Miss Tanzania avuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Miss World kutokana na utovu wa Nidhamu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Miss Tanzania 2020-2021 Rosey Manfere hajatangazwa kwenda kushiriki Miss World 2021 na badala yake ametangazwa mshindi wa pili Juliana Lugumisa kutokana na utovu wa nidhamu kati ya Miss Tanzania Rosey na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania.

=====


 
Waweke wazi taratibu walizotumia mpaka kufikia hapo na sio statement za jujuu tu, hawa watu walishaonyesha walakini toka waanze kuwapa washindi gari used choka mbaya kama zawadi!!
 
Huyo number mbili mbona havutii, nadhani shindalo la miss Tanzania lipate waandaji wapya tu chini ya basila amekuwa anatoa washindi wabovu na nilimuona akimpromote huyu mshindi wa pili probably ana interest naye.
 
"UTOVU WA NIDHAMU"
πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Hicho kusingizio Cha utomvu wa nidhamu design ya kumuonea wizara ya habari Sanaa itolee ufafanuzi na haki itendeke kwa mshindi wa kwanza, maana basila naye alikuwa na tuhuma zake ukute dada alikataa kunyanywaswa Sasa wakasingizia nidhamu.
 
Waweke wazi taratibu walizotumia mpaka kufikia hapo na sio statement za jujuu tu, hawa watu walishaonyesha walakini toka waanze kuwapa washindi gari used choka mbaya kama zawadi

Dada wa watu hakutaka kuliwa kimashara akaamua liwalo na liwe kwanini kuachiwa miwaya wakati ana safari ndefu ya kujijenga kimaisha.
Labda aliliwa kimasihala akapata mimba na hataki kuitoa,
 


Mrembo anayeshikilia tajia la Miss Tanzania 2020 -2021, Rose Manfere, amevuliwa uwakilishi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia.

Hatua hiyo imechukuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya kugundua baadhi ya tabia za mrembo huyo ambazo zitakuwa kikwazo cha kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Taarifa za Kuaminika ambazo Mtanzania Digital imezipata kutoka kwenye Kamati ya Miss Tanzania, zimeeleza kuwa:

"Mrembo ambaye anatakiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi anatakiwa awe na tabia njema kuanzia hapa nchi na kufuata kanuni na taratibu za mkataba wake nakwamba akikiuka kamati inatakiwa kuchukua hatua zinazostahili," kimeeleza chanzo hicho.

Aidha, kimeongeza kuwa, nafasi hiyo amepewa mshindi wa pili wa Miss Tazania 2020-2021 Juliana Rugumisa(Mwenye nguo ya rangi ya chungwa) ambaye kamati imeona ana faa kuwa mwakilishi wa taifa.

Shindano la miss World mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico mwishoni mwa mwaka huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…