Raisi na viongozi wenine wa juu ni waajiriwa serikalini kama waajiriwa wengine, wanalipwa mishahara kwa kufuata sheria na katiba ya nchi. Haiwezekani raisi akalipwa 200,000 tena kwa mwaka akati kima cha chini ni 300,000 kwa mwezi. Hawa mabwana wanapata pesa nyingi za marupurupu katika safari, vikao na mambo kama hayo kama ilivyo kwa mtu yeyote yule serikalini kwamba anapata pesa safarini na vikaoni ila viwango vinatofautiana kutokana na cheo.
Sasa raisi analipwa mshahara shilingi ngapi kwa mwezi?
Hamna aliyetayari kuweka wazi mshahara wake Tz, raisi analipwa kati ya 300,000 hadi 2,000,000 kwa mwezi coz hivyo ndo katiba inavyotaka alipwe ila anatengeneza pesa zaidi ya hapo kwa mwezi tokana na sababu nilizosema hapo juu.
Umejuaje kama rais analipwa "kati ya 300,000 hadi 2,000,000 kwa mwezi"?
Mkuu katiba na sheria ya nchi ndivyo inavyosema hamna mtu aliye juu ya katiba, pesa anayolipwa ni fupi ila hela anayomake kwa mwezi ni ndefu. Tofautisha mshahara na pesa mtu anayotengeneza kwa mwezi, pesa anayotengeneza ni ndefu coz inajumlisha mshahara, allowances na vitu kibao yule jamaa akisafiri analipwa na unajua kasafiri mara ngapi akienda kwenye mikutano analipwa ila hizo hazijumlishwi kwa mshahara.
Mambo ya pesa fupi na hela ndefu siyataki mimi. Nataka kujua mshahara wake kwa mwezi ni shilingi ngapi? Unajua ama hujui?
Sijui.
Raisi na viongozi wenine wa juu ni waajiriwa serikalini kama waajiriwa wengine, wanalipwa mishahara kwa kufuata sheria na katiba ya nchi. Haiwezekani raisi akalipwa 200,000 tena kwa mwaka akati kima cha chini ni 300,000 kwa mwezi. Hawa mabwana wanapata pesa nyingi za marupurupu katika safari, vikao na mambo kama hayo kama ilivyo kwa mtu yeyote yule serikalini kwamba anapata pesa safarini na vikaoni ila viwango vinatofautiana kutokana na cheo.
Mkuu tofautisha kati ya $ 200, 000 na 200, 000 !
Nyani,Hii mada ina zaidi ya miaka 5 sasa na hakuna mtu anayejua mshahara wa rais ni kiasi gani!!
Nyani,
Once upon a time mshahara wa rais wa Tanzania haukuwa siri. Umeanza kufanywa siri enzi za Mkapa kwa sababu hawa walianza kuwa wezi na hawakutaka Watanzania wajue jinsi wanavyoibiwa. Lakini tutajua tu. Enzi za Mwalimu 1966 mshahara wale ulikuwa shilingi elfu sita kwa mwezi. Katika yale maandamano ya wanafunzi kupinga national service akaupunguza kwa asilimia 20.