Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Miss Tanzania 2020-2021 Rosey Manfere hajatangazwa kwenda kushiriki Miss World 2021 na badala yake ametangazwa mshindi wa pili Juliana Lugumisa kutokana na utovu wa nidhamu kati ya Miss Tanzania Rosey na waandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania.
=====
=====
View attachment 1852966
Mrembo anayeshikilia tajia la Miss Tanzania 2020 -2021, Rose Manfere, amevuliwa uwakilishi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia.
Hatua hiyo imechukuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya kugundua baadhi ya tabia za mrembo huyo ambazo zitakuwa kikwazo cha kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Taarifa za Kuaminika ambazo Mtanzania Digital imezipata kutoka kwenye Kamati ya Miss Tanzania, zimeeleza kuwa:
"Mrembo ambaye anatakiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi anatakiwa awe na tabia njema kuanzia hapa nchi na kufuata kanuni na taratibu za mkataba wake nakwamba akikiuka kamati inatakiwa kuchukua hatua zinazostahili," kimeeleza chanzo hicho.
Aidha, kimeongeza kuwa, nafasi hiyo amepewa mshindi wa pili wa Miss Tazania 2020-2021 Juliana Rugumisa(Mwenye nguo ya rangi ya chungwa) ambaye kamati imeona ana faa kuwa mwakilishi wa taifa.
Shindano la miss World mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico mwishoni mwa mwaka huu.