Miss Tanzania avuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Miss World kutokana na utovu wa Nidhamu

Miss Tanzania avuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye Miss World kutokana na utovu wa Nidhamu

hapa inatakiwa aite press atoe ushuhuda kwa nini kavuliwa taji hilo hapo ndiyo tutaona madudu ya waandaaji
 
Mrembo anayeshikilia tajia la Miss Tanzania 2020 -2021, Rose Manfere, amevuliwa uwakilishi wa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya Dunia.

Hatua hiyo imechukuliwa na kamati ya Miss Tanzania baada ya kugundua baadhi ya tabia za mrembo huyo ambazo zitakuwa kikwazo cha kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Taarifa za Kuaminika ambazo Mtanzania Digital imezipata kutoka kwenye Kamati ya Miss Tanzania, zimeeleza kuwa:

"Mrembo ambaye anatakiwa kupata nafasi ya kuiwakilisha nchi anatakiwa awe na tabia njema kuanzia hapa nchi na kufuata kanuni na taratibu za mkataba wake nakwamba akikiuka kamati inatakiwa kuchukua hatua zinazostahili," kimeeleza chanzo hicho.

Aidha, kimeongeza kuwa, nafasi hiyo amepewa mshindi wa pili wa Miss Tazania 2020-2021 Juliana Rugumisa(Mwenye nguo ya rangi ya chungwa) ambaye kamati imeona ana faa kuwa mwakilishi wa taifa.

Shindano la miss World mwaka huu linatarajiwa kufanyika nchini Puerto Rico mwishoni mwa mwaka huu.
Juliana Rugumisa(Mwenye nguo ya rangi ya chungwa) 🤷‍♂️🤷‍♂️🤷‍♂️
 
Itakuwa kawagomea kutoa tu.
Haiwezekani avuliwe bila sababu kuwekwa wazi.

Jpm. Wanyonge wanaonewa sasa. Awamu hii[emoji2089][emoji2089]
 
Na hapo kwenye tabia zisizofaa itakua ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Nilikua namsikia clouds fm kwenye kipindi cha njia panda wakiomba michango ya hali na mali ili kuwasaidia watoto wenye usonji
 
Back
Top Bottom