Misri wameisaidia pakubwa Israel kupigana na Hamas. Bila msaada huo pamoja na mataifa makubwa ya Ulaya, Israel ingekimbia vita mapema

Misri wameisaidia pakubwa Israel kupigana na Hamas. Bila msaada huo pamoja na mataifa makubwa ya Ulaya, Israel ingekimbia vita mapema

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Vita vya Gaza vitaendelea kuwa ni vita vibaya kuwahi kupigananwa duniani kati ya maadui wawili wenye nguvu zinazopishana sana na bado ikashindikana kupatikana mshindi kwa muda mrefu.

Gazeti la Haaretz limetoa siri kwamba Misri imekuwa ikitamka hadharani kuwa ina uhasama na Israel kuhusiana na vita vya Gaza lakini kiundani utawala wa nchi hiyo umefanya njama na Israel kuiachia iipige Hamas wakihofia nguvu za Hamas kubaki na kuingia nchini Misri.

Baadhi yetu tulishawahi kutilia shaka namna Israel ilivyoweza kupeleka vikosi mpaka kwenye lango la kuingia Gaza huko Rafah bila upinzani wa maana kutoka Misri. Muda mfupi baada ya hapo jeshi hilo la Israel likaweza kuuchukua ukanda wote wa Philadephi ambao ndio mpaka pekee Gaza unaopakata na taifa la nje mbali na Israel.

Kwa maana hiyo Misri itakuwa haikuhusika na kupigwa kwa kundi la Hamas peke yake bali na mauwaji ya maelfu ya wapalestina na uharibifu wa eneo lote la Gaza ambapo uharibifu wake unazidi hata ule uliotokea maeneo ya Bakhmut na Mariupol nchini Ukraine.

Kudhihirisha kuwa Hamas na wenzao hawapigani na Israel peke yao ni kuwa hata sasa nchi tano za Ulaya na Markani zimeendelea kupinga hukumu ya mahakama ya ICCJ inayotaka Netanyahu akamatwe na kushitakiwa.

Wapiganaji hao wa Gaza wamekatiwa misaada yote ya silaha na chakula lakini la kushangaza mpaka sasa hawajasalimu amri na wanaendelea kupigana.
 
Mashariki ya kati itakalika siku ambayo Iran & Saudi Arabia 🇸🇦 watakaporudisha mahusiano ya moja kwa moja ya kidiplomasia. Na huo utakuwa mwisho wa Israel na mashoga zake wanaoteteresha amani ya ukanda ule.
 
Ulitaka Misri awe upande wa Hamas mchana kweupe? Subiri Trump aingie madarakani uone na uelewe vzr atakachokifanya hapo middle East maana atakuwa hana cha kupoteza sababu hata gombea tena urais
 
Bado nchi yako tu sasa kuitaja juu ya msaada wa kivita huko Israel

Na huwenda mpaka Gaza wameisaidia Israel kupigana na Gaza
 
Mashariki ya kati itakalika siku ambayo Iran & Saudi Arabia 🇸🇦 watakaporudisha mahusiano ya moja kwa moja ya kidiplomasia. Na huo utakuwa mwisho wa Israel na mashoga zake wanaoteteresha amani ya ukanda ule.
Shida ya Mashariki ya Kati ni Uislam/utawala wa Iran

Wanaamini kila nchi ya Mashariki ya Kati inatakiwa iwe na mapinduzi kama ya Iran na Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah awe mkuu wao.

Hili kufanikisha Hilo lazima falme zote za Middle East zife
 
Sorry, Naombeni site ya kudownload full movie free za makampuni ya movie kama universal pictures
 
Nasikia zilitengwa kama 200b kufadhalia ule uhasi pale misri kutoka usa kwa jeswish ili maandamano ya kuvuruga misri yasambse
Morsi hakuwa kipenzi Cha USA na wenzie,maana ni pro Islam na Palestine,alikua Muslim brotherhood,hiyo ni hatari kwa Israel,so jeshi likapora mamlaka
 
Sorry, Naombeni site ya kudownload full movie free za makampuni ya movie kama universal pictures
Sidhanii kama mahala pake ila muda kidogo nilikua natumia u torent sijaitumia muda sijajua kama bado ipo inatumika ama laaa
 
Back
Top Bottom