Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Kuna haja kuwe na hoja ya Ukomo ktk Ubunge say vipindi viwili au vitatu tu!

Hebu fukiria.. mtu analipwa 84,000,000 kwa mwaka na mbunge kwa miaka 20 au 30???

Yet hawa hawa wabunge wako ktk Bodi za mashirika mbali2 ambapo a Sitting ni 500,000 hadi 1,000,000 kwa siku!

Is our society just and Fair?
 
Ingekuwa mshahara ni sawa na wa Mwalimu wangepigana vikumbo kugombea Ubunge,tena wasomi mahiri wanaacha kufundisha vyuo vikuu wanakimbilia Bungeni?

Kuna haja ya kuangalia malipo katika vyeo hivi vya kisiasa kwani wanarizika na malipo yao na kuacha kuwatetea wenzao wa fani zingine hivyo wanabaki kutafuta mbinu za kutonyang'anywa nafasi hiyo ya Ubunge.

Wananchi tuamke tupigania mslahi ya Mbunge yawiane na watendaji wengine katika nchi, hiyo ni dawa ya kuzuia watu kugombania sehemu moja.
 
Mkuu wangu Kasheshe,
Pesa ya mafuta utatumia kuhudimia wananchi wa Ileje wakati unashinda Dar Es Salaam?

Hata pesa za mafuta, hawa waheshimiwa wanakula tu.

Wanakula mishahara ya madereva wao itakuwa fedha ya mafuta kutembelea majimboni?
 
Hebu fukiria.. mtu analipwa 84,000,000 kwa mwaka na mbunge kwa miaka 20 au 30???

Yet hawa hawa wabunge wako ktk Bodi za mashirika mbali2 ambapo a Sitting ni 500,000 hadi 1,000,000 kwa siku!

Is our society just and Fair?

Mzalendo unazidi kunpandisha hasira, nikikumuka na hawa hawa wabunge wanaona watoto/wajukuu/watukuu zetu wanakaa chini shuleni, hawana waalimu. Wazazi wanajifungua katika mazingira magumu mno. Hawa, hawa, hawa Wabunge kuna siku tu nao watajua moto wa wananchi.
 
Halafu hawa hawa wanapitisha mikataba mibovu,wafanya biashara na wana tamaa ya madaraka na mali.
 
Mzalendo, nahisi adrenalins zangu zimepata hitilafu ghafla. Zimepanda na kumwagika!!

ooooh now i understand, i understand. Pesa kweli ni shetani.
 
...tatizo langu sio ni nini wanalipwa, bali wanalipwa kwa kipi walichokifanya? Kama nchi tungeweza kuamua kulipana tu mishahara mikubwa yaani wafanyakazi walipwe kiasi chochote, lakini uzalishaji wetu unaendana na kile tunachotaka kulipwa?

Tunaweza kuendelea kudai marupurupu lakini tusipojua namna ya kuongeza mapato ili tupate marupurupu ni kazi bure. Labda tatizo linakuja pale ambapo uzalishaji wetu hauendani na matumizi yetu. Unataka ng'ombe akupe maziwa, wakati humhudumii vya kutosha, utapata wapi?

Viongozi wetu ni kama aliens kutoka kwenye sayari zingine, hawaishi na jamii kuona matatizo ya msingi ya jamii, labda pia hatuna vipaumbele, ndio maana ni rahisi mno watu kudai mishahara mikubwa wakati output hakuna.

Why even pay leaders who are always on the move exploring the world, dosing, doing nothing? what is the country getting out of them?
 
Mzalendo, nahisi adrenalins zangu zimepata hitilafu ghafla. Zimepanda na kumwagika!!

ooooh now i understand, i understand. Pesa kweli ni shetani.

Mkuu...
Ndiyo maana walisemaga kuwa... "what you dont know wont hurt you"!and "ignorance is bliss!" hawakukosea..
Now that you know..kubali maumivu tu...
 
"Mkuu Yo Yo, ya Zito yametosha, jee kwa kila kitu Zitto ndio awe "punching bag". Unadhani kama wale wabunge wote wangejali maslahi si wangesema kuhusu hili. Kwanza kumbuka wakati wa ukame 2006 walipoingia tu Bungeni walitaka kuongezewa marupurupu, kama sio kelele za wananchi ungekuta muda ule ule wameongezewa. Japo nahisi ndani ya hii miaka mitatu watakuwa wameongezewa....."

********************

MFUMWA: Yo Yo ana hoja kuhusu Zitto, kwani huyu Bwana, ambaye kapachikwa jina la "Dowans" amejijengea uwezo wa kuyatazama masuala ya ufisadi kama vile yana masilahi ya taifa. Inawezekana kuhuisu hili tena akawa tayari kupingana na viongozi wenzake ktk Chadema kwamba malipo ya milioni 84 kwa mwaka kwa Mbunge yana masilahi kwa taifa! Kwani ku-spin hoja si kazi kubwa tena siku hizi hasa kama Spin Doctor huyo anapata msukumo muafaka.

Nasema haya kwa sababu sasa hivi hata Ngeleja kamuachia Zitto ulingo kwani waziri huyo kasema mjadala wa Dowans na ufungwe.
 
Sasa nyie mlitaka wakale wapi? Mbona wazungu wanatuibia kila siku, tutaishia kusema hivihivi kila siku.

Hawa tunawachagua wenyewe, tena wanakuja kutunyenyekea na tunawapa kula, halafu tunalalamika kwa yale wanayoyafanya wakati wanastahili kwua watumishi wetu!

Paka keshaota makucha na anatawala nyumba, hatuwezi kumtoa
 
JF,

Mshahara na marupupupu ni milioni 7 kwa mwezi! Bado vikao vya kamati na maslahi mengine!

Kwa mwaka Mbunge hupata Shilingi milioni 84!

Na akimaliza mda wa miaka mitano hupata milioni 30 kama kifuta jasho!

Mwal Msingi hulipwa 150,000 kwa mwezi na kwa mwaka hupata 1,800,000! Hebu angalia tofauti ni shilingi 82,8000,000 kwa mwaka!!!

Uwiii !!!!! Jamani hii tofauti kwa nchi maskini ni kubwa mno!!!

Ndo maana rushwa ktk uchaguzi haitaisha!

Hivi Jaji Mkuu, Spika, Raisi na PM kuna mtu ana data wanalipwa kiasi gani tz?

Source: Slaa akiongea Hedaru Bunge mradi wa ulaji

Dk Slaa anamsaka Spika Sitta na Kamati yake ya Maadili ya Bunge. Wenyewe huwa hawataki mambo yao ya maslahi yawekwe kwenye public.

Dk. Slaa, Je, unao uwezo wa kuhimili rungu la Spika na Kamati ya Maaadili? Asante kwa kutujuza na rungu likikushukia bado tuko upande wako; usijali songa mbele.
 
Ibrah,
Tena hapo spika atamtoa macho slaa, nakumbuka kikao kimoja waziri mkuu walikuwa anajibu kuhusu matumizi ya magari ya fahari kupunguzwa, coment ya spika ilikuwa nanukuu "Jamani haya yetu msiyaguse, yaani spika atembee kwenye mahindra" mwisho wa kunukuu, unaweza kuona jinsi hawa jamaa walivyo wabinafsi tena mafirauni kabisa

Eee mola tumekosanini sisi Wadanganyika
 
Ndugu wana-JF, mabibi na mabwana. Kwa heshima na taadhima naomba kutamka kwenu kwamba nataka kugombea ubunge kupitia JF. Sababu kubwa inayonisukuma kufikia hatua hii ni MSHIKO mnene kule ndani ya nyumba na wala si matatizo yenu wala njaa niliyo nayo.

Tafadhali wandugu, naomba tu mnipe sababu au michango ya mawazo ya kwanini NISIGOMBEE nafasi hii ilihali pesa zipo kama zilivyoanishwa kwenye vyombo vya habari. Naomba kuwasilisha na aksanteni kwa kunisikiliza.
 
Ndugu wana-JF, mabibi na mabwana. Kwa heshima na taadhima naomba kutamka kwenu kwamba nataka kugombea ubunge kupitia JF. Sababu kubwa inayonisukuma kufikia hatua hii ni MSHIKO mnene kule ndani ya nyumba na wala si matatizo yenu wala njaa niliyo nayo. Tafadhali wandugu, naomba tu mnipe sababu au michango ya mawazo ya kwanini NISIGOMBEE nafasi hii ilihali pesa zipo kama zilivyoanishwa kwenye vyombo vya habari. Naomba kuwasilisha na aksanteni kwa kunisikiliza.

- JF ni nyumba ya great thinkers na sio anything else, tuheshimu hilo.

FMES!
 
Mimi kilichonishtua ni kujua kuwa kumbe wabunge wetu wanalipwa lita 1,000 za mafuta kila mwezi na kwamba kila lita ya mafuta inahesabiwa kununuliwa kwa Tshs 2,500/= kitu ambacho si sahihi hata kidogo.

Usafi unaanzia nyumbani, nadhani katika hili sikubaliani nao hata kidogo.

Kingine kilichonishtua ni kusikia nyumba anayokaa Spika wa Bunge inalipiwa kodi $7,000.00 kwa mwezi.

Hili nalo limenishtua kwani ni wazi kwa mwaka ni $84,000.00 ikimaanisha baada ya miaka 5 basi serikali inakuwa imekwishalipa $420,000.00 ambayo ingetumiwa vema ingeweza kujenga nyumba ambayo viongozi wote wa Bunge kwa miaka ijayo wangekaa bila kutuingizia gharama zisizo za lazima. Nahisi nyumba hiyo ina viti vinavyofanya massage automatically (kama ipo Dar).
 
- Hivi unajua mkuu kuwa RA anaishi kwenye nyumba kubwa ya serikali maalum kwa uwt?

- Only in Tanzania mkuu! usishangae ya musa maana mengine huyajui!

FMES!
 
Ole wao - mapesa hayo yangetosha kujenga hospital vijijini, kujenga shule, kununua chakula kwenye shule za serikali, kuajiri na kulipa waalimu wetu vizuri, madaktari, kutengeneza miundo mbinu etc.

Lakini wameamua kuchota na kula wenyewe ndio maana Wageni wanakuja kuchota rasilimali zetu - wala hawaoni kwani wako busy kulipana fedha itokanayo na jasho la walipa kodi

- SASA TUFANYEJE JAMANI??? WE NEED A SOLUTION - NANI ANAWAPANGIA INCOME YAO? AU NI WAO WENYEWE?? GOD INTERVENE THIS SITUATION ITS HURTING -
 
- Hivi unajua mkuu kuwa RA anaishi kwenye nyumba kubwa ya serikali maalum kwa uwt?

- Only in Tanzania mkuu! usishangae ya musa maana mengine huyajui!

FMES!

Akikaa nyumba ya serikali sio tatizo....labda tufahamishe hio nyumba iko wapi...
Nijuavyo RA kanunua nyumba DOM anakaa kila akifikia huko na watu watu wake wa karibu...(ukinisahihisha ntakubali, may my source is wrong)

Tutashangaa kama RA anakaa nyumba ya private...then GOT ije kulipia!!!..like Spika(as per MAX above) ...ndio kitu ambacho tumekipigia kelele GOT kuuza nyumba zake..huku watendaji wakikaa ktk Hoteli na kuliingiza Taifa Hasara.
 
- Mkuu ulikuwa hujui kwamba viongozi kama yeye wanakuwa na nyumba mbili between Dar na Dodoma?
 
Back
Top Bottom