Misri yagundua mji uliokuepo miaka 3,000 iliyopita

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Wataalamu wa historia ya nchini Misri wamefanya ugunduzi wa kushangaza wa mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 3,400 wakati wa muda wa farao.

aa020c23-5114-4053-8402-b5214bdcb2f5.jpeg

Uzinduzi huo umetajwa kuwa muhimu tangu kugunduliwa kwa kaburi la kale la Tutankhamun.

Wana akiolojia hao ambao walikuwa wakitafuta hekalu katika eneo la jangwa karibu na mji wa Luxor. Lakini wakaanza kugundua jambo lingine, ukuta wa nyumba ambazo zilionekana kila upande.

Kulikuwa na vyumba vilivyokuwa na vitu ambavyo Wamisri wa kale walikuwa wakitumia kila siku katika maisha yao.

Pete na vyungu vilivyochorwa kwa rangi na kugongewa muhuri wa farao aliyekuwa na nguvu kubwa nchini humo .

Kulikuwa na duka la kuuza mikate katika eneo la jirani ambapo ushahidi wa maandalizi ya chakula cha watu wengi yalionekana.

Sehemu nyingine kulikuwa na ishara ya shughuli za kiwanda.

Inaonekana kuwa wakazi wa eneo hilo walikuwa wanajishughulisha kutengeneza mapambo ya maeneo ya kuzikia na hekaluni.

Uzinduzi huo ulikuwa na taarifa nyingi hata kuhusu majibu ya kwanini eneo hilo lilitelekezwa na watu wake.

Ugunduzi huu ni jambo muhimu sana katika historia ya Misri na wataalamu wake wa akiolojia.

Mji huu uliohifadhiwa vizuri umeelezewa kuwa kumbukumbu ya historia ya Misri.
 
Tutankanum aliwasumbua sana wana Historia kupata majibu yake, jamaa alikuwa na tatizo la genetic kutokana na baba yake kuwa ni ndugu ya mama yake
 
🤣 ila watu wanajua kutafuta hela! Haya na si tutakuja kugundua fuvu la funza wa kwanza tupeni muda kiduchu tu.
 
mkuu, hata hapa Bongo umewahi kugundulika mji wa watu walioishi kabla ya kuzaliwa kwa yesu, upo chini ya maji, zamani watu waliishi kawaida tu lakini baada ya miaka mingi maji ya bahari yakaja
subiri nitafute picha zake niweke hapa
 
Leta lkn hawa ndugu sometimes huwa wanaturusha stimu ili wapige hela tu maana mnaweza jikuta kila siku mnatafuta lkn hata miaka 20! Na hampati kitu zaidi ya kutumia gharama zenu ambazo hazirudi Sasao ndo linakuja swali la tufanyaje..🤣

Sidhani Kama wote wanakuwaga wakweli..
 
ni kweli mkuu lakini pia utafiti wa haya mambo licha ya kuhitaji pesa inahitaji uchawi mfano kule Misri farao kaacha rahana kwa yeyote atakayesumbua maiti yake, wamekufa wazungu wengi
za Hapa Tz hizi hapa
IMG_1318.JPG
 
ni kweli mkuu lakini pia utafiti wa haya mambo licha ya kuhitaji pesa inahitaji uchawi mfano kule Misri farao kaacha rahana kwa yeyote atakayesumbua maiti yake, wamekufa wazungu wengi
za Hapa Tz hizi hapaView attachment 1747975
Kama utaweza tuletee uzi kuhusu haya mambo mkuu nimekuwa interested na hako kakionjo ka misri nataka nijue changamoto zao n.k
 
Kwamba miaka yote hiyo tuseme hakuna aliyewahi kufika huko? Au ndiyo yaleyale ya Livingstone kugundua Lake Victoria wakati wasukuma walikuwepo......
 
ni kweli mkuu lakini pia utafiti wa haya mambo licha ya kuhitaji pesa inahitaji uchawi mfano kule Misri farao kaacha rahana kwa yeyote atakayesumbua maiti yake, wamekufa wazungu wengi
za Hapa Tz hizi hapaView attachment 1747975
Farao yupi mkuu,? Hivi unajua kuwa farao sio jina la mtu Bali ni cheo,ni sawa na wewe kusema rais wa Tanzania alisema kuwa atakayejishughulisha na mwili wake atalaaniwa,rais yupi sasa utakuwa unamaanisha,Nyerere ,mkapa au Magufuli?
 
Najua mkuu, ni pharao ramesses wa pili, huwa mara nyingi hatumtaji jina kwa kuwa yeye ndio pharaoh maarufu zaidi wa wote
Ahsante kwa marekebisho
 
Back
Top Bottom