Nani kakuambia tunashindanisha? Kila ufisadi na zama zake.Kwani mapungufu ya Nyerere yanamfanya JK kuwa Kiongozi Imara
Mantiki ni hii"Hatushindanishi Ubovu" nyerere pamoja na mapungufu yake kama binadamu hakuna kiongozi wa Tanzania anayeweza kulinganishwa naye labda kwa Mbali Sokoine,ila siwezi kumuweka sababu akuwai kuwa Rais
Rais wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere "MSHAHARA wangu ni Shilingi elfu tano kwa mwezi. Shilingi elfu tano katika nchi masikini. Masikini anayepata shilingi 200 kwa mwezi itamchukuwa miaka 25 kufikia kiwango cha mshahara wangu kwa mwezi. ndiyo nakubaliana na nyinyi kwamba tunalipana (Viongozi) mishahara mikubwa mno, na nitahakikisha mishahara hii tunayolipana inarekebishwa."
Maneno haya aliyatamka mwaka 1966. Dar es Salaam wakati akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam walioandamana hadi Ikulu kupinga kwenda JKT na pia kulalamikia mishahara minono ya viongozi wa serikali.
Kuna mtu yeyote mwenye uhakika kama kweli mishahara ilirekebishwa. Mshahara wake uliwa kiasl gani baada ya marekebisho? Na je kwa sasa Rais analipwa kiasi gani?
...Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' ...... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'
Say what...? Hizo habari za mshahara wa rais nimekuwa nikizitafuta kwa zaidi ya miaka 6 sasa bila mafanikio yoyote.
Wewe umejuaje mshahara wa raisi Mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 27,000? Enzi hizo mishahara ya viongozi ilikuwa ikiwekwa wazi ama?
Mkapa mshahara wake wakati akiwa rais unaujua? Kikwete je?
Mwaka 1992 nilisoma kwenye gazeti la Mfanyakazi...kama unalikumbuka
na walisema 'mshahara wa Rais wakati huo ni 27,000/- na bado nakumbuka....hilo...mishahara ya Marais wengine sikupata data lakini unaweza fanya calculation kwa kuanzia kima cha chini by the time Nyerere anatoka mshahara wa Rais ulikuwa mara 12 ya kima cha chini now nasikia ni mara 58 ya kima cha chini
Je, kwa sasa umesikia huo mshahara ni mara 58 zaidi ya ule wa kima cha chini toka kwa nani/wapi?
Source ya hiyo niliiona kwenye article ya Issa Shivji sikumbuki gazeti...
Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,
Mwezi wa saba mwaka huu 2013 kuliibuka mgogoro idara ya uratibu na maslahi ya rais baadhi wakitaka mshahara wa rais na masurufu yake upandishwe hadi milioni 60,
Mkuu EMT.Nikisoma hiyo quotation, inaonekana Nyerere alikuwa anahoji watawala kulipwa mishahara mikubwa.
Hakuona kama ni sahihi yeye kulipwa Sh 5000 kwa mwezi katika nchi maskini kama Tanzania.
Hiyo ndiyo iliyomfanya akakubaliana na hao wanafunzi kuwa watawala walikuwa wanalipana mishahara mikubwa na kuhaidi kuwa atahakikisha mishahara hiyo waliyokuwa wanalipana inarekebishwa.
Suala kubwa hapo Ritz ni je, hiyo mishahara kweli ilirekebishwa wakati wa utawala wake au hata baada ya utawala wake?
Mkuu EMT.
Wanafunzi waliandamana mpaka Ikulu kupinga mishahara ya viongozi, Nyerere mwenyewe amekiri msome vizuri kuhusu kupunguza mishahara kwa kweli sifahamu bado ni siri, tofauti na mishahara ya wabunge inajulikana na inazidi kupanda kila siku.
Leo rais Kikwete analipwa mshahara na masurufu yake milioni 47.8, wakati kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi wa umma ni 180,000,
wakati Mw. Nyerere analipwa kiasi hicho cha mshahara, mzee wako alikuwa anapokea kiasi gani na alikuwa analitumikiaje taifa/ktk secta ipi?wewe mbona mtoto wa kwanza wa Josephine.
Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?
Oh boy!! Kwani mshahara wa rais ni kiasi gani?Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?
Oh boy!! hoja zingine jamani basi tena. Watu wameshajibu vya kutosha kama mtu anaelewa atakuwa ameelewa. Jiulize: Anayepata kima cha chini leo hii itamchukua muda wa miaka mingapi kufikia mshahara wa Kikwete? Au namna nyingine jiulize; tofauti gani kati ya mshahara wa kima cha chini na ule wa Rais?
Mbaya zaidi huu mshahara wa Rais haukatwi kodi kama mishahara ya sisi walalahoi!
Mshahara wa rais ni shilingi ngapi kwani? Wapi mnazipata hizo habari za mshahara wake? Maana inainekana kama vile watu mnaujua ilhali sisi wengine tumekuwa tukiuulizia tokea 2007 na hata Zitto naye mapema mwaka huu (kama sijakosea) alisema haujui.
Tafuta tu hansard za bunge la bajeti
kwenye bajeti za matumizi ya Ikulu
kila mwaka wanaandika mishahara ya watumishi wote serikalini
including Rais, ukisikia kipengele cha matumizi ya kawaida ni pamoja na mishahara