Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Mishahara ya viongozi wa Tanzania

Wapewe tu, mbona wenzao wa UK wanalipwa Pound 64,766/= kama Tsh 127,893,795.80 bila kodi na ukizingatia hili ni Bunge la kuigwa mfano na ni la Commonwealth. While now wanalipwa only Tsh 156,000,000/= hii ni pamoja na floating, sitting, enterteinment, takrima poshoz.


Summary of current rates with effect from 1 April 2008

Members' parliamentary salary £63,291 from 1 April
Allowances
Staffing Allowance Maximum of £100,205
Incidental Expenses Allowance (IEP) Maximum of £22,193
IT equipment (centrally provided) [worth circa £5,000]
Pension provision for Members' staff 10% of employee’s gross salary
London Supplement £2,916
Additional Costs Allowance Maximum of £24,006
Winding up Allowance Maximum of £40,799
Communications Allowance Maximum of £10,400
Car Mileage (per mile) 40p (for first 10,000 miles)
25p (after 10,000 miles)
Bicycle allowance (per mile) 20p
Motorcycle allowance 24p

Sasa mtaalam wa kujumlisha na kubadilisha fedha afanye totalization na comparison ya kile wanachopata pale B.... opps Mjengoni
This factsheet is available on the internet at:
Page could not be found | Houses of Parliament
ons_and_archives/factsheets.cfm

What about their GDP?

Na wafanyakazi wengine walipwaje wa huko huko UK? huoni ni aibu kila kukicha mnatembeza bakuli kuombeleza, afu mnataka kujilinganisha na wale ambao mnaenda wapigia magoti wawasaidie?


UNASAHAU TU NDUGU, KWAMBA UKIMUIGA TEMBO.. UTAPASUKA MSAMBA!
 
Jamani tanzania! Mumeona wapi mtu kaajiriwa lakini ana jipangia mshahara mwenyewe? Huu ndiyo ubovu wa system ya tanzania. Wabunge si wameajiriwa na wananchi? Why shouldn't the people have a say in their pay.

Sijawahi kuona mtu ameajiriwa akaji pangia malipo mwenyewe, labda ndiyo maana watu wana kimbilia ubunge. Mambo haya only in tanzania!
 
Jamani tanzania! Mumeona wapi mtu kaajiriwa lakini ana jipangia mshahara mwenyewe? Huu ndiyo ubovu wa system ya tanzania. Wabunge si wameajiriwa na wananchi? Why shouldn't the people have a say in their pay. Sijawahi kuona mtu ameajiriwa akaji pangia malipo mwenyewe, labda ndiyo maana watu wana kimbilia ubunge. Mambo haya only in tanzania!

Mwajiri yuko hoiiii bin taabani..mwajiriwa anadai kupandishwa mshahara kwa viwango vya kutisha...na hasubiri mwajiri afikiri na kuamua bali hukwapua hazina ya mwajiri Bila woga wala haya! mwajiri kabaki mdomo wazi afanye nini?
 
Siwezi kuchangia ktk hili in any way, kama hiyo mishahara ya hawa watu bado inabaki kuwa siri.

Sioni maantiki. Aijuaye atuwekee hapa.
 
Wewe Pinda usitupindishe ulaghai wako. utalinganisha mishahara ya wabunge na wafanyakazi wengine wa umma kweli.

Nadhani nawe umeshaanza kulewa madaraka. kwa kipi cha ajabu wanachotufanyia wananchi mpaka wanastahili mishahara mikubwa hivyo. niambie walimu na manesi wanalipwa kiasi cha kulingana na wabunge. walimu na manesi ni watu ambao wanastahili malipo zaidi kwani kazi wanayoifanya kwa kweli ni nzito kulinganisha na wabunge wako kazi kufanya umalaya bungeni hawana lolote.

Viongozi wa tanzania amkeni naona bado mmelala usingizi. Hizi ziara za hapa na pale zinafanya na akili nazo zinabakia huko mnakokwenda.
 
Slaa atakumbuka siku zote kwa hoja zake tata ambazo hakuna shujaa anazirukia kwa urahisi .Slaa wewe ni shujaa pekee ambaye husema unayo yaamini na uweli mtupu lakini inakuwa mwiba kwa wenzio.

Pinda umepoteza touch na wananchi kabisa .CCM na uchaguzi mkuu tuta hoji sana juu ya mishahara
 
Date::5/1/2009
POSHO ZA WABUNGE:Wafanyakazi Dar wamuunga mkono Slaa

Winfrida Mtoi
Mwananchi

WAFANYAKAZI wa Mkoa wa Dar es Salaam, wameunga mkono hoja ya Mbunge wa Karatu, Dk Wilbrod Slaa kwamba mawaziri na wabunge wanalipwa mishahara mikubwa na ya kutisha.

Walisema hali hiyo pia , inachochea ufisadi na utovu wa nidhamu kazini.

Kauli ya wafanyakazi hao imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutetea wabunge kuwa wanalipwa mishahara midogo.

Kauli hiyo ya wafanyakazi, iko katika risala yao ya kudhimisha sherehe za Mei Mosi zilizofanyika jana.

Walisema kila waziri na mbunge ana malipo yasiyopungua Sh12 milioni kwa mwezi, kiwango ambacho kwa mfanyakazi wa kima cha chini ni sawa na mshahara wa miezi 144 au miaka 12.

"Mfano mbunge au waziri ana malipo si chini ya Sh milioni 12 kwa mwezi kwa mujibu wa marekebisho ya sasa, malipo hayo ni mshahara wa miaka 12 kwa mfanyakazi wa kima cha chini," alisema Katibu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), mkoani Dar es Salaam Everist Mwalongo.

Risala hiyo ilisomwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi.

Mwalongo alisema kima cha chini cha mfanyakazi wa sekta ya umma ni Sh101,480 na sekta binafsi ni Sh65,000.

Alielezea mazingira hayo ya kuwepo kwa pengo kubwa la kiwango cha mishahara, kinawakatisha tamaa wafanyakazi.

Alisema kwa msingi huo kuna haja kwa serikali kushirikiana na vyama vya wafanyakazi katika kupanga upya kima cha chini.

Mwalongo alisema kima cha chini kinacholipwa ni kinyume na katiba ya nchi na sheria ya kazi na kwamba pendekezo lao Tucta ni angalau kifikie Sh315,000 kwa mwezi.

"Kuendelea kulipa mshahara wa sasa licha ya kwamba haitoshi ni kukiuka katiba ya nchi na sheria za kazi, pia kukaribisha mianya ya rushwa, wizi na ufisadi kwa baadhi ya wafanyakazi, jambo ambalo limeanza kuchafua sifa nzuri ya nchi yetu," alisema.

Akijibu hoja hiyo, Lukuvi ambaye pia ni Mbunge wa Ismani mkoani Iringa, alisema risala hiyo ni ya kisiasa zaidi na kwamba wabunge na mawaziri hawalipwi mishahara kwa kiwango walichokitaja.

Alisema yuko tayari kuwakaribisha wafanyakazi ofisini kwake ili washuhudie hati za malipo ya mishahara ya ubunge.

Hata hivyo, alikiri kuwa wabunge na mawaziri hupata posho nyingi kwamba hiyo inatokana na nafasi za kazi wanayoifanya.

"Suala la posho lisiwasumbue kwa kuwa kila mtu anakula mezani kwake lakini hata hivyo hawafikii kiwango hicho cha milioni 12," alisema Lukuvi.
 
Kila mtu anakula mezani kwake? what the hell!.. na wale wanaokula kwenye meza za watoto wetu nao? Tena kula kwa mikono miwili?
 
Yes mbunge wa Sierra Leone hulipwa mshahara na marupurupu yasiyozidi Dola 2,000 kwa mwezi, hata wengine hawana magari huenda ofsini kwa baiskeli!
 
upuuzi mtupu!! hivi wanadhani sifa? sikio la kufa halisikii dawa, CCM ndo walipofikia sasa, ni kama hawasikii...
 
Kuunga mkono kwa mdomo/risala tu!! Si wa copy na ku paste angalau zile mbinu za Wazee ya defunct EA
 
Mi nshawaambia 2010 watz tugome kuongozwa na CCM.
 
Hawa wanafikiri lakini kama iko siku wananchi watachoka na watadai haki yao kwa kuingia maungoni - wanataka kuipeleka nchi kubaya kwani ikiwa ni wachache tu wanaofaidi keki ya Taifa basi mwisho wake si mwema.
 
Kila mtu analia mezani pake?

Hiki ni kiburi na kulewa madaraka. Mshahara wa ukuu wa mkoa yeye, na mshahara wa ubunge yeye hapo weka nje posho na marupurupu mengine yaambatanayo na nafasi zake hizo mbili. Sitashangaa ukijumlisha income yake yote kwa mwezi ni zaidi ya 10Millions au hata zaidi ya waziri.

Unategemea huyu ndo awe mtetezi wa wanyonge bungeni? SAHAU! Na uliza akiingia ofisini anafanya nini? Kwanza mchelewaji na hakuna wa kumuuliza! WIZI MTUPU!
 
Ufumbuzi wa uroho wa wabunge ni kugunguza kama sio kufuta kabisa mishahara na kuwakilishwa na wabungwe wa kujitolea. Sheria ya wagombea binafsi nayo iruhusiwe ili kupunguza makali ya kulindana miongoni mwa vyama vya kisihasa hususan chama twawala (CCM).

Umefika wakati kwa taasisi za kiraia kuendesha vuguvugu ili kuwahamasisha watanzania waandamane kudai wabunge wa kujitolea na haki yao ya kuwa na wagombea binafsi. Watishie hata kugoma kupiga kura mwakani iwapo maombi yao haya hayatafanyiwa kazi, vyama haviwezi kujichagua vyenyewe.
 

"Suala la posho lisiwasumbue kwa kuwa kila mtu anakula mezani kwake lakini hata hivyo hawafikii kiwango hicho cha milioni 12," alisema Lukuvi.

Eti Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam penye makao makuu ya kila sehemu
 
Lukuvi atueleze kwanza uliko mradi wa mabasi ya wanafunzi kabla hajaanza kubwabwaja hapa .
 
Wananchi tumechoka, tena tumechoka sana.
Wengine tulichoka tangu siku tulipo anza pata mawazo ya kutafuta huku ughaibhuni.

Tatizo kubwa kwetu sote ni haka kajini MAhaba kanaitwa AMANI NA UTULIVU.
Maana yake kuwaandoa wakubwa kwenye meza zao ni kuondoa amani.
Kama unafanywa mjinga au unafyonzwa, fonzwa huku umetulia.

Amani inalindwa kwa mtutu wa bunduki, kwa lugha nyingine Amani inapatika kwa mtutu wa bunduki.

Ni mpaka hapo Kigagula wa kutupunga huyu jini mahaba wetu akipatika ndipo tutawaaangukia kwa nguvu zetu zote.
 
Back
Top Bottom