Miss Tanzania 2009 aswekwa rumande

Miss Tanzania 2009 aswekwa rumande

sasa ndo atoboe matairi ya usafir wa mwenzie bila haya.......

huo ndio usafiri alokuwa anatumia kwenda kwa yule demu wake mwingine. sasa ili kukomesha tabia hiyo aliamua kuyapiga msumari matairi ya swala yake. unazikumbuka baiskeli za swala shem?
 
Hawana majina? kwa makosa gani? mahakama gani ya mwanzo ya mwisho ya kati? kama hujui kitu bora usibandike vitu nusu nusu.

Miss tz 2009. Kashambulia na kuharibu mali amekosa wazamini yuko segerea
 
huo ndio usafiri alokuwa anatumia kwenda kwa yule demu wake mwingine. sasa ili kukomesha tabia hiyo aliamua kuyapiga msumari matairi ya swala yake. unazikumbuka baiskeli za swala shem?

hahaaaaa shem nazikumbuka!!!

sas kamani hivyo YOYO kakosea mbona hapo miss tz kaonesha tu anampenda sana na hataki kushea na mwingine!!!
 
Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald na Boyfriend wake Kenedy amepandishwa kizimbani leo kwenye mahakama ya Wilaya Kinondoni akishitakiwa kwa kosa la kufanya vurugu na kuharibu mali za bendi ya Volcano Sound inayomilikiwa na mwanamuziki Taji Mbaraka mtoto wa Marehemu Mbaraka Mwishehe kwenye ukumbi wa TPDC Mikocheni.


Kesi hiyo iliyofunguliwa Oysterbay na ilikuwa na jalada na OB /RB/2267/010 KUHARIBU MALI NA SHAMBULIO imesomwa leo katika mahakama hiyo na mshitakiwa Miss.Miriam amewekwa mahabusu ya mahakama hiyo baada ya kukosa dhamana, kesi imaeahirishwa, hata hivyo ndugu na jamaa wanahangaika ili kuhakikisha anapata dhamana kabla muda wa kuwachukua mahabusu kutimia ili kuweza kumnasua na kupata dhamana, bado haijafahamika kama ataweza kutimiza masharti ya dhamana na kufanikiwa kupata kwa leo au la.


Kimsingi kama Miriam atapatikana na hatia hii itakuwa ni jambo baya kwa mrembo huyo anayeshilikila taji la Miss Tanzania 2009/2010 kwakuwa mrembo huyo aliaswa na wadau mbalimbali wa urembo kuwa balozi mwema kwa Nchi, jamii na kwa kamati ya Miss Tanzania .


From Michuzi JR
 

Attachments

  • 8.jpg
    8.jpg
    23.7 KB · Views: 45
muache akasherekee valentine segerea-wanalewa sifa hawa mamiss wetu,kwani kweli ni warembo,basi wanakuwa walewa sifa za kijinga.
 
Sasa cc tumsaidiaje kama ameshindwa kutuliza hasira yake. MWACHE TU!
 
Sasa huyu bi Mariam atakosaje mdhamini wakuu? Kwani Hashim Lundenga na wenzie, si ndio wadhamini wenyewe?
 
Ameweka rekodi/historia...Miss Tz wa kwanza kusherehekea valentine lupango!
 
hivi hawa mamiss wa Tz wana nini jamani? mbona utulivu hawana kabisa, maana kila miss amakuwa na vituko vyake, huwa wanatolewa wapi hawa?

Tatizo ni kuiga kila kitu eti ni maendeleo na hao ndio wanazawadiwa magari tujitazame hivi ipo kweli haja ya kuwa na mashindano ya urembo kama matokeo yake ni hayo ? Kila mmoja na vituko vyake
 
Hebu msome EX-PASTER uone madhara ya kukaa uchi. Mashindano ya kishetani yanaleta tabia za kishetani
 
Ni haka kapya kajuzi juzi hata Miss World sijui kama kameshaenda tayari huu ndo umaarufu wa kijinga

Miss World ya 2009 kaenda na hakuambulia chochote!..Kajiwekea doa kweli kwenye hii issue!..
 
02_10_c4fhp4.jpg
Miss Tanzania 2009, Miriam Gerald akiongozwa na Polisi kuingia katika mahabusu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni Dar es Salalaam jana alikpofikishwa pamoja na rafiki yake Kennedy Victor kusomewa mashitaka ya kushambulia na kuharibu mali. Miriam alipelekwa mahabusu kwa kukosa mdhamini. (Picha na Mroki Mroki).
 
Back
Top Bottom