Mishahara minono kwa kwa wafanyakazi wa NIDA

Mishahara minono kwa kwa wafanyakazi wa NIDA

Habari wakuu,

Natumaini wote ni wazima wa afya.

Kama mnakumbuka, wiki mbili au tatu zilizopita niliwahi kuomba msaada hapa kuhusu maswali ya usaili wa nafasi ya Registration Officer II upande wa NIDA. Nawashukuru wote mliochangia. Kwa neema ya Mungu, mdogo wangu ambaye nilikuwa namtafutia hayo maswali amefaulu na amepata nafasi hiyo.

Hata hivyo, kuna changamoto kidogo. Tayari alikuwa ameanza kazi kwenye shirika binafsi ambapo analipwa TSh 2.5 milioni take-home kwa mwezi, ingawa ana mkataba wa miaka minne.

Sasa kabla sijampa ushauri wa kufanya uamuzi, ningependa kupata maoni kutoka kwa wenye uzoefu au wanaofahamu.

Je, Registration Officer II wa NIDA anayekuwa ameajiriwa kwa mara ya kwanza analipwa kiasi gani? Pia, mbali na mshahara, kuna faida gani za kufanya kazi NIDA ambazo zinaweza kufanya iwe na busara kuacha kazi ya private sector na kuhamia huko?

Nitashukuru sana kwa mchango wenu, hasa kutoka kwa wenye uzoefu au taarifa sahihi.

Asanteni sana.

NB: Juzi nimeona wametoa gawio kubwa sana serikalini la 60+ Billion (my take -inaonesha wako vizuri sana kwenye revenue hawa jamaa).

Seran Wisle Mad Max
Security of tenure kwa ajira za private ni ndogo kufananisha na serikalini. Na ni bora akachukua kazi ya kudumu kuliko kazi ambayo inakikomo.
 
😅😅😅Kijana uliza uambiwe kwanza ,TPA inakusanya zaidi ya bil 204 ,huku TASAC inakusanya bil 20 ,ila TPA iko chini ya TASAC ..TASAC wana mishahara kufuru hauwezi kufananisha hata nusu ya TPA .

Mamlaka za uthibiti ni taasisi zenye mamlaka ya juu ,zinasimamka sheria ..Basi zipo Mamlaka za uthibiti(Top kwa mishahara ) kuna Taasisi ( kawaida ) ,halafu kuna agency kama GPSA .

Kama unabisha kaulize ,makusanyo ya mapato hayareflect ubora wa Taasisi kwa sababu kila taasisi ina bajeti yake ya uendeshaji ,wana ukomo wa bajeti ...Pesa za ndani zinatumika kupitia expenditure account ,na kukusanya ni account nyingine...😅😅

Serikali inapopanga mapitio ya mishahara ,hakuna taassi ndogo inaweza kuizidi mishahara mamlaka ya uthibiti .Hii ni kutokana na majukumu ,mamlaka za uthibiti zinawazidi mpaka waliopo wizarani ,uliza ukaambiwe..

kingine usichojua Mamlaka za uthibiti zina wafanyakazi wachache ,tena wale professional ila mamlaka nyingine ni kurundika tu ,diploma wengi ... Tambua ...
Kijana mm nina wadau hizo taasisi zote ulizotaja na mishahara yao naijua ila kwa huko NIDA ndo sijajua maana nimetafuta sijapata.

Napouliza hapa ni kwamba nahitaji kumsaidia dogo, nina both experience ya kufanya kazi serikalini na private for 10 years now. Ninachotaka hapa ni kumshauri dogo either aendelee na private japo kwa mikataba au aingie huko serikalini afanye kwa muda then atoke aende private au ajiajiri ndo sababu ya kuuliza.
 
NIDA ni taasisi ya serikali sio mamlaka ya udhibiti , Mamlaka ya udhibiti ndipo kuna mishahara minono Hiyo ni kutokana na sheria za mashikirika ya Umma. Ukienda mamlaka ya udhibiti kama EWURA , TCRA , TCAA, LATRA , TASAC kulipwa hata mil 4 ni kawaida . Pesa za chini zipo ila kulipwa parefu asahau .

Lazima ujue shirika ni mamlaka ya udhibiti au taasisi ya kawaida , hata pale TPA hawana maajabu kweny mishahara kwa vile sio mamlaka ya udhibiti ila pesa wanapiga za chini chini , wakitaka kupandisha mishahara japo fungu lipo ila wanapigwa rungu la sheria za viwango vya mishahara ya Mamlaka za udhibiti na taasisi .​
TPA= Tanzania Ports Authority. Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.
 
Kijana mm nina wadau hizo taasisi zote ulizotaja na mishahara yao naijua ila kwa huko NIDA ndo sijajua maana nimetafuta sijapata.

Napouliza hapa ni kwamba nahitaji kumsaidia dogo, nina both experience ya kufanya kazi serikalini na private for 10 years now. Ninachotaka hapa ni kumshauri dogo either aendelee na private japo kwa mikataba au aingie huko serikalini afanye kwa muda then atoke aende private au ajiajiri ndo sababu ya kuuliza.
Nimekuambia NIDA ni taasisi ya kawaida ,so atarajie mishahara ya kawaida ,sio mamlaka ya udhibiti.
 
MTIHANI WA HISABATI WA KUJIPIMA
10/07/2026

Bwana jumbe ameajiriwa katika shirika binafsi kwa mkataba wa miaka minne. Kama mshahara wa Bwana Jumbe kwa mwezi ni TZS 2500,000.
(i) Je akisave TZS 2500,000 kila mwezi kwa mwaka atakua na TZS ngapi?
(ii) Je akisave TZS 2500,000 kila mwezi kwa miaka minne atakua na TZS ngapi?
(iii) Kama jumbe ana mpango wa kustaafu akiwa amekusanya TZS 50,000,000 atastafuu baada ya miaka mingapi tangu aanze kazi? Assume ataongezewa mkataba.
 
Huyu bwana Jumbe hana matumizi ya kila siku ndani ya miaka 4?
 
Kijana mm nina wadau hizo taasisi zote ulizotaja na mishahara yao naijua ila kwa huko NIDA ndo sijajua maana nimetafuta sijapata.

Napouliza hapa ni kwamba nahitaji kumsaidia dogo, nina both experience ya kufanya kazi serikalini na private for 10 years now. Ninachotaka hapa ni kumshauri dogo either aendelee na private japo kwa mikataba au aingie huko serikalini afanye kwa muda then atoke aende private au ajiajiri ndo sababu ya kuuliza.
Si useme tu ni wewe mkuu?
Anyway NIDA naona kama njaa sana
 
Back
Top Bottom