Mishahara minono kwa kwa wafanyakazi wa NIDA

Habari wakuu,

Natumaini wote ni wazima wa afya.

Kama mnakumbuka, wiki mbili au tatu zilizopita niliwahi kuomba msaada hapa kuhusu maswali ya usaili wa nafasi ya Registration Officer II upande wa NIDA. Nawashukuru wote mliochangia. Kwa neema ya Mungu, mdogo wangu ambaye nilikuwa namtafutia hayo maswali amefaulu na amepata nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna changamoto kidogo. Tayari alikuwa ameanza kazi kwenye shirika binafsi ambapo analipwa TSh 2.5 milioni take-home kwa mwezi, ingawa ana mkataba wa miaka minne.

Sasa kabla sijampa ushauri wa kufanya uamuzi, ningependa kupata maoni kutoka kwa wenye uzoefu au wanaofahamu.

Je, Registration Officer II wa NIDA anayekuwa ameajiriwa kwa mara ya kwanza analipwa kiasi gani? Pia, mbali na mshahara, kuna faida gani za kufanya kazi NIDA ambazo zinaweza kufanya iwe na busara kuacha kazi ya private sector na kuhamia huko?

Nitashukuru sana kwa mchango wenu, hasa kutoka kwa wenye uzoefu au taarifa sahihi.

Asanteni sana.

NB: Juzi nimeona wametoa gawio kubwa sana serikalini la 60+ Billion (my take -inaonesha wako vizuri sana kwenye revenue hawa jamaa).

Seran Wisle Mad Max
Kwani kwenye tangazo la ajira scale yao ilikuwaje ?
 
Watu waliacha kazi private wakaenda serikalini ambapo net salary haifiki nusu ya take home yao kule private.

Wengine waliacha kwenda especially mtu anaona kazi yake ngumu kuwa replaced au iliisha ni rahisi kupata nyingine kutokana na ana ujuzi, elimu na uzoefu gani.
 
NIDA ni taasisi ya serikali sio mamlaka ya udhibiti , Mamlaka ya udhibiti ndipo kuna mishahara minono Hiyo ni kutokana na sheria za mashikirika ya Umma. Ukienda mamlaka ya udhibiti kama EWURA , TCRA , TCAA, LATRA , TASAC kulipwa hata mil 4 ni kawaida . Pesa za chini zipo ila kulipwa parefu asahau .

Lazima ujue shirika ni mamlaka ya udhibiti au taasisi ya kawaida , hata pale TPA hawana maajabu kweny mishahara kwa vile sio mamlaka ya udhibiti ila pesa wanapiga za chini chini , wakitaka kupandisha mishahara japo fungu lipo ila wanapigwa rungu la sheria za viwango vya mishahara ya Mamlaka za udhibiti na taasisi .​
 
Habari wakuu,

Natumaini wote ni wazima wa afya.

Kama mnakumbuka, wiki mbili au tatu zilizopita niliwahi kuomba msaada hapa kuhusu maswali ya usaili wa nafasi ya Registration Officer II upande wa NIDA. Nawashukuru wote mliochangia. Kwa neema ya Mungu, mdogo wangu ambaye nilikuwa namtafutia hayo maswali amefaulu na amepata nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna changamoto kidogo. Tayari alikuwa ameanza kazi kwenye shirika binafsi ambapo analipwa TSh 2.5 milioni take-home kwa mwezi, ingawa ana mkataba wa miaka minne.

Sasa kabla sijampa ushauri wa kufanya uamuzi, ningependa kupata maoni kutoka kwa wenye uzoefu au wanaofahamu.

Je, Registration Officer II wa NIDA anayekuwa ameajiriwa kwa mara ya kwanza analipwa kiasi gani? Pia, mbali na mshahara, kuna faida gani za kufanya kazi NIDA ambazo zinaweza kufanya iwe na busara kuacha kazi ya private sector na kuhamia huko?

Nitashukuru sana kwa mchango wenu, hasa kutoka kwa wenye uzoefu au taarifa sahihi.

Asanteni sana.

NB: Juzi nimeona wametoa gawio kubwa sana serikalini la 60+ Billion (my take -inaonesha wako vizuri sana kwenye revenue hawa jamaa).

Seran Wisle Mad Max
Very interesting! Yaani aache mshahara wa 2.5 (take home) private sector na mkataba wako wa miaka 4! Eti aende kuajiriwa serikalini kwa mshahara wa chini milioni 1! Hapo lazima uchawi utahusika.

Miaka minne aki save hata milioni 1 tu kila mwezi si anakuwa na mtaji wa kutosha kabisa kujiajiri iwapo hataongezewa mkataba!
 
Ndio maana nimelete huku ili nijue wanalipa kiasi gani?
 
Hawawezi kumlipa hata nusu ya huo mshahara kwa mtu anayeanza kazi. Kama ni mpambanaji ni bora akajikusanyia zake mtaji wa kumuwezesha kupambana mtaani. Ila kama ni muoga wa maisha na hana uwezo wa kuhifadhi akiba, akubali kujitia kitanzi serikalini.
 
NIDA ni taasisi ya serikali sio mamlaka ya udhibiti , Mamlaka ya udhibiti ndipo kuna mishahara minono Hiyo ni kutokana na sheria za mashikirika ya Umma. Ukienda mamlaka ya udhibiti kama EWURA , TCRA , TCAA, LATRA , TASAC kulipwa hata mil 4 ni kawaida . Pesa za chini zipo ila kulipwa parefu asahau .

Lazima ujue shirika ni mamlaka ya udhibiti au taasisi ya kawaida , hata pale TPA hawana maajabu kweny mishahara kwa vile sio mamlaka ya udhibiti ila pesa wanapiga za chini chini , wakitaka kupandisha mishahara japo fungu lipo ila wanapigwa rungu la sheria za viwango vya mishahara ya Mamlaka za udhibiti na taasisi .​
Hizo mamlaka za udhibiti sio taasisi za serikali? Umasema TPA hakuna maajabu wakati wana njia za kukusanya mapato? Kwani NSSF na PSSF ni mamlaka za udhibiti mbona mishahara yao ni mizuri? Mimi nimachofahamu taasisi ikiwa na njia za mapato inakuwa rahisi kulipa mishahara mizuri kwa sababu ina chanzo cha mapato
 
Habari wakuu,

Natumaini wote ni wazima wa afya.

Kama mnakumbuka, wiki mbili au tatu zilizopita niliwahi kuomba msaada hapa kuhusu maswali ya usaili wa nafasi ya Registration Officer II upande wa NIDA. Nawashukuru wote mliochangia. Kwa neema ya Mungu, mdogo wangu ambaye nilikuwa namtafutia hayo maswali amefaulu na amepata nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna changamoto kidogo. Tayari alikuwa ameanza kazi kwenye shirika binafsi ambapo analipwa TSh 2.5 milioni take-home kwa mwezi, ingawa ana mkataba wa miaka minne.

Sasa kabla sijampa ushauri wa kufanya uamuzi, ningependa kupata maoni kutoka kwa wenye uzoefu au wanaofahamu.

Je, Registration Officer II wa NIDA anayekuwa ameajiriwa kwa mara ya kwanza analipwa kiasi gani? Pia, mbali na mshahara, kuna faida gani za kufanya kazi NIDA ambazo zinaweza kufanya iwe na busara kuacha kazi ya private sector na kuhamia huko?

Nitashukuru sana kwa mchango wenu, hasa kutoka kwa wenye uzoefu au taarifa sahihi.

Asanteni sana.

NB: Juzi nimeona wametoa gawio kubwa sana serikalini la 60+ Billion (my take -inaonesha wako vizuri sana kwenye revenue hawa jamaa).

Seran Wisle Mad Max
Kama ameshapata hiyo ajira kwanini hawajamwambia kiasi cha mshahara atakaolipwa?
 
Hizo mamlaka za udhibiti sio taasisi za serikali? Umasema TPA hakuna maajabu wakati wana njia za kukusanya mapato? Kwani NSSF na PSSF ni mamlaka za udhibiti mbona mishahara yao ni mizuri? Mimi nimachofahamu taasisi ikiwa na njia za mapato inakuwa rahisi kulipa mishahara mizuri kwa sababu ina chanzo cha mapato
😅😅😅Kijana uliza uambiwe kwanza ,TPA inakusanya zaidi ya bil 204 ,huku TASAC inakusanya bil 20 ,ila TPA iko chini ya TASAC ..TASAC wana mishahara kufuru hauwezi kufananisha hata nusu ya TPA .

Mamlaka za uthibiti ni taasisi zenye mamlaka ya juu ,zinasimamka sheria ..Basi zipo Mamlaka za uthibiti(Top kwa mishahara ) kuna Taasisi ( kawaida ) ,halafu kuna agency kama GPSA .

Kama unabisha kaulize ,makusanyo ya mapato hayareflect ubora wa Taasisi kwa sababu kila taasisi ina bajeti yake ya uendeshaji ,wana ukomo wa bajeti ...Pesa za ndani zinatumika kupitia expenditure account ,na kukusanya ni account nyingine...😅😅

Serikali inapopanga mapitio ya mishahara ,hakuna taassi ndogo inaweza kuizidi mishahara mamlaka ya uthibiti .Hii ni kutokana na majukumu ,mamlaka za uthibiti zinawazidi mpaka waliopo wizarani ,uliza ukaambiwe..

kingine usichojua Mamlaka za uthibiti zina wafanyakazi wachache ,tena wale professional ila mamlaka nyingine ni kurundika tu ,diploma wengi ... Tambua ...
 
Back
Top Bottom