nyerere anatoka mshahara wa Rais ulikuwa mara 12 ya kima cha chini now nasikia ni mara 58 ya kima cha chini

Bado maswali

Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?

Majibu

Source ya hiyo niliiona kwenye article ya Issa Shivji sikumbuki gazeti...

Na hii labda itamsaidia Nyani Ngabu kwenye suala lake na mshahara wa rais

Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,

Mwezi wa saba mwaka huu 2013 kuliibuka mgogoro idara ya uratibu na maslahi ya rais baadhi wakitaka mshahara wa rais na masurufu yake upandishwe hadi milioni 60,
 
Last edited by a moderator:
Nikisoma hiyo quotation, inaonekana Nyerere alikuwa anahoji watawala kulipwa mishahara mikubwa.

Hakuona kama ni sahihi yeye kulipwa Sh 5000 kwa mwezi katika nchi maskini kama Tanzania.

Hiyo ndiyo iliyomfanya akakubaliana na hao wanafunzi kuwa watawala walikuwa wanalipana mishahara mikubwa na kuhaidi kuwa atahakikisha mishahara hiyo waliyokuwa wanalipana inarekebishwa.

Suala kubwa hapo Ritz ni je, hiyo mishahara kweli ilirekebishwa wakati wa utawala wake au hata baada ya utawala wake?
Mkuu EMT.

Wanafunzi waliandamana mpaka Ikulu kupinga mishahara ya viongozi, Nyerere mwenyewe amekiri msome vizuri kuhusu kupunguza mishahara kwa kweli sifahamu bado ni siri, tofauti na mishahara ya wabunge inajulikana na inazidi kupanda kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz
Ni wazi Nyerere hakufurahishwa na hasa ukitilia maanani hakujipangia mwenyewe huo mshahara; Nyerere aliwatumikia wananchi hakutaka wananchi wamtumikie yeye; nadhani swali hilohilo ungewauliza wanasiasa wetu wa siku hizi wanaolazimisha kujipangia mshahara wa mamilioni wakati mtanzania wa kawaida anaishi katika maisha yaliyo duni; katika upande huu wa dunia ninaoshi pamoja na kuwa na kuwa ni taifa la kibepari watu hawaingii kwenye siasa kutafuta kujitarisha wanaingia kuwatumikia wananchi. Nyerere amefariki kama mtu wa kawaida hakuacha mali za kujilimbikizia nadhani mpaka hapo majibu unayo!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu EMT.

Wanafunzi waliandamana mpaka Ikulu kupinga mishahara ya viongozi, Nyerere mwenyewe amekiri msome vizuri kuhusu kupunguza mishahara kwa kweli sifahamu bado ni siri, tofauti na mishahara ya wabunge inajulikana na inazidi kupanda kila siku.

Mkuu Ritz
Ni wazi Nyerere alikubaliana na demokrasia ya kuhoji hivi leo wanafunzi wakitaka kuandamana kupinga hiyo mshahara hata Manzese watafika?
 
Last edited by a moderator:
Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,

Mshahara wa rais ni shilingi ngapi? Na hizi habari wewe umezitoa wapi?
EMT bado maswali yapo aisee maana ukiuliza source ya wapi watu wanazitoa hizo habari hupati jibu la uhakika.
 
Last edited by a moderator:
Mimi naona hii mada watu mmeipindisha pindisha kwa sababu ya jazba zisizo na ulazima.

Mada inauliza kama mishahara mikubwa ya viongozi wakati wa awamu ya kwanza ni sahihi.

Jibu lake ni kwamba SI SAHIHI. Ushahidi wa jibu hilo ni kauli ya Mwalimu ya kupinga mishahara hiyo na pia kitendo cha wasomi kuandamana kuipinga.

Hayo mengine nje ya hapo ni para-agenda...
 
wewe mbona mtoto wa kwanza wa Josephine.
wakati Mw. Nyerere analipwa kiasi hicho cha mshahara, mzee wako alikuwa anapokea kiasi gani na alikuwa analitumikiaje taifa/ktk secta ipi?
 
tuanzie hapa mshahara ya mbunge na marupurupu kwa mwezi ni million 11 kwa sasa, mbunge ambaye ni waziri kuna ongezeko lake la mshahara kwa kuwa ni waziri..hiyo ni added advantage.....then kwa tetesi zangu nilizopata toka kwa watu wa serikalini mpaka sasa mshahara wa raisi uko juu ya 20mil......
 
Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?
 
Mbaya zaidi huu mshahara wa Rais haukatwi kodi kama mishahara ya sisi walalahoi!
 
.............Asante Ritz kwa kutukumbusha kwamba CCM na serikali yake walianza dhuruma kwa wananchi tokea zamani.
 
Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?
Oh boy!! Kwani mshahara wa rais ni kiasi gani?
 
Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?

Mzee, kwani mshahara wa Kikwete wewe unaujua? Kama unaujua, umeujuaje? Kuna sehemu umeandikwa?
 
Mbaya zaidi huu mshahara wa Rais haukatwi kodi kama mishahara ya sisi walalahoi!

Mshahara wa rais ni shilingi ngapi kwani? Wapi mnazipata hizo habari za mshahara wake? Maana inainekana kama vile watu mnaujua ilhali sisi wengine tumekuwa tukiuulizia tokea 2007 na hata Zitto naye mapema mwaka huu (kama sijakosea) alisema haujui.
 
Tafuta tu hansard za bunge la bajeti
kwenye bajeti za matumizi ya Ikulu
kila mwaka wanaandika mishahara ya watumishi wote serikalini
including Rais, ukisikia kipengele cha matumizi ya kawaida ni pamoja na mishahara
 
Hmmm...sasa mbona hata Zitto alisema haujui mshahara wa rais?

Na ile thread yangu iko tokea 2007 kule kwenye jukwaa la Intelligence na hakuna aliyewahi kutoa jibu la uhakika.

Leo hii wewe unaibuka na kujua wapi habari za mshahara wa rais zilipo.

Things that make you go hmmm.....
 
Back
Top Bottom