Mishahara ni hongo ya kufanya watu waamini tofauti na na wanavyo amini

ndo unavyo jidanganya eti yuko so happy, hahahaa utumwa huo, je ana maamuzi binafisi? anaweza amua leo asiende kazini? acha kujipa moyo
Wewe ukiwa na bishara zako kwa hiyo utakuwa unaamua tu leo siendi kazini si utafilisika?

Badilisheni dhana zenu kichwani hizo. Ukiwa umeajiriwa au umejiajiri huwezi kuwa mvivu. Na kama eti unajiajiri sababu uwe na maamuzi ya kukaa tu nyumbani bila kwenda kazini naomba nisiendelee kubishana wala kueleweshana na wewe. Hatufanani.
 
Niko upande wa mleta mada hii mada ingekuja jukwaa la ajira hata mimi ningemshambulia. Maadamu jukwaa ni la ujasiriamali mada ni sahihi na huyo anayemshambulia basi limemgusa.
 
Mleta Uzi hongera kwa kuleta point adimu
Watu wengi waloajiriwa wanatabia ya kuridhika mapema sana na mwisho wa siku huishia kuishi maisha ya middle class.Hukaa wakiamini hakuna maisha nje ajira
Unapowaletea mada nzito kiasi hiki ni pigo kwa....
 
Mimi niko tayari kutelekeza ndoto zangu na kutimiza za mwajiri wangu katika nafasi ya uanasiasa.

Mishahara ya politician minono na madeal mengi kujiajiri kukasome
 
Mkuu hili jukwaa sio la wafanya kazi sasa unataka tuongee nini?.Jukwaa lina husu nini?

Kuna jukwaa la ajira kule tunazungumzia watu kuajiriwa
Kuna haja gani ya kupondea wenzio.? We toa mada kuhusu kujiajiri piga kimya ..walioajiriwa achana nao, we unafikiri walimu wote wakianzisha shule itakuaje ? usikariri maisha. B12 ana brand yake ya biashara na najua ni kubwa kuliko biashara yako ila hadi leo kaajiriwa clouds anapiga kazi, punguza maneno ya shombo, zamani ulikua na mada nzuri na nilikua nafuatilia ila siku hizi naona umeishiwa umebaki kupiga vijembe tu, kama huna cha kufanya kakae hata na kuku wako mpige story.
 
chasha uko too biase kwenye mtazamo wa kuajiriwa na kujiajiri na ukiwa na maneno hayo basi utapata taabu sana kuishi na wafanyakazi wako dunia hubadilika na mitazamo ibadilike unataka kunieleze kua uko bora kuliko walioajiriwa? Binafsi nimejiajiri lakini nakupinga mno kwenye baadhi ya mambo kimtazamo.
 
hatuwezi tukaajiriwa wote na hatuwezi tukajiajiri wote... ili ni jukwaa la uchumi na ujasiriamali..

hata waajiriwa wanahusika ili jukwaa maana wana mchango mkubwa kwenye uchumi... na kazi zao wengine zinahusiana na uchumi moja kwa moja..
 
hatuwezi tukaajiriwa wote na hatuwezi tukajiajiri wote... ili ni jukwaa la uchumi na ujasiriamali..

hata waajiriwa wanahusika ili jukwaa maana wana mchango mkubwa kwenye uchumi... na kazi zao wengine zinahusiana na uchumi moja kwa moja..
mnakuwa wabishi sana hili jukwaa lishavamiwa na watu wabishi watu wajuaji watu wa kwenye AC muda wote
 
nyie wafanya kazina maneno sana chasa mbona kaelezea kwamba humu ni swala la kujiajiri, mngeingia kipindi cha nyuma msingeongea haya shida jukwaa lisha vamiwa na watu wa ajabu ajabu sana wabishi na wafanya kazi sasa humu wanaingia kudefend ajira zao na kuambukiza wenzao. humu ni kuhamasisha watu kujiajiri
 
kwani kosa ni nini?? kuwa kwenye Ac ni dhambi??

wapo waliojiajiri na wanaokaa kwenye ac pia.. mfano max na mike na jamiiforums yao.. wamejiajiri ila wanashinda kwenye ac tu na computer zao...

ili jukwaa linahusiana na uchumi pia na hapo ndipo waajiriwa wanapohusika

mnakuwa wabishi sana hili jukwaa lisha vamiwa na wajinga watu wabishi watu wajuaji watu wa kwenye AC muda wote
 
acha ubishi wewe kijana shida mmevamia hili jukwaa kwa spidi na nyie mnatia uoga mnatengeneza vizazi vya waoga humu.wacha kutengeneza vizazi vya watu waoga wacha kupalilia watu waajiriwe.hao wakina B12 ni waoga tu ndo maana hawawezi acha kazi na hawawezi kuwa mfano wa kipigiwa

casha anahamasisha watu wapunguze kizazi za uoga ila hamumuelewi mmekazana na ajira acheni hizo tunatengeneza vizazi vya waoga
 
kizazi cha uoga nazani uoga wenu wa chuoni ndo mna utransfer hadi humu, jukwaa mvuto halina kwa sababu ya watu kama nyie
 
kizazi cha uoga nazani uoga wenu wa chuoni ndo mna utransfer hadi humu, jukwaa mvuto halina kwa sababu ya watu kama nyie
Tunarithishana kizazi cha watu waoga na hao ndo story wanaambia watoto wao wasome waje kuwa mameneja na wapate kazi nzuri za Benki
 
kwa mtazamo wangu wat wanakubali kuajiriwa kwa kukosa mitaji... Ndôto wanakuwa nazo tatizo pa kuanzia
 
Mkuu you are missing the point big time...., mwisho wa siku ni bottom line au ni nini? unataka biashara yako upate sifa kwamba nina biashara au faida ?, ngoja nikupe scenario tatu...

Mimi kama lecturer nianzishe Chuo au nifanye kazi kwenye vyou hata sita part time nipate salary wapi nitabreak even mapema ? (kumbuka biashara ina overheads)

Mimi kama Doctor Bingwa wa Moyo ni rahisi (peace of mind) kufungua hospital yangu (kumbuka hii management and has nothing to do with being a doctor) au niwe naitwa hospitals tofauti by contract and paid a huge salary..

Mimi kama Kocha wa mpira tuseme (Zidane) niendelee ku-coach kwa mshahara au nianzishe timu yangu na kuwa owner...

Kumbuka mdau vitu sio black or white.., na unaweza ukawa employed ila kwa uzito wako ukaweka terms unazotaka na bado ukawa shareholder ingawa sio owner....
 
mawazo ya yako ni full upotoshaji umejawa na kiwango kisicho semekana cha uoga
jebu nitajie kwenye list ya fobbers ni wafanya kazi wangapi wako kwenye ile list? au Tanzania tu nitajie wafanya kazi matajiri

acha kuzungumzia kuwa na pesa ya kubadili mboga na kununua used car na kuwa na pesa ya kwenda ufukweni

Mengi anapesa anaweza hata enda kukaa kwenye visiwa vya Hawaii mwaka mzima anakula bata hizo ndo pesa
Mohamed Entreprises hana pesa ya kubadili mlo bali anapesa ya kuweza kuleta mtikisiko

acha kuleta story za mishara ya kukuwezesha kubadili milo na kununua used car na ukijitahidi sana unajenga nyumba
 
unamaanisha waliojiajiri wote wana hela za kukaa ufukweni hawaii mwaka mzima..

na hawa nyumba zao zinazouzwa na mabank kisa mikopo biashara zimebuma now wana mafanikio kuliko waajiriwa..

hata waajiriwa wapo wanaoweza kwenda hawaii.. kina kimei, mchechu, na wengine kibao...

mnakosea sana mnavyoongelea waliojiajiri kwa kutoa mifano ya mengi na dewji.. unasahau hao wote walishawai kuajiriwa tena sana tu.. mengi kafanya sana kazi za watu...

mnasahau pia kuna walioajiajiri wengi tu ambao wana maisha mabovu kuliko walioajiriwa... na hawana hata hela za dharura..

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…