iPad ya Apple
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 322
- 126
Wanaukumbi.Rais wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere "MSHAHARA wangu ni Shilingi elfu tano kwa mwezi. Shilingi elfu tano katika nchi masikini. Masikini anayepata shilingi 200 kwa mwezi itamchukuwa miaka 25 kufikia kiwango cha mshahara wangu kwa mwezi. ndiyo nakubaliana na nyinyi kwamba tunalipana (Viongozi) mishahara mikubwa mno, na nitahakikisha mishahara hii tunayolipana inarekebishwa." Maneno haya aliyatamka mwaka 1966.
@Ritz , kati ya habari yako na ya Mchambuzi ipi inaweza kuchambuliwa kwa uhalisiaMkuu Ritz,"Tulipokuwa tukitawaliwa na wakoloni tuligawanywa katika makundi matatu. Wazungu walikuwa juu, wahindi walikuwa katikati na waafrika walikuwa chini, kwa hali zao za elimu, mali na vyeo. Yawezekana wachache wa kundi Fulani la chini walipata bahati ya kuwa miongoni mwa kundi la juu, lakini kwa ujumla, hivyo ndivyo tulivyokuwa.....
Nimewataja mawaziri kama mfano tu. Lakini maneno haya yanawahusu waafrika wote wenye hali nzuri. Leo Permanent Secretary Mwafrika mshahara wake ni Shs. 4,000/- kwa mwezi. Hatujali permanent secretary kupata mshahara mkubwa kuliko waziri wake. Sababu ni kwamba hatutaki mawaziri wetu walinganishe mishahara yao na Ma – Permanent secretary wao, na kusema ni midogo. Tunataka mawaziri wetu walinganishe mishahara yao nay a wale vibarua wanaopata Shs.71/50, na watambue kuwa ni mikubwa. Hatutaki Waziri wetu awe na tama ya kupunguza tofauti ya pengo kati ya mshahara wake wa Shs. 3,000/- kwa mwezi na mshahara wa permanent secretary wake wa Shs.4,000/- kwa mwezi. Tunataka waziri wetu awe na tamaa ya kupunguza tofauti kati ya mshahara wake wa Shs. 3,000/- kwa mwezi na ule wa kibarua wa Shs 71/50 kwa mwezi. Kadhalika mshahara wa permanent secretary mzungu ni Shs.4,800/- au zaidi. Hatutaki permanent secretary mwafrika aseme kuwa huu ni ubaguzi, na adai yeye pia apate mshahara huo. Tunamtaka afikirie njia za kusaidia kupunguza tofauti iliyopo sasa kati ya mshahara wake wa Shs. 4,000/- kila mwezi na ule wa kibarua wa Shs. 71/50 kwa mwezi. Tunataka kila mwafrika ambaye sasa hivi hali yake ni nzuri ailinganishe hali yake na wale walio wengi ambao hali yao ni mbaya."
Kwa mantiki hiyo pia inawezekana hawa viongozi wa sasa hivi wanaolipana mishahara mikubwa wameiga huu utaratibu kutoka miaka hiyo viongozi walivyokuwa wanalipana mishahara.Kwa mantiki yako mkuu kama mnahalisha kulipana mishahara mikubwa kwa nini mnatuibia???
Rushwa za ajabu hadi kujengewa ma paradise Bilira Kempisk!!
Hamuoni aibu???
Nilijua utatia team una kiherehere dah ngoja ninyamaze nisije nikapigwa ban kwasababu ya huu utumbo ulioandika hapo juu
Mkuu Nguruvi3.
Sio sahihi na ndio maana alikuwa muwazi kupita kiasi na kusema kuwa watarekebisha maana ni mikubwa huku nchi ni maskini!
Huyu Babu yetu alikuwa muwazi na mwenye uzalendo uliotukuka tofauti na marais waliomfuata akiwemo Babaako nawewe ka-rais msaidizi na tajiri kuliko hata mzee Mengi!
Tunajua janja yako kwanini umeleta uzi huu; ni wazi unataka kuhalalisha mishahara mnazolipwa za kufuru kwamba hata enzi za Nyerere haya pia yalikua yanatendeka! Kwamba sio ajabu na ninyi mkifanya!
Inaonyesha dhahiri jinsi mlivyokosa vision lakini bado kitambo kidogo tu mtavuna mlichokipanda! Mtatuambia ni kwanini mmeifanya nchi yetu Mama-Tanzania shamba la Bibi yenu! Poor you..
Hizo ni fikra zako wapi nimekuambia kuwa natetea mishahara wanayolipana viongozi sasa hivi.
Mimi sina uhusiano wowote na Rais Kikwete, unachofanya ni makosa Name Calling.
Huu ni mjadala huru.
Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,
Mwezi wa saba mwaka huu 2013 kuliibuka mgogoro idara ya uratibu na maslahi ya rais baadhi wakitaka mshahara wa rais na masurufu yake upandishwe hadi milioni 60,
Mwaka 1966 uchumi wa nchi ulikuwa kwenye vipimo vya wastani wa nchi inayokua kistaarabu, na leo mwaka 2013 uchumi wa nchi upo kwenye kasi ya mdororo usioridhisha!
Tafteni tofauti ni asilimia ngapi?
Mwalimu Nyerere ni mmoja wa viongozi wachache duniani
waliokufa MASIKINI kabisa, hakuwa na hisa kwenye kampuni yoyote ya ndani au nje ya nchi, hakuwa na biashara yoyote zaidi ya utumishi, hakuwa na hata nyumba ya sifa zaidi ya kulazimishwa kujengewa, na zaidi Mwaka 1966 mshahara wake ALIUPUNGUZA kutoka shilingi 5,000/= hadi 3,000/= pesa nyingine alisema iende kwa Walimu na Madaktari,
Leo tunamjadili kwakumlinganisha na wafanyabiasha waliopo ikulu? Wauza madawa ya kulevya waliopo ikulu? Mafisadi waliopo ikulu?
Kuokoteza visababu vya kipuuzi kwaajili ya kuziba udhaifu na ufedhuri wenu havitawaokoa!
Hapo kuna makosa ya kiuandishi ama ni nini??!!!! Maana 5000 kwa 200 inapatikana ndani ya miezi 25 ambayo ni miaka 2 na mwezi mmoja na sio miaka 25. Mkuu Ritz, au Mwl alisema 50,000??