Mishahara ni hongo ya kufanya watu waamini tofauti na na wanavyo amini

Mishahara ni hongo ya kufanya watu waamini tofauti na na wanavyo amini

Utajiajiri vipi bila mtaji? Au hiyo shule na duka la nguo utavianzishia hewani? Watu wamesoma ndiyo, wanatamani kujiajiri ila tatizo ni mtaji.
Kwani mtaji maana yake ni nini? Hii ndio shida ya kuamini mtaji ni fedha! [emoji15]
 
Inaaminika kwamba mishahara watu wanayo lipwa ni hongo ya kuwafanya watelekeze Ndoto zao na waanze kutekeleza ndoto za wale wanao wapatia mishahara.

Hii inapata Nguvu kwa sababu Msomi au mtu yoyote yule yuko tiyari aajiriwe kwenye duka la kuuza nguo lakini hayuko tiyari kufungua kibanda chake cha kuuza nguo.

Msomi yuko toyari aajiriwe kwenye kama mwalimu na mwenye shule lakini hawezi anzisha yake.

Hivyo mishahara ni hongo za kufanya watu waamuni kwamba Dream zao zina makosa na Dream za wale wanao walipa ndo ziko sahihi.

Bila mishahara watu wasinge neglect Dream zao.
Mkuu ukisema inaaminika-swali ni inaaminika na nani? Kuna utafiti wowote kuhusu hili? Vinginevyo sema unaamini hapo itaeleweka. Kama ni kweli inaaminika basi toa ushahidi. Kuhusu mshahara sijaona mahali popote ambapo mshahara unasemekana ni hongo-dhana hii wewe ndo umeitoa. Mshahara ni malipo yanalipwa kwa mtu anaetoa huduma halali kwa mtu au taasisi nyingine. Kila mmoja wetu anakua na malengo yake kuhusu maisha anayotaka, kila mmoja wetu mwenyezi Mungu kamjalia uwezo wa aina fulani na mazingira ya aina fulani-kutokana na hayo huamua njia ya kumfikisha malengo yake. Wengine huamua kujiajiri na wengine huamua kuajiriwa. Wengine huajiriwa na baadae huweka misingi wakajiajiri. Wako pia wenye kujiajiri lakini baadae huamua kuajiriwa. Kila kimoja kina faida zake na hasara zake.
Ndoto ni kitu muhimu lakini uwezo na kuwa na nyenzo ni muhimu pia. Ndo maana kunawanaotaka kujiajiri lakini hushindwa kufanya hivyo, na kuna wanaotaka kuajiriwa lakini uwezo wao na nyenzo zao huwa duni wakaamua kufanya vitu binafsi vya kuingiza kipato lakini sio kwamba wanafurahia bali wanapambana na maisha kwani tonge lazima liende mdomoni.
Kujiajiri sio ndoto ya kila mtu-ni mkakati wa jinsi ya kupata kipato uwe na maisha ya aina fulani. Ukichukua wasomi kama ulivyoelezea duniani kote wengi ni waajiriwa na wanaojiajiri ni wachache na hawa hutegemea wasomi hao hao kuendesha biashara au mashirika yao. Bila kuwepo waajiriwa si serikali wala sector binafsi itapiga hatua.Unasema "Bila mishahara watu wasinge neglect Dream zao"-hapa naona ndo umejichanganya-mshahara ni malipo ya kazi bila mshahara basi kwa nini ufanye kazi. Ni sawa na kusema bila faida hakutakuwa na wanaojiajiri-kumbuka faida ni kinachobaki baada ya kulipia gharama za uzalishaji ikiwa ni pamoja na nguvu kazi-mishahara. Anaejiajiri anaendesha maisha yake kutokana na faida na naeajiriwa anaendesha ya kwake kutokana na mshahara. Tukiwa wote na nyenzo sawa na ndoto sawa basi dunia itagota.
Namalizia kusema anaefikiria anaeweza kujiajiri na mazingira yake yanaruhusu hata kama itabidi ajiongeze afanye hivyo yule mwenzangu mimi anaefikiri njia bora ni uajiriwa na mazingira yanaruhusu hata kama itabidi apambane afanye hivyo. Wale wanaokwama ajira shida, kujiajiri shida wanafanya vitu vidogo vidogo bora tonge liende mdomoni. Wanaojiajiri na kutengeneza private sector ni muhimu kwa taifa lolote kwani huweza kutoa ajira nyingi hata kushinda zile za serikali. Wanaoajiriwa na serikali upande wa sera nao hutengeneza mazingira ya watu kujiaajiri.
 
Mmeisha kuwa Brain washed kwamba Biashara lazima kika siku ukamate laki kadhaa.

Hata kama kwa siku anapata faida elfu 5 au hata elfu 3 ni yake na yeye yuko kwenye orodha ya watu walio dhubutu.

Anapiga progress na siku moja atakuwa mbali sana.

Mimi binafisi naamini sitakufaga masikini na itakuwa hivyo.

Safari ya ujasiriamali ni kweli ni ngumu na ndo maana wengi wanaishia kutembea na CV kutafuta watu wa kuwaajiri


Sawa boss heri yako wewe usiye brainwashed. “Don’t be addicted to money. Work to learn. don’t work for money. Work for knowledge.”
 
Hivi unahisi dunia nzima watu wanaweza kujiajiri na wasiwepo wakulipwa mshahara mkuu? Huwezi badili hii dhana duniani, kama wewe una biashara yako unapata hela na aliyeajiriwa anapata hela itoshe tunakutana sokoni wote kununua mahitaji. Mnawakandia sana waajiriwa asee.
Yaan leo kaongea pumba..halafu i dont know he is always against employed people...jamani hatuwez wote kujiajiri lazma kuna watu waajiriwe na wengine wajiajiri...
 
Mleta mada anahitaji kufanya rejea ya Ujasiriamali ni nini....Dhana ya Ujasiriamali imebadilika sana toka Karne ya 17 hadi ya 21.Zile Falsafa za akina Karl Max kuhusu Labour zilishabadilika pia.Kwa ufupi waajiriwa pia ni wajasiramali Kwa Definition latest!Ni watu wanaaona fursa na wakazichangamkia.Kwa nchi kama TZ hivi vibiashara vidogo vinamilkiwa na waajiriwa.Mfano hapa nilipo Waajiriwa wa umma ndiyo wamilki wa maduka.Binafsi nimeajiriwa umma,lakini Nina portfolio zaidi ya 5: Trading,agro-processing,farming, Govt securities,DSE nk.Mashamba yangu naajiri watu.Lakini mwisho wa siku napima ipi inalipa.Zama zimebadilika.Usimtishe mtu kwamba ni mwoga,Sarakasi za gharama za uendeshaji wa Biashara na mengineyo tunacheza nayo Kila siku.Mwisho huu uongo kwamba unajiamlia ulale mje muuache.Bill Gate hakuwahi kukosa kazini Kwa zaidi ya miaka 10!!Na Kwa nini ujiajiri kwa incentive ya Kutoenda kazini siku hujisikii?
Aliyejiajiri na aliyajiriwa Wote wanapata mshahara:majina ndiyo tofauti-Director's Fees au Dividents au ujira ni kitu kimoja,vyote ni matokeo ya Kupata faida.
 
Yaan leo kaongea pumba..halafu i dont know he is always against employed people...jamani hatuwez wote kujiajiri lazma kuna watu waajiriwe na wengine wajiajiri...
Wafanyakazi utawajua tu, acha kujitoa ufahamu.
Hili jukwaa lina kazi ya kujenga kizazi cha kuajiri. nyie ndo mnafurahia wachina kuja kufanya biashara ambazo sisi tunaweza kufanya. Ila hatuzifanyoa kwa sababu tusha aminishwa kwenye kuajiriwa.

Yaani na wewe ndo ile kazi ikiisha unaweza jinyonga,
 
Mmeisha kuwa Brain washed kwamba Biashara lazima kika siku ukamate laki kadhaa.

Hata kama kwa siku anapata faida elfu 5 au hata elfu 3 ni yake na yeye yuko kwenye orodha ya watu walio dhubutu.

Anapiga progress na siku moja atakuwa mbali sana.

Mimi binafisi naamini sitakufaga masikini na itakuwa hivyo.

Safari ya ujasiriamali ni kweli ni ngumu na ndo maana wengi wanaishia kutembea na CV kutafuta watu wa kuwaajiri
yani mtu ahangaike na 3000 kwa siku eti mradi tu aonekane na yeye kajiajiri wakati kuna ajira inayoweza kumlipa zaidi ya hivyo, we jamaa acha kudanganya watu na kujifanya mjuaji
 
We ndo nyumbu kweli... yani mtu ahangaike na 3000 kwa siku eti mradi tu aonekane na yeye kajiajiri wakati kuna ajira inayoweza kumlipa zaidi ya hivyo, we jamaa acha kudanganya watu na kujifanya mjuaji wakati boya tu
Anadanganya au wewe ndo unadanganya? coment yako tu inaonyesha nyie ndo wale mko radhi kutumikishwa usiku na mchana lakini hamko tiyari kuanzisha zenu
 
Tuwe wavumilivu bwana mkubwa amekumbusha jambo muhimu hata mimi ni mwajiriwa lakini nimepata kitu
 
kuajiriwa kwenyewe ni dream ya wasomi wetu, mtu mwenye mission na vision atatumia ajira kama daraja la kufikia ndoto yake na sio kubweteka.
 
Huyu Chasha Poultry Farm ndio huyo huyo anajiita MURUSI.akiona amezidiwa hoja anakuja na id nyingine inaitwa MURUSI anaanza kubishana,hii thread ya 4 nawasoma tu.
Ni upumbav huo.


Hance Mtanashati nakuomba uje kufanya upelelezi wa multple id uku
Hahahaaa ndo kiwango chako cha kiwaza kimefikia Tamati, kwenye kuwaza hapo ndo mwisho wako. endelea kupiga Ramli tu.Mimi sijifichi n niko Verfied
 
Watu wanajua ujasiriamali/kujiajiri ni mpk ufuge kuku/ng'ombe au uwe na frame ya kuuza nguo etc.

Hawajui mhasibu/mwanasheria mwenye firm yake nae ni mjasiriamali.
 
Ishu sio makombora mkuu, jiulize watu wangapi wameajiriwa lakini wana maisha mazuri kuliko wewe?

Acha kukariri na vimiradi vyenu vya kuku hivyo boss. Maisha ni kuchagua, mwingine kaajiriwa lakini yuko so happy na kazi yake na mshahara wake, anatunza familia yake anaweka akiba yake sawa tu na wewe una miradi yako lakini kila siku presha, nani afadhali sasa?

Ukiwa na choice yako usilazimishe iwe kwa kila mtu na isiwe sheria!
hahahaaaaaa asante sana maana sio wote tutakuwa wafanyabiashara, wakulima au wafugaji wengine wajigawa kwingine hayo ndo maisha
 
Back
Top Bottom